May 24, 2012

MTANGAZAJI WA CLOUDS FM LOVENESS aka DIVA CHINI YA LAMAR KUACHIA NGOMA(BONGO FLEVA)




Mtangazaji wa Clouds FM Loveness aka Diva anatarajia kujaribu bahati yake kwenye muziki wa Bongo Fleva kuona upande huo wananchi watampokeaje.

Diva ambaye hujiita ‘Mimi’ ni miongoni mwa watangazaji wanaozungumzwa zaidi nchini kwa mabaya  mengi na mazuri machache kutokana na aina ya utangazaji wake kwenye kipindi cha Ala za roho katika kituo hicho cha radio maarufu kwa burudani nchini kutokana na sifa yake ya kuongea mambo mazito ya kimapenzi bila kificho.

 Hizi ni baadhi za tweet
Diva aka mimi under xclusive muzik the lebal !soon to relize a hit song piga simu
Retweeted by
 
hey baby ,its 25th may 1988
My new song will be called Piga simu ft Diamond Platnumz .... Produced by Lamar
Working under fish Crab cooked out ,Lamar signed me. LOOL - money on ma mind. Whoop Whoop !!
Done wit Lamar .... Now we on the script of the video filmatic we be holding ya Diva down,Produced by Lamar#hit
Heading to lamar .... One more song :-) will be released next week , Diamond will Be the Perfect feature ! Stay tuned.
At Push Mobile , with DJ Nelly , business connect People.

DIAMOND :SHOW LIVE NDANI YA BIG BROTHER JUMAPILI

Msanii wa Bongo Flava Naseeb Abdul, aka Diamond,anayetamba na nyimbo zake za nimpende nani na Mawazo, anatarajia kupiga show katika shughuli ya eviction ya Big Brother inayosemekana itakua ni ya kipekee mjini Johannesburg, South Africa.
Msanii huyo anayetamba kuwa nominee wa MTV African Music Awards na tuzo kibao za Kilimanjaro Music Awards, ameondoka nchini leo kuelekea pande za madiba tayari kuwapa moto wa Diamond Platnumz Baby

PICHA NA MATUKIO YOTE KATIKA KESI YA MBUGE WA UBUNGO, JOHN MNYIKA

Mahakama Kuu ya Tanzania kanda ya Dar es Salaam, imemthibitisha John Mnyika kuwa ndiye Mbunge halali wa Jimbo la Ubungo, Dar es Salaam kwa tiketi ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo, CHADEMA.


Hakimu Pendo Msuya aliyeisoma hukumu hiyo alitupilia mbali madai yote matano yaliyowasilishwa katika keshi hiyo kwa kuwa upande wa mlalamikaji ulishindwa kuwasilisha ushahidi usio na mashaka kuhusu madai husika.


Kesi hiyo yenye namba 107 ilifunguliwa mwaka juzi na aliyekuwa mgombea kiti hicho kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi, CCM, Hawa Ng’humbi dhidi ya John Mnyika kupinga ushindi alioupata baada ya Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2010.




Madai hayo yalikuwa ni pamoja na:
  1. Mlalamikiwa kumtuhumu mlalamikaji kuhusika na kashifa za uuzwaji wa jengo la Umoja wa Wanawake (UWT)
  2. Kubadilishwa kimakosa kwa kura katika fomu za matokeo ya Ubunge
  3. Kuwepo kimakosa kwa watu katika chumba cha kuhesabia kura
  4. Matumizi ya tarakilishi ya mlalamikiwa wakati wa kujumlisha kura
  5. Ukiukwaji wa taratibu za kisheria katika uchaguzi ambazo zilisababisha kuwepo kura hewa 14,854

Baada ya hukumu kutolewa, wanahabari walimwuliza Ng’humbi ikiwa atakata rufaa ama la, ambapo alijibu kuwa bado hajaamua.








