KUJITAMBUA NA KUSIHI KAMA ULIVYO
Katika maisha ni vyema sana kujitambua na kuishi kama ulivyo, ni wazi
kabisa binadamu tumeumbwa na tabia tofauti, lakini ukijitambua basi
utajikubali na kujua nini ufanye katika maisha yako na unaweza kuishi
vizuri kuliko kujiingiza katika matatizo ama shida ambazo zinaweza
kukukumba kwasababu ya kutaka kuishi maisha kama ya mtu fulani au mtu
mwingine, wapo watu hawalali wapo radhi kuiba, kufanya ukahaba alimradi
awe na maisha kama ya fulani, kama fulani ana gari au nyumba ya kifahari
isiwe kwako tatizo na kujiona kama maisha haujayapatia maana huwezi
kujua mwenzio amepata kwa njia gani. jitambue na ongeza juhudi katika
kazi yako na utafikia malengo yako ni mbaya sana kulazimisha kufanya
jambo bila juhudi.
Na:Corleone
No comments:
Post a Comment