HISIA ZA UKWELI HUONEKANA KATIKA MAPENZI YA KWELI
Hisia za kweli huonekana katika mapenzi ya kweli
Ni vigumu sana kuishi kwa furaha na mpenzi ambaye moyoni mwako hauna
hisia juu yake. Na hii ni kutokana na kujikuta umependa kwasababu ya
maslahi kwamba unachokitaka ni pesa ama umeamua kuishi naye kutokana na
kumuonea huruma, vilevile kutokana na shinikizo la ndugu nk, ni jambo la
muhimu sana kuzingatia hisia ulizonazo inapendeza na ni furaha kuwa na
mwenza unayempenda kwa kila kitu yaani hisia zako juu yake ni za kweli
na yeye pia awe na hisia za kweli juu yako vinginevyo kama hakuna hisia
za kweli basi migogoro inaweza kujitokeza mara kwa mara na kupelekea
kutokuwa na penzi la kudumu furaha yako italetwa na namna ambavyo
unafuata hisia zako na si kufanya kwa kuiga, tamaa au kujilazimisha
No comments:
Post a Comment