Naye Mwenyekiti wa CHADEMA, Freeman Mbowe, akitoa maoni yake mara baada ya hukumu hiyo kusomwa amesema, Mahakama imetenda haki lakini akawataka watu wote wanaopeleka kesi mahakamani kuhakikisha wanakuwa na ushahidi wa kuthibitisha madai hayo ili kuepusha kupoteza muda na gharama kubwa inayotumika katika kesi.

CHADEMA imepanga kufanya mkutano mkubwa wa hadhara siku ya Jumapili jijini Dar es Salaam. 

MFANYAKAZI WA NDANI ALIYETUHUMIWA KUMUUA MTOTO

Mfanyakazi wa ndani anayetuhumiwa kumuua mtoto wa mwenye nyumba katika eneo la Sinza Mori akiwa amewekwa chini ya ulinzi na majirani wa eneo hilo. Kulia ni mtangazaji wa Clouds FM, Gea Habib. 

May 22, 2012

SHOW YA MKASI JUMATATU HII

MUME WA MSANII WA FILAMU,JACK PATRICK ANASAKWA NA POLISI KWA MADAI YKUWA ANAUZA MADAWA YA KULEVYA



Stori: Makongoro Oging na Haruni Sanchawa
MUME wa msanii maarufu wa filamu nchini, Jack Patrick, Abdulhatif Fundikira anasakwa na polisi kwa madai kuwa anauza dawa za kulevya ‘unga’.
Uchunguzi wa gazeti hili umebaini kuwa Fundikira anasakwa baada ya mwanamke mmoja Mariam Mohamed Saidi,29, kudakwa na polisi wa Kitengo cha Kupambana na Kudhibiti Madawa ya Kulevya nchini ambapo amemtaja Fundikira kuwa ndiye mwenye dawa alizokamatwa nazo ambazo ilikuwa azisafirishe kuzipeleka Uturuki.
Uchunguzi wetu umebaini kuwa polisi walifika nyumbani kwa Fundikira saa 10 usiku wiki iliyopita lakini wakaambiwa kuwa hakuwepo, alikwenda kwenye msiba wa ndugu yake mikoani.
“Lakini hata mke wake hawakumkuta na hata walipopigiwa simu, zikawa hazipatikani na inavyoonesha wamepata fununu za kutafutwa na polisi hivyo kujikuta katika hali mbaya kila upende, wa dola na hata jamii,” kilisema chanzo chetu.
Gazeti hili lilimtafuta Kamanda wa Kikosi cha Kupambana na Kudhibiti Madawa ya Kulevya nchini, Godfrey Nzowa na kumuuliza kuhusu madai hayo naye alikiri kujua tukio hilo.
Akasema vigogo wa mtandao wa dawa za kulevya wamejulikana na kilichobakia ni kufuatilia nyendo zao na kuwadaka mmojammoja.
Akizungumza na mwandishi wetu wiki iliyopita ofisini kwake, Nzowa alisema kwamba orodha yao ni ndefu na kwamba Mei 16, mwaka huu kigogo mmoja akiwa na mke wake huko maeneo ya Buguruni Malapa wilaya ya Ilala jijini Dar es salaam walitoroka kwao baada ya kupata taarifa kwamba mfanyakazi wao anayewasafirishia ‘unga’ nchi za nje,Mariam Mohamed Said ,29, amekamatwa.
Kamanda Nzowa amesema kwamba Mariam alikamatwa Mei 16, saa 9 usiku, Uwanja wa Ndege wa Mwalimu Julius Nyerere akiwa na kilo 10 za bangi zenye thamani ya shilingi milioni 12 zilizofichwa kwenye sanduku ambapo mtuhumiwa huyo amedai kwamba amekua akifanya biashara ya baibui.
“Uchunguzi unaonesha kuwa inawezekana isiwe ni biashara ya bangi tu bali hata aina nyingine ya dawa za kulevya wamekua wakisafirisha,” alisema.
Mariam alikamatwa akiwa na bangi mabunda 23 yaliyofungwa kitaalam wakati akijiandaa kupanda ndege ya kwenda Uturuki na alionyesha nyumba ya kifahari ambayo ina chombo maalum cha kunasa picha, CCVT.
Kamanda Nzowa alifafanua kwamba Mariam atafikishwa mahakamani wakati wowote upelelezi ukikamilika.
Hata hivyo, alikataa kutaja majina ya vigogo waliotoroka kwa madai kuwa ataharibu uchunguzi na amewaomba wananchi kuendelea kutoa ushirikiano kwa jeshi la polisi.

