Rais Jacob Zuma na mkewe Bongi Ngema wakikata keki.
...Wakiwa na nyuso za tabasamu.
...Hapa ni wakati wa ndoa ya kimila.
Zuma akiwa amevaa ngozi ya chui na kubeba ngao wakati wa harusi ya kimila.
...Harusi ya kimila ikiendelea.
Picha Zote kwa hisani ya AFP/GETTY IMAGES.
RAIS
wa Afrika Kusini, Jacob Zuma, jana Jumamosi ameoa mke wa sita katika
sherehe ya siku ya pili iliyopambwa kwa shamra za kabila la Wazulu.
Rais huyo mwenye umri wa miaka 70 alimwoa Bongi Ngema siku ya Ijumaa
katika mvumo wa nyimbo za Kizulu akiwa amevaa ngozi ya chui na kubeba
ngao huku akiwa amezungukwa na wanaume waliokuwa wamvalia nguo za
wapiganaji wa kijadi.
Msimamizi
wa ndoa hiyo alikuwa ni mke wa nne wa Zuma aitwaye Nkandla katika
sherehe iliyofanyika KwaZulu-Natal na kufuatiwa na sherehe za kisasa
ambazo zilikuwa ni pamoja na kukata keki.
Zuma
na Ngema wana mtoto wa miaka saba wa kiume. Ndoa hiyo ni ya tatu
katika miaka minne iliyopita naya pili tangu ashike urais wa nchi hiyo
mwaka 2009 akiwa rais mwenye wake wengi.
Kiongozi
huyo ameoa mara sita na ana watoto 21 ambapo mmoja wa wake zake
amekufa na mwingine ambaye ni Waziri wa Mambo ya Ndani, Nkosazana
Dlamini-Zuma – ametalikiana naye. Wanawake hao hufaidika kwa kusafiri na
rais huyo na kufanya kazi za ukatibu mahsusi, pamoja na kufuatana naye
katika ziara za kiserikali.
Pamoja
na kwamba Zuma aligharimia ndoa hiyo yeye mwenyewe, serikali pia
imeongeza bajeti yake maradufu kwa zaidi ya Dola milioni mbili kutokana
na kumwoa mwanamke huyo akiwa mmoja wa familia yake.
Hata
hivyo, ndoa ya wanawake wengi inaonekana kupoteza umaarufu nchini
Afrika Kusini ambapo ustaarabu wa nchi za Magharibi unazidi kuota
mizizi ambapo idadi kubwa ya watu wa nchi hiyo hawakubaliani na
utamaduni huo hivi sasa.
Na 24 SEVEN 365
Na 24 SEVEN 365
No comments:
Post a Comment