Dec 29, 2011

waganga na wauguz wahukumiwa kwenda jela bahrain

 waganga na wauguz ambao inasemekana walishiliki katika kutibu wanaharakati walioumia wakati wa maandamano ya kupinga erikal wamehukumiwa vifungo vya miaka tofauti  kati ya miaka 5 mpaka 15 jela.

waganga hao walikuwa wkatika hospitali ya sulmania ,wanashutumiwa kwa kuwatishia walinzi wa usalama kwa kutumia siraha ,visu n a vifaa vungne vya kufanyia upasuaji.msemaji wa wizara ya habari bahrain sheikh mubarak bdukaziz khalifan alisema "waganga hao na wauguz walifanya kitendo cha kigaidi kwa kuwazuia walinzi wa usalama wasifanye kazi zao na kushiriki katika maandamano kinyume nasheria"

THIERRY HENRY MKATABA WA MIEZI MIWILI NA ARSENAL

Mchezaji wa sasa wa club ya  NEW YORK BULLS  strike THIERRY HENRY mwenye umri wa miaka 34 yupo kwenye mkubaliano(majadiliano) ya kuichezea ARSENAL kwa miezi miwili kwa mkopo hapo january.
THIERRY HENRY amekuwa akifanya mazoezi na wachezaj wa club ya arsenal siku za hiv karibuni ,na kupelekea kuonyesha kiwango kizur ambacho kinawashawishi management ya club ya arsenal kumrudisha kambini hiyo january.

WENGER atakuwa anakubwa na tatizo la uhaba wa washambuliaji kuanzia mwaka ujao yaan 2012 ambapo washambuliaj baadhi kama MAROUANE CHAMAKH na GERVINHO watakuwa katika nchizao wakishiriki AFRICAN CUP OF NATIONS mwezi ujao,hvyo watamwach ROBIN VAN PERSIE na mshambuliaj asiyetumainiwa sana na mashabiki wa Arsenal PARK CHU-YOUNG.
  Chu-young amejiunga na Arsenal mwezi August lakini bado hajaonesha cheche zake katika premier league hadi sasa.
      HENRY ambaye aliiacha club y arsenal na kwenda kucheza mpira hispania katika club ya barcelona mnamo mwaka wa 2007,anaweza kuisaidia club ya arsenal katika michezo saba inakuja ikiwa makubaliano pande hzo mbili yataenda sawa kama yalivyopangwa,bila kusahau FA na champion league ,
ARSENAL wataitajka kumlipa HENRY kiasi cha dola 70,000 kwa week.


Cpwaa - Hhmm (Official Video HQ)

h
mzigo mpya wa C PWAA

Lameck Ditto - Tushukuru Kwa Yote (Official Video)


Hapa DITTO amefunika ile mbayaaa!!!!

TID - Hanitaki (Official Video)


VIDEO MPYA NA KALI YA TID hebu isikilize ni bonge ya ngoma

Dec 28, 2011

HALIMA MCHUKA AFARIKI

MWANAMKE mtangazaji wa kituo cha habari cha TBC ,HALIMA MCHUKA amefariki dunia leo alfajiri ,inasemekana HALIMA alikuwa akisumbuliwa na tatizo la ugonjwa wa kiharusi ambalo limejirudia hiyo jana akiwa kazini.
Tatizo ls ugonjwa huu lilishawahi kumpata mnamo mwaka 2007 januari na kupelekea kulazwa hospitalini ambapo wakati akiendelea kupata matibabu katika mwaka 2007 aliweza kutembelewa na mheshima rais Dk Jakaya kikwete na mkeo, kama picha inavyoonesha hapo chini.

kwa taarifa niliyoisikia TBC inasema kuwa "ALIKUWA NA TATIZO HILO JANA MCHANA MARA BAADA YA KUTANGANZA KIPINDI CHA SALAAMU CHA TBC_TAIFA na akazidiwa ndipo alipopelekwa hospitalini kwa matibabu zaidi.
                                          kwenye picha ni aliyesimama katikati
HALIMA MCHUKA alijiunga na RADIO TANZANIA DAR ES SALAAM  mnamo miaka ya 1990 ambapo alikuwa ni mtangazaji mzuri wa mchezo wa soka(mpira) uwanjani.
Mungu alitoa na mungu ametwaa, mungu ailaze roho ya marehemu mahali pema peponi AMINA.
                                           marehemu HALIMA MCHUKA