AY na MARCO CHALI WAWASILI JOHANNESBURG KUSHOOT VIDEO




Rapper, mwanamuziki na mjasiriamali wa Tanzania Ambwene Yesaya akiwa na producer Marco Chali wa Mj Records leo asubuhi wamewasili mjini Johannesburg nchini Afrika kusini kushoot wimbo wa msanii huyo.

Katika mtandao wa twitter AY ameandika “In Johannesburg wit @Marcochali..Cool weather..ready 2 shoot my new video with @I_Am_Godfather cc @ArthurSamTz@Murunga_Josh”

Video hiyo ambayo imedaiwa itagharimu dola za  marekani 20,000 ambazo ni zaidi ya shilingi milioni 31 za kitanzania itafanywa na kampuni iitwayo Godfather Productions ya Afrika kusini inayomilikuwa na Micheal Uche Ogoke.

Kwa mujibu wa Ogeke aka Godfather, shooting ya video hiyo itafanyika alhamis hii mjini Johannesburg.

Kampuni hiyo imeshafanya video za P Square na Flavour wa Nigeria na wiki hii ina ratiba ya kufanya video nyingine ya kundi la P-Square mjini Johannesburg na Capetown.
    imenadaliwa na leotainment.blogspot.com

YOUNG BUCK THROWN OUT FROM HIS TENNESSEE MANSION

Young Buck Thrown Out From His Tennessee Mansion:::}Things are taking a turn for the worse for Young Buck. TMZ has just brought up a report that the former member of G-Unit, who filed for bankruptcy back in 2010, has been ordered to vacate his 5,000-square-foot home in Tennessee by May 16, and he still owes I.R.S. more than $300k in unpaid taxes.Court documents regarding his eviction showed that the sale of Buck's house, which was bought in 2004, has been signed off by a judge handling his bankruptcy case. It also uncovered that the judge ordered that the proceed from the sale will be used to pay off the 31-year-old rapper's $333,975.69 debt.According to the gossip site, the "Let Me In" rapper was seen carrying boxes and removing all of his belongings from the house earlier this week.While he has yet to comment about his eviction, Buck recently informed his fans that he's going to serve time behind bars. "I got to go to the penitentiary for two months," he said in his v-log. "F**k with me for real, hold me down. And when I get out of the penitentiary, all you rap n****s better get the f**k out the way. I ain't even gonna say no names, but it's a good thing I'm about to go to the penitentiary."Buck, whose real name is David Darnell Brown, became a target in a drive-by shooting back in March. It was reported that the MC, who faced gun charges in 2011, escaped unscathed when nearly a dozen bullets were fired at his SUV when a white Chevrolet Tahoe drove past it at approximately 3:30 A.M. on March 4.

