Sep 9, 2016

MSAKO WA WAFANYA BIASHARA WA KUUZA MIILI YAO ''dadapoa' na ''kakapoa''


JESHI la Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam limesema linafanya operesheni ya kuwakamata wamiliki wa nyumba za kulala wageni wanaofanya biashara kinyume cha sheria.

Taarifa iliyotolewa na Kamishna wa Kanda hiyo, Simon Sirro, ilisema wamebaini baadhi ya nyumba za kulala wageni zinatumika kuhifadhi magenge ya majambazi na wahalifu wengine.

Alisema nyumba hizo zimekuwa zikitumiwa na wanawake na wanaume wanaofanya biashara ya kuuza miili yao maarufu ‘dadapoa’ na ‘kakapoa’.

“Ni wajibu wa Polisi kufanya ukaguzi wa mara kwa mara kwenye nyumba za kulala wageni, hoteli, migahawa, vilabu vya vileo, kumbi za starehe zinazokesha na zisizokesha na watakaobainika kuvunja sheria hatua kali za kisheria zitachukuliwa dhidi yao,” alisema.

Katika hatua hiyo, Kamishna Sirro aliwatahadharisha wafanyabiashara wa nyumba hizo kufuata utaratibu wa kupokea wageni kwa kuandika majina yao kwenye vitabu, namba za vitambulisho vyao na sehemu wanapotoka na pale watakapomtilia shaka mteja yeyote watoe taarifa kituo chochote cha polisi.
                   maelezo zaidi pitia udakublog
                    chanzo :www.udakuspecially.com

MSAFARA WA MAKAMU WA RAIS ,MAMA SAMIA SULUHU HASSAN WAPATA AJALI



 Msafara wa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzani, Mama Samia Suluhu Hassan ambao ulikuwa unaelekea Wilayani Tandahimba ukitokea Ikulu ndogo ya Rais ,mkoani Mtwara, umepata ajali na kusababisha majeruhi ambao wamekimbizwa hospitali ya rufaa Ligula.

Ajali imetokea mbele kidogo ya kijiji cha Nanguruwe kilichopo halmashauri ya wilaya ya Mtwara Majeruhi walioumia ni dereva  pamoja na wasaidizi wanne wa Makamu Rais.
Majeruhi wa ajali wakipata msaada wa  huduma ya kwanza mara baada ya gari walilokuwa wanasafiria kuacha njia na kupinduka.

Awali kabla ya gari hilo lililobeba wasaidizi wa Makamu wa Rais kuacha njia na kupinduka, gari liliokuwa limebeba waandishi wa habari wa channel ten, startv na clouds tv liliacha njia na nusura kupinduka.

Barabara ya kutoka Mtwara kuelekea Tandahimba si ya kiwango cha kuridhisha na kuruhusu magari kwenda mwendokasi hali iliyosababisha magari hayo kuacha njia na moja kupinduka kabisa na kusababisha majeruhi

CHANZO CHA HABARI:MICHUZI BLOG