Dec 19, 2011

UGONJWA WA FACEBOOK

Watumiaji wa mtandao wa jamii wa Facebook wameonywa juu ya kuibuka kwa ugonjwa mpya wa ulevi wa mtandao huo.  Ugonjwa huo mpya unajulikana kitaalamu kama Facebook Addiction Disorder (FAD).
Mtaalamu wa saikolojia  Dr. Michael Fenichel, ambaye ametoa machapisho kadhaa kuhusu FAD mtandaoni, ameelezea dalili za ugonjwa huo ni pale mtumiaji anapoipa kipaumbele Facebook kuliko shughuli zingine za kila siku kama kuamka, kula, kutumia simu kwa matumizi mengine ama kusoma barua pepe zingine.
"Jambo la kustaabisha ni kuwa, kama ilivyo kwa simu za mikononi, hakuna mtu anayegundua juu ya muda na nguvu inayopotea kazini na majumbani.  Sasa hata watu watembeapo, wamejitolea muda wao kwa ajili ya Facebook.”   Dr.  Fenichel aliyazungumza hayo katika chapisho la mtandaoni juu ya changamoto mpya kutokana na FAD.
FAD inaweza pia kuelezwa kama ulevi kupindukia wa tarakilishi.

Jitambue kuwa na ugonjwa huo endapo...
Kwa mujibu wa  Joanna Lipari,  mtaalamu wa saikolojia ya tiba kutoka Chuo Kikuu cha California, Los Angeles alipohojiwa na CNN report, hizi ni dalili kama unaugua ugonjwa wa FAD
1. Unapoteza usingizi kwa ajili ya Facebook. Matumizi ya Facebook yanapokuwa ya lazima kwako kiasi cha kuwa logged in usiku kucha, matokeo yake ni kushinda mchovu siku nzima ifuatayo.
2. Unatumia zaidi ya saa moja ukiwa  Facebook. Lipari alisema ni vigumu kusema ni kiasi gani kiasi kikubwa cha matumizi ya Facebook, lakini kwa wastani mtu anapaswa kutumia chini ya nusu saa kwa siku akiwa Facebook.
3. Unaanza kuzoweana na kuwa karibu na wapenzi wako wa zamani uliokutana nao Facebook.
4. Unadharau kazi kwa ajili ya Facebook. Hii inamaanisha unautumia muda mwingi Facebook kuliko kutimiza majukumu yako ya kazi..
5. Mawazo juu ya Facebook yanakuacha katika wahka. Ikitokea ukaikosa Facebook unapatwa na mfadhaiko, wasiwasi ama dukuduku.  Hii inaashiria unahitaji msaada wa haraka sana.
Wataalamu wa tiba huko Marekani wamekutana na ongezeko la wagonjwa wanaokabiliwa na athari za mitandao ya jamii, ikiwa ni pamoja na kutofanya kazi ama kukosa hamu ya mapenzi.
Facebook
Facebook, iliyoanzishwa na bilionea mdogo zaidi ulimwenguni Mark Zuckerberg, ina watumiaji zaidi ya milioni 500 kote ulimwenguni, nusu yao huingia Facebook kila siku. Idadi ambayo kama ingekuwa ni nchi, basi ingekuwa ya tatu duniani kwa idadi ya watu baada ya China na India.
Kuna picha zaidi ya bilioni 2, huku video zikiwa zaidi ya milioni 14 katika kurasa mbalimbali za Facebook.  Takribani sekunde zipatazo bilioni 6 hutumiwa ndani ya Facebook kila siku, kote ulimwenguni.
Kwa mujibu wa Willis Wee, mwanzilishi wa blog ya habari za jamii na masoko ya Penn-Olson.com, idadi hii ni zaidi ya mara mbili ya idadi ya watumiaji wa mtandao maarufu wa utafutaji wa Google.