ALICIA KEYS AND STEVIE WONDER COLLABORATION

Alicia Keys and Stevie Wonder Collaborate at 2012 Billboard Music Awards:::}Alicia Keys joined Stevie Wonder on stage near the end of 2012 Billboard Music Awards. She made a duet with the music veteran, who played a piano, in a medley performance of his singles "Higher Ground" and "Overjoyed"."I'm here tonight to say, 'Thank you, Stevie. Thank you for bringing our world so much wonder. Thank you for bringing us so much joy. Thank you for bringing us all so much soul'," she said when introducing Stevie at the beginning of the segment.
She then presented him with Billboard Music Icon Award. When he accepted the award, he requested her to sing "Empire State of Mind" and she did it to a loud applause. "I wanted to say to all of you - Alicia, all who are watching - my fans, family, friends and loved ones, musician friends, every single person," he said in his speech."This really belongs to you and most of all, it belongs to almighty god because all of it is possible for me because my prayers came true. So I must also say to all of you, we are in a place in life where we have to commit ourselves to one thing, and that is to love. 
I truly believe that love always will rule over hate, and peace over war."I do believe that, and I feel that we are approximately 7 billion people in the world, and I'd like for all of us today - including you - to commit yourself today to using your heart and putting your best love forward. Not only that, committing yourself, coming together to change the world by being as one. 
Please!"2012 Billboard Music Awards was kicked off with a live performance by LMFAO and was hosted by Ty Burrell and Julie Bowen. The full winner list was led by Adele with a total of 12 gongs. Other special honorees were Katy Perry (Spotlight Award), Taylor Swift (Woman of the Year), and Whitney Houston (Millennium Award).

May 17, 2012

WASHIRIKI WA BIG BROTHER AFRIKA WALEJEA


 Meneja Uhusiano wa Kampuni ya Multichoice Tanzania, Barbara Kambogi (kushoto) akiongea mchana huu kwenye ukumbi wa mikutano wa hoteli ya Southen Sun,Jijini Dar es Salaam wakati wa mkutano wa Washiriki wa Big Brother Afrika (Julio na Hilda walio katikati) na Waandishi wa Habari. Kulia ni Meneja Masoko wa Kampuni ya Multichoice Tanzania,Furaha Samalu.
 Washiriki wa Big Brother Afrika 2012, Julio na Hilda.
 Aliyekuwa Mshiriki wa Big Brother Stargame 2012, Julio Batalia akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) mchana huu kuhusu ushiriki wake katika jumba lile la Big Brother.
 Aliyekuwa Mshiriki wa Big Brother Stargame 2012, Hilda Reiffenstein akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) mchana huu kuhusu ushiriki wake katika jumba lile la Big Brother.
 Aliyekuwa Mshiriki wa Big Brother Stargame 2012, Hilda Reiffenstein akijibu maswali ya waandishi wa habari.
 Mkutano na waandishi wa habari ukiendelea.
 Aliyekuwa Mshiriki wa Big Brother Stargame 2012, Julio Batalia akijibu maswali huku pembeni yake yupo  Meneja Uhusiano wa Kampuni ya Multichoice Tanzania,Barbara Kambogi. 
 Aliyekuwa Mshiriki wa Big Brother Stargame 2012, Hilda Reiffenstein akiendelea kujibu maswali huku pembeni yake ni Meneja Masoko wa Kampuni ya Multichoice Tanzania,Furaha Samalu.
Mmiliki wa Kajunason Blogspot Bw. Cathbert Kajuna akiongea na aliyekuwa Mshiriki wa Big Brother Stargame 2012, Hilda Reiffenstein.

BOB MARLEY DAY 2012 -JUMAMOSI HII NDANI YA VIWANJA VYA POSTA DAR



 Mkurugenzi wa Caribbean Beat Entertainment Benji Cosmo (katikati) akiongea na waandishi wa habari juu ya tamasha la kumuenzi hayati Bob Marley linalotarajiwa kufanyika jumamosi ya wiki hii katika Viwanja Posta jijini Dar es Salaam. Kutoka kulia ni Ras Magere ambaye ni kiongozi wa 'The Warrios Band', Ras Inno anayewakilisha 'The Inocent People Band',  Jhikoman pamoja na Jonson.
Ras Inno ambaye ni kiongozi wa 'The Inocent People Band' akiwahakikishia waandishi wa habari kushiriki katika tamasha hilo.
Ras Six almaarufu kama Six Dozen wa 'Tunaweza Band' akiwakilisha band.
Kikosi cha 'The Warrios Band' kutoka Arusha wakitoa burudani mbele ya waandishi wa habari.

