Jul 7, 2012

HONGERA HASHEEM THABEET , KWA KUSAINI MKATABA WA MIAKA 2



Hasheem Thabeet, Mtanzania anayecheza mpira wa kikapu Marekani amesaini mkataba wa miaka 2 na timu ya Oklahoma City Thunder..!!!

Watanzania ni wakati sasa wa kujivunia mafanikio ya baadhi ya watanzania wanaofanya vizuri katika viwango vya kidunia, katika historia ya michezo tangu tupate uhuru ni Hasheem Thabeet pekee ndio ameweza kufanikiwa na kucheza ligi ya juu kabisa duniani katika michezo.

Wako watanzania wengi wamefanikiwa katika michezo mbali mbali na kufanikiwa kucheza katika ligi za michezo mbali mbali  na katika nchi mbali mbali ila kila mchezo una ligi zake ambazo ni za kiwango cha juu  juu kabisa ni yeye pekee ndio amweza kufanya hivyo kwa kufanikiwa kucheza mfululizo. Hasheem amecheza timu za Memphis na baadae kucheza Houston Rockets na mwshoni mwa msimu uliopita alicheza Portland Trail Blazers. Katika timu ya Blazers alicheza michezo yote 16 liyokuwa imebaki kabla ya msimu kumalizika.

Hasheem kwa sasa ndio mwafrika mwenye kiwango cha juu kabisa miongoni mwa waafrika wanaocheza kikapu Marekani na ni mchezaji pekee anayecheza huko toka ukanda wa Afrika , Mashariki, Kati na Kusini. Hasheem ni mchezaji wa Afrika ambaye ameingia NBA akiwa na kiwango cha juu kabisa katika historia ya mchezo huo, yaani No. 2 NBA Draft ya 2009.

Kwa Hasheem kuchukuliwa na timu kama Oklahoma City ambao ni mabingwa wa kanda ya magharibi ya NBA na mwaka huu walicheza fainali ya ubingwa wa NBA na kushindwa na Miami Heat, inaonyesha jinsi ambavyo bado mchezaji huyo anathaminiwa na bado uwezo mkubwa wa kuisaidia timu kubwa kama OKC ili iweze kufikia malengo yake.

Hivyo basi kwetu sisi Tanzania tunampongeza na kujivunia mafanikio hayo. Hasheem pia amekuwa ni mchezaji pekee wa kiwango cha juu ambaye amekuwa akirudisha fadhila nyumbani na kila anapopata mapumziko huwa anarudi nyumbani kuja kushirikiana na watanzania wenzake ili kuwainua na kuibua vipaji.

Kwa niaba ya shirikisho la mpira wa kikapu Tanzania, natoa pongezi nyingi kwa Hasheem na tunamtakia kila heri na tumuombee kwa Mungu ili afanikiwe zaidi katika kikapu.

Mungu Mbariki Hasheem, Mungu ibariki Tanzania, Mungu Ibariki Afrika.

Phares Magesa
Makamu wa Rais
Shirikisho la Mpira wa Kikapu Tanzania (TBF)

No comments:

Post a Comment