UGONJWA WA FACEBOOK


UKWELI KUHUSU YALIYOTOKEA UDSM WANAFUNZI 43 KUFUKUZWA

Mwishoni mwa mwezi wa nane ,bodi ya mikopo ilitoa horodha ya majina ya wanafunzi waliofanikiwa kupata mikopo,ambapo walikuwa takribani wanafunzi elfu ishirini na nne(24000).wanafunzi takribani elfu kumi na tatu (13000)walikosa  mikopo nchi nzima ilihali wengi wao walipata udahili kwenye vyuo na pia  walikuwa na sifa zote za kupata mkopo. Umoja  wa vyuo vikuu nchini (TAHLISO) ulitoa tamko kuwa wanafunzi wote waliokosa mikopo waripoti vyuoni na matatizo yao yangeshungulikiwa wakiwa vyuoni. wakiwa vyuoni wanafunzi hao ambao wengi ni kutoka familia duni, walikuwa wakikabiliwa na maisha magumu yaliyotokana na  ukosefu wa mikopo maarufu kama "NO LOAN".
  Kwa upande wa  chuo kikuu cha Dar es salaam ,takribani wanafunzi 1673 walikosa mikopo.Tulipofungua  chuo mnamo tarehe 10/10/2011 tulikuwa wanafunzi wa mwaka wa kwanza waliokosa  mikopo wakiishi maisha ya kusikitisha chuoin.Baadhi  yao walkuwa wakishinda kwa kula mlo mmoja ambao ni mkate mkavu na maji asubuhi, wengine  walikuwa wakishinda njaa  mpaka siku mbili  hali iliyopelekea kuzimia  ovyo mabwenini.Sisi tuliokuwa na mikopo tulilazimika kukatiana chapati moja wakati waasubuhi na kushirikiana chai kikombe kimoja na d=baadhi ya wanafunzi hao ili siku ziende.Baadhi ya wanafunzi waliokosa  mikopo walikuwa wamekwisha kufungasha vitu vyao na kurudi makwao baada ya kushindwa kulipa  ada na gharama nyingine za maisha chuoni.Hivyo basi tuliyokuwa tunayaona UDSM  yalitoa taswira ya  hali ya mambo ilivyo katika vyuo vingine nchini.
 






DAWA YA MAPENZI

PAMOJA na kwamba wapo watu wengi waliofanikiwa katika suala zima la mapenzi, bado wapo vijana wa kiume ambao wamekuwa wakishindwa kuzikonga nyoyo za akina dada kutokana na kukosa maswali na majibu muafaka wanapokuwa wamewekwa kitimoto na watu hao wa jinsia tofauti, kwa nia njema ya kuweza kufahamiana na kujenga mahusiano.

Mara nyingi mazungumzo ya awali baina ya mwanamke na mwanaume huwa sawa na usaili wa kazi, huku mwanamke akiwa na maswali mengi zaidi kwa mwanaume, akijaribu kuepuka kuingia mkenge, hasa kama alipata kuumizwa au kuachwa kwenye mataa kwenye uhusiano wa kimapenzi siku za nyuma.

Baadhi ya vijana wa kiume, hususan wale waliolelewa katika maadili mema au utisho wa kidini, hutishwa na maswali ya akina dada na kujikuta wakishindwa kutoa majibu muafaka, hivyo kuwakosa akina dada hao. Unapomkosa msichana kwa sababu yoyote ile, ni wazi kuwa utaanza kujenga hofu unapokwenda kukutana na msichana siku nyingine. Ndiyo maana sasa unapaswa kufahamu maswali muafaka ya kuuliza na majibu muafaka kwa maswali ya mwanamke.

Wapo vijana ambao wangependa kufahamu kama kijana wa kiume naye anayo nafasi ya kumweka kitimoto msichana, hasa katika zama hizi za usawa wa jinsia ambapo wasichana wengi wamekuwa na hulka ya kujiamini na kujisimamia, ikilinganishwa na miaka ya nyuma kidogo. Pengine dukuduku haliishii hapo, kwani wapo wale watakaotaka kufahamu ni mambo gani muhimu ambayo kijana wa kiume anapaswa kumuuliza kijana wa kike, katika mkutano wao wa kwanza, au katika siku za mwanzo za mazungumzo yao.

Pia tunaweza kujiuliza, je, yapo maswali mafupi na marahisi ambayo mvulana anaweza kumuuliza msichana na kubaini kama ni msichana anayefaa kuwa mpenzi au mchumba, au ni changudoa? Kwa vyovyote vile, ni dhahiri kuwa ipo haja kwa vijana wa kiume ambao ndio wazungumzaji wakubwa katika uwanja wa mapenzi, kufahamu maswali muafaka wanayopaswa kuwauliza wale waliozigusa nyoyo zao na kuisisimua miili yao kiasi cha kuwafuatilia.