LULU AKWAA GONJWA BAYA MAHABUSU _SEGEREA



Mgonjwa mwenye UTI akitibiwa.

Elizabeth Michael ‘Lulu’.
Na Shakoor Jongo
MASKINI Kalulu Kadogo! Habari mbaya zilizotua kwenye dawati la Amani wiki hii zinaeleza kuwa staa wa filamu za Kibongo, Elizabeth Michael ‘Lulu’ amekwaa gonjwa baya akiwa mahabusu katika Gereza la Segerea jijini Dar es Salaam.
Akizungumza na gazeti hili baada ya kunaswa kwenye duka linalouza madawa ya binadamu maeneo ya Kinondoni, rafiki wa karibu wa Lulu alidai kuwa alikuwa akinunua dawa za kumpelekea Lulu gerezani kwa kuwa amepatwa na ugonjwa unaomshambulia sehemu nyeti wa
Urinary Tract Infections (U.T.I).
“Namchukulia Lizzy (Lulu) dawa, amepata U.T.I, si unajua mazingira ya usafi kwenye vyoo vya gerezani?
“Ni rahisi sana mtu kupata au kuambukizwa U.T.I kwa sababu ya mazingira ya vyoo vya public (vinavyotumiwa na watu wengi),” alisema rafiki huyo ambaye huwa hakauki gerezani hapo.
Hata hivyo, baada ya kupeleka dawa, Amani lilimpigia simu rafiki huyo ili kujua hali ya Lulu ambapo alidai kuwa anaendelea vizuri huku hofu kubwa ikiwa kwenye ujauzito wake kuhofiwa kuchoropoka.
Lulu yupo nyuma ya nondo za mahabusu ya Segerea kwa msala wa kifo cha Steven Charles Kanumba ‘The Great’ akitarajiwa kufikishwa mahakamani kwa mara nyingine Mei 21, mwaka huu.

    
 source:Gazeti la Uwazi

50 CENTS AZIDIWA GHAFLA


Msanii 50 CENTS ameanua kuweka wazi juu ya afya yake, ambapo kupitia mtandao wa twitter  amepost picha baadhi zikimuonesha yupo hospitali akiuguliwa na ugonjwa ambao akuuweka wazi:
      BAADHI YA PICHA NA TWEETE ZA 50 CENTS
The G-Unit general tweeted pictures of himself in a hospital bed surrounded by stuffed animals, stating that “I’m in the hospital but my gangsta grillz LOST TAPE is done so it will be out on time.”
He also explained that “I don’t want to go into surgery” and wrote, “Do not do a @djdrama gangsta grillz this is all I get. Ain’t this a b*tch. I give 15 tracks you give me this.”
50 Cent is currently prepping the release of his The Lost Tape mixtape, due May 22nd.
I'm in the hospital but my gangsta grillz LOST TAPE is done so it will be out on time. http://t.co/tnz1D4fs
May 16 via UberSocial for BlackBerry Favorite Retweet Reply

I don't want to go into surgery. @FloydMayweather call my phone why your phone off http://t.co/XoW0mbQq
May 16 via UberSocial for BlackBerry Favorite Retweet Reply

Do not do a @djdrama gangsta grillz this is all I get. Ain't this a b*tch. I give 15 tracks you give me this. http://t.co/uPHjaWvP
May 16 via UberSocial for BlackBerry Favorite Retweet Reply
fif1
fif2
fif3

USHOGA AMERIKA:PILIPILI USIYOILA YAKUWASHIA NINI?



