KUONGEA SI KUTENDA ! Wabunge wazalendo wametafakari na kuchukua hatua
dhidi ya wizi na ubadhirifu wa fedha za umma kwa maslahi ya Taifa. Je
mbunge uliyemchagua yuko katika kundi gani?Je ana na njema na Taifa
letu, Anafanya nini panapokuwa na uthibitisho kuwa mabilioni ya fedha
ambayo yangesaidia kuboresha huduma za jamii
yametumika kizembe au yametafunwa na waliopewa dhamana ya uongozi,
Anaungana na wenzake katika kubadilisha hali hiyo au anatanguliza
maslahi yake binafsi kwa sababu hakuna chama chochote ambacho kina sera
ya WIZI NA UBADHIRIFU hiyo ni sera ya VIONGOZI WABINAFSI, NDULI,
DHALIMU, KUPE, MAFISADI, WAOGA NA WANAFKI. Je ulipomchagua ulitegemea
kumpa madaraka na cheo ili akalamike au atumie cheo chake kuboresha
maisha ya watanzania , Unadhani amewajengea heshima wananchi wa jimbo
lenu au amewaletea fedhea. TAFAKARI NA CHUKUA HATUA. MUNGU IBARIKI
TANZANIA , MUNGU IBARIKI AFRIKA
na CG FM RADIO
na CG FM RADIO
No comments:
Post a Comment