Kama ilivyoelezwa hapo juu, mara nyingi wanaume hujikuta wakitishwa na wanawake, kutokana na maswali yao magumu ambayo huwakatisha tamaa. Hii ni kwa sababu wanaume ndio hasa hujionesha kuwa wanataka kilicho uvunguni. Wanapobanwa kwa maswali na kukosa majibu muafaka, wanaume hawa hunyongea na kujikuta wakiziba midomo yao mapema kabla hata hawajafahamu mwanamke alimaanisha nini.

Lakini badala ya kukata tamaa mapema na kujikosesha mwanamke ambaye mwili wako husisimka na roho yako kupasuka mnapoonana, mwanaume anawajibika kujisimamia na kuchukua hatua, bila kujali kuwa mwishoni mambo yanaweza yasiwe mazuri.

Mwanamke anaweza kujiamini na kusimama kidete mithili ya mwanasheria wa Serikali aliyedhamiria kutetea ukweli, lakini hiyo haimaanishi kuwa mwanaume anapaswa kutetemeka na kunywea kama afanyavyo mtoto mdogo aliyepatikana na hatia ya udokozi.

Kuna njia mbalimbali ambazo mwanaume anaweza kuzitumia kukabiliana na hali hiyo ya kutisha na kukatisha tamaa. Njia mojawapo ni kuhakikisha kuwa unakuwa huru na kujiamini, huku ukiruhusu nguvu ya tabasamu na kicheko kutawala katika mazungumzo husika. Hakikisha kuwa tabasamu na kicheko chako haviwi vya bandia.

Lakini pia ni muhimu, kama ilivyosisitizwa, kuwa na majibu muafaka kwa maswali ya mwanamke. Mathalani, kama mwanamke atakuuliza, "Umewahi kuishi na mwanamke?" mweleze ukweli kuhusiana na maisha yako, ukisema, mathalani, "Ndiyo, nimepata kuishi na mke na nina mtoto mmoja." Baada ya hapo, yamkini utalazimika kueleza sasa unataka nini kwake ambapo pengine itabidi umhakikishie kuwa pamoja na historia yako hiyo, leo hii unampenda yeye.

Njia nyingine ya kukabiliana na shinikizo la mwanamke ni kukabiliana naye moja kwa moja na kujibu kila swali lake kwa jibu makini. Mathalani akikuuliza, "Ni kipindi gani kirefu zaidi ulichopata kuishi na mwanamke au kuwa na girlfriend?" mwambie ukweli papo hapo, mathalani kwa kusema, "Miaka mitatu. Vipi kuhusu wewe? Uliwahi kuwa na uhusiano wa kimapenzi na mwanaume kwa kipindi gani?"

Pamoja na njia hizi, pia kuna maswali muafaka unayopaswa kuuliza na kuhakikisha kuwa unamshinda
mwanamke wako na kuiteka roho yake. Pamoja na kusaidia kumteka mwanamke, maswali hayo yatakusaidia pia kupata taarifa muhimu kuhusiana naye.

Unalopaswa kuzingatia zaidi ni kutokubaliana na kila jibu la kwanza unalopata kwa mwanamke kwa kila swali. Mara nyingi ukweli wa mwanamke hudhihirika unapomuuliza maswali kadhaa ya nyongeza kwa kila swali moja la msingi. Hapa lazima ujue kutumia maarifa ya bungeni katika kuuliza maswali ya nyongeza - mara nyingi hata bungeni maswali ya nyongeza ndiyo huwa na manufaa zaidi kuliko yale ya msingi.

Kwa hiyo, usiwe na papara ya kuuliza swali linalofuata, kabla hujapata majibu ya kuridhisha kwa
swali lililoulizwa. Pia zingatia kuwa wanawake wote ni wadadisi na watundu kwa asili. Mwanamke aliyeona thamani katika jinsia yake huuliza maswali magumu na ya kiudadisi kwa mwanamume anayemjia kwa ajili ya kumtaka kimapenzi.

Ni jambo zuri kwa mwanamke kuwa mdadisi kuhusiana na mwanaume anayemnyemelea, lakini ni dhahiri kuwa hakuna mwanaume anayependa kuona mwanamke akimpa shinikizo la damu kutokana na maswali yake. Ili kufanikiwa katika jambo hili, mwanaume anapaswa kutofautisha mwanamke mdadisi na mwanamke anayetaka mashindano. Mara nyingi hata kiimbo katika sauti ya mwanamke hubainisha msimamo wake, kama ni mdadisi au mtu wa shari anayetaka kukusasambua na kisha kukuachia maumivu na kuondoka zake.