Kwa Mukhtasari:
Yaliyokubalika juzi, yalikanwa jana, yaliyokanwa jana, yanakubalika leo. Rais Obama alipokubali ndoa za watu wa jinsia moja alifahamu kwamba jamii ya Amerika ina raia wa kila nui. Tunaomkashifu Obama ni wale tunaoomboleza zaidi kuliko waaliofiwa na tunaowashwa na pilipili iliyo shambani mwa jirani.
WATANZANIAna Waafrika wengi walionyesha kero na butwaa kufuatia tangazo kwamba Rais wa Marekani Barack Obama ameonyesha nia kuunga mkono haki za raia wa Amerika walio na mahusiano ya jinsia moja. Bila shaka mtazamo huo umekita mizizi kwenye imani kwamba uhusiano wa jinsia moja ni mwiko katika muktadha wa mila ya Kiafrika na ni dhambi katika mabano ya dini kuu ulimwenguni.
Makundi kadhaa  yalichukua jukwaa kukashifu hatua ya Rais Obama kana kwamba hatua ya Obama ni ukoma na ingewaangamiza kwa maradhi yasiyo na tiba. Isitoshe, ikumbukwe Rais Obama ni kiongozi wa Amerika na sioTanzania
 
Katika kukabili mabadiliko katika jamii haiwezekani kutumia itikadi na vifaa vilivyopitwa na wakati kupambana na changamoto za sasa. Ndivyo ilivyo tunapokumbana na suala kama ushoga lililo na utata kwenye nyoyo za watu wengi.
Iwapo msimamo wako unachochewa na dini, ni vema kutambua kwamba utakatifu wa tabia na mienendo sio jambo linaloweza kuendeshwa na sheria za umma hasa katika jamii ya imani zinazotofautiana. 
Yaliyokubalika juzi, yalikanwa jana, yaliyokanwa jana, yanakubalika leo. Mawimbi ya jamii hupanda na kushuka na ni sharti wanadamu wawe na wepesi wa kuyakubali angaa jamii iepuke kukuru kakara za migongano. Kuna mataifa yanayoendeleza hukumu ya kifo kwa kukatwa shingo, mengine yana hukumu hiyo hiyo kwa kuchanjwa sindano iliyo na sumu ilhali mengine kwa kitanzi shingoni.
Hukumu ya kifo
Kuna mataifa mengine yameonelea kuwa hukumu ya kifo kwa mbinu yoyote ile haileti haki kwa mhathiriwa; yaani kwa mwizi kuuawa, aliyeibiwa hanufaiki na chochote. Badaye, labda adhabu ya kufaa ingekuwa kumnyima tu uhuru katika jamii, kifungo cha maisha.
Suala la mapenzi ya jinsia moja ni mojawapo ya mambo ambayo hatuwezi kuwa na misimamamo inayokubalika kote na kwa wote. Hasa mjadawal mkuu ni ule wa swaji, Je, ni ushoga ni tabia ambayo mhusika ameichagua, kwa raha zake?  Au Je, ushoga ni suala la kimaumbile na mhusika amelipokea na kwalo hana uwezo kulibadili?
Uwezekano kwamba hali hii ni hali ya kimaumbile haupendezi wapinzani wengi wa haki za mashoga. Kwa sababu ya imani na tamaduni, mawazo ya wengi hayana fursa kutazama suala la ushoga katika mabano ya ‘ni kawaida’
Wengi wa wanaolaani mapenzi ya jinsia moja wanafanya hivyo kwa sababu finyu, sababu zilio ovu kimsingi. Wanateremea na kuona raha kwamba kuna watu wengi huko nje walio kwenye ‘dhambi’ mbaya kuliko zile zao. Kwa kutazama wengine kwa jicho la kuwakashifu, wengi wa watu wa aina hii wanajivunia kwamba hali zao ni kheri.
 Wanaopenda kukashifu tofauti watatafuta kila chembe cha tofauti kuzitumia kuendesha ubaguzi wao. Na hata kama tungechukua mkondo kwamba mashoga ni watu wasiotamanika katika jamii, ni lipi la kutenda kwa watu tusiokubali tabia zao, ilhali tabia zao hazituumizi kwa kwa lolote?
Hawawezi kujieleza
Tusichoweza kukataa ni kwamba kuna idadi kubwa ya raia hawa miongoni mwetu. Hata hivyo katika mataifa ya Afrika, ukosefu wa kuwakubali umewasukuma gizani hawawezi kujieleza au kujitambua; na kwa sababu wamezama na kufyata ndimi, Afrika inajinadi kwa dai ‘uhusiano kati ya watu wa jinsia moja si jambo la kiafrika’.
Hilo si kweli, uhusiano kati ya watu wa jinsia moja umekuwepo kwa karne kadha barani Afrika. Mahusiano hayo hata hivyo  hayakuwa mno ya kingono.
Tukikubali kwamba tunao kipengee hiki cha jamii, swali la pili ni lipi kuwatendea. Ustaarabu sio kuangamiza wale tusiopenda tabia zao, ustaarabu ni kuheshimu tofauti kati yetu, kuwaachia anga yao huku nasi tukipaa kwenye anga yetu. Katika kufahamu hilo jamii itaishi kwa uanana kwani haki itakuwa imetendwa.
Obama anafahamu kwamba jamii ya Amerika ina raia wa kila nui. Tunaomkashifu Obama ni wale tunaoomboleza zaidi kuliko waaliofiwa na tunaowashwa na pilipili iliyo shambani mwa jirani.

ASAMOAH GYAN NA DEDE AYEW WAMEACHA KWENYE KIKOSI CHA GHANA

Mshambulizi matata Asamoah Gyan hayuko kwenye kikosi cha timu ya taifa ya Ghana kilichotajwa na Kocha Kwesi Appia.
Asamoah Gyana na Dede Ayew wote nje

Gyan ameachwa nje hata baada ya shinikizo kwamba ajumuishwe kwenye kikosi cha Ghana.
Wengine waliotemwa ni mwamba wa Chelsea Michael Essien na Andre 'Dede' Ayew ambaye ana jeraha.
John Paintsil na aliyekuwa nahodha wa Ghana John Mensah nao pia hawamo.
katiuka kikosi chake kipya kocha Appiah amewajumuisha wachezaji sita wapya wengi wakiwa wanachezea soka la kulipwa ulaya. hata hivyo amejumuisha wachezaji tisa toka ligi ya nyumbani.
Asamoah Gyan aliamua kujiondoa toka timu ya taifa baada ya kushambuliwa na mashabiki baada ya uchezaji wake duni katika michuano ya kombe la bara afrika la hivi majuzi.
ilikuwa inatarajiwa kwamba angelirejea katika timu kabla ya mwezi ya Juni.
kwa upande wa Ayew , alifanyiwa upasuaji hivi majuzi nae Essien alisema atashughulika zaidi na timu yake ya Chelsea.

Kikosi cha Ghana:

Golkipa: Adam Kwarasey (Stromsgodset, Norway), Robert Dabuo (Wa All Stars), Daniel Adjei (Liberty Professionals), Ernest Sowah (Berekum Chelsea)
Walinzi: Samuel Inkoom (Dnipro, Ukraine), Daniel Opare (Standard Liege, Belgium), Harrison Afful (Esperance, Tunisia), Richard Kissi Boateng (Berekum Cheslea), Masawudu Alhassan (Genoa, Italy), John Boye (Rennes, France), Lee Addy (Dalian Aerbin, China), Daniel Addo (Arsenal Kyiv, Ukraine) Rashid Sumaila (Dwarfs), Jerry Akaminko (Manisaspor, Turkey), Isaac Vorsah (Hoffenheim, Germany)

Viungo: Anthony Annan (Vitesse Arnhem, Netherlands), Derek Boateng (Dnipro, Ukraine), Emmanuel Agyemang Badu (Udinese ,Italy), Rabiu Mohammed (Evian, France) Richard Mpong (Medema) Albert Adomah (Bristol City, England), Christian Atsu (Rio Ave, Portugal), Ishamel Yartey, (Servette, Switzerland), Sulley Muntari (AC Milan, Italy), Kwadwo Asamoah (Udinese, Italy).
Washambulizi: Jordan Ayew (Marseille, France), Dominic Adiyiah (Arsenal Kyiv, Ukraine), Ben Acheampong (Kotoko), Emmanuel Baffour (New Edubiase), Emmanuel Clottey (Berekum Chelsea).
  SO

source:BBC swahili

LADY JAYDEE MSHAHARA WANGU ULIKUWA TZS 80,000

Ukiwa mtembeleaji mzuri wa twitter kuna mengi kuhusu mastaa utakayoyafahamu. Huko ni sehemu ambayo watu maarufu wanajisikia huru zaidi kuongea masuala yanayowahusu.

Wiki hii Lady Jaydee ameweka wazi mshahara wake aliokuwa anapokea katika kazi yake ya kwanza na ya mwisho katika maisha yake kabla ya kujiingiza kwenye muziki na kuwa mjasiriamali.

“Kazi yangu ya kwanza kuajiriwa mshahara ulikuwa TZS 80,000. Ilidumu kwa miezi kadhaa kazi yangu ya mwisho kabla sijaachana na kuajiriwa," aliandika.
 
Kazi yangu ya kwanza kuajiriwa mshahara ulikuwa TZS 80,000/= ilidumu kwa miezi kadhaa kazi yangu ya mwisho B4 Sijaachana na kuajiriwa, KESHO

Hakusema ni kazi gani lakini kwa mujibu wa historia yake ni kuwa aliwahi kuwa mtangazaji wa radio.

Lady Jaydee kama ilivyo kwa wasanii wengine waliokuwa wafanyakazi kama Profesa J, Ray C na wengine, hakuridhika na kipato alichokuwa anapata na hivyo kuamua kufanya muziki ambao leo hii umempa utajiri mkubwa.

Akiwa anamiliki lounge maarufu sana jijini Dar es Salaam ya Nyumbani ameendelea kujiweka vizuri zaidi kifedha ukiachilia mbali fedha anazopata kutokana na muziki.

Kwa wengine mafanikio yake yanawapa wasiwasi ambao kwetu sisi tunaona hauna maana. Katika kutafuta habari zake kwenye mtandao, tumekutana na swali lililokuwa limeulizwa na mtu asiyejulikana katika mtandao wa wiki.answers.com linalouliza “Is Judith wambura member of freemason?

Jibu lililotolewa kwenye mtandao huo ni “Freemasons do not, generally, advertise the fact they are Freemasons. No public statement can be found by Judith Wambura admitting membership. Therefore any statements made as to membership are speculation.”



Si yeye tu anayehisiwa hivyo kwani tayari Diamond na marehemu Stephen Kanumba wamewahi kuhusishwa na habari hiyo.

SOMA TUKIO ZIMA LA KIFO CHA MAFISANGO,PICHA.



 Ramadhabni Wasso akiwa na huzuni.
 Beki wa zamani wa klabu ya Simba, Ramadhani Ramadhani Wasso akiwa akiwa na huzuni baada ya kufika katika 
chumba cha kuhifadhia maiti asubuhi hii.
 Mshambul;iaji wa Simba Haruna Moshi 'Boban' akiingia 
katika chumba cha kuhifadhia maiti asubuhi hii kuangalia 
mwili wa mshambuliaji wa Simba Patrick Mafisango aliyefariki kwa ajali ya gari.
 Bobani akiwa na Said Kokoo
  Ramadhani Wasso akijaribu kuchungulia kupitia mlango kuangalia 
mwili wa Patrick Mafisango kupitia uliokuwa umehifadhiwa katika
 chumba cha maiti asubuhi hii.
  Gari lilosababisha kifo cha Mshambuliaji wa kimataifa wa 
mabigwa wa soka Tanzania na Bara Simba SC,Patrick Mutesa 
Mafisango Leo Alfajiri Picha na Mdau Francis Dande-Muhimbili na 
kwa hisani ya Haki Ngowi Blog