Pia kuna jambo lingine muhimu kuhusiana na mawasiliano baina ya watu wa jinsia tofauti waliodhamiria
kupendana. Wanawake ni wasikilizaji wazuri zaidi kuliko wanaume na kwa hiyo vijana wengi wa kiume
hupaswa kujifunza sanaa ya kusikiliza, ili kujihakikishia kuwateka wanawake.

Kwa ujumla, mwanaume hupaswa kumuuliza mwanamke maswali ya kusisimua na yenye maana kuhusiana na yeye mwenyewe - maswali ambayo kuna kila dalili kuwa unataka kufahamu majibu yake na si kuuliza ilimradi tu.

Mojawapo ya malalamiko ambayo wanawake hutoa kuhusiana na wanaume ni kwamba wanaume huzungumza masuala yanayohusiana na nafsi zao tu na kushindwa kumuuliza mwanamke japo swali moja tu kuhusiana na nafsi yake. Jambo lingine la maana kabla ya kuyafahamu maswali muafaka ya kumuuliza mwanamke ni kuhakikisha kuwa huulizi maswali hayo bila kuwa tayari kujibu maswali mengine kama hayo kutoka kwake.

Mifano ya maswali ya kumuuliza mwanamke ambayo na wewe pia unapaswa kuwa na majibu yake ni kama vile, ni kosa gani kubwa ambalo unadhani wanaume hulifanya zaidi katika uhusiano wa kimapenzi? Swali hili ni muhimu kwa sababu litakubainishia ni kitu gani humuudhi zaidi mwanamke uliye naye, ili ukiepuke. Pia jibu lake hukupa taswira ya jumla ya mwanaume katika akili ya mwanamke unayezungumza naye.

Maswali mengine ni kama vile, Je, unawadhania wanaume kuwa waroho wa ngono au wenye kujali maslahi ya wanawake? Je, ni sifa zipi unazozidhania kuwa sifa za uhusiano wa kimapenzi unaopaswa kupigiwa mfano? Je, ulipata kuwa na uhusiano na mwanaume aliyekuwa changamoto kwako? (Mpe nafasi ya kueleza alikuwa changamoto kwa namna gani). Ni kitu gani muhimu zaidi katika mustakabali wa mapenzi?

Maswali mengine ya kumuuliza mwanamke ni kama vile je, uliwahi kuvunjika moyo kwa suala la kimapenzi? (Unapouliza swali hili omba kwamba jibu liwe 'ndiyo', kwani mwanamke aliyepata kuvunjika moyo ana roho ya upole na uvumilivu zaidi). Mengine ni je, ni kitu gani hukushtua unapokuwa unaelekea kufungua moyo wako kwa mwanaume? Je, katika mahusiano yako ya zamani na wanaume wewe ndiwe uliyewatema au wao ndio waliokutema?

Maswali mengine ni je, unadhani uliwahi kuwa na uhusiano wa kimapenzi wenye mafanikio? Je, ni kwa nini uhusiano wako wa mwisho wa kimapenzi na mwanaume ulivunjika?

Unapouliza maswali haya na mengine ya aina hii, kumbuka kuwa mwanamke anaweza kuja juu na kwa hiyo unapaswa kuwa tayari kumjibu. Kumbuka kuwa uhusiano wa kimapenzi ni kitu kinachohitaji kufikiria kwanza kabla ya kuchukua hatua na mara zote ni vema kumkosa mwanamke unapomtongoza kuliko akutose unapokuwa umemzoea.

HUU SI USAILI

Maswali haya ukiyauliza kwa mfuatano fulani utaonekana kama umemweka mwanamke katika usaili. Hali hii haitakupa alama zozote chanya na wala huwezi kujihakikishia kuwa utampata. Hakikisha kuwa maswali haya yanajitokeza kwa asili tu katika mazungumzo yenu.

MAGAZETI YA LEO YAMEANDIKAJE?


MAGAZETI YA LEO YAMEANDIKAJE?


WORLD'S SHORTEST WOMEN

  • Jyoti Amge crowned world shortest woman at just 62cm tall
  • She weighs only 12lbs - just 9lbs more than she did at birth
The 2ft teenager is already a mini celebrity in her hometown of Nagpur, India, but is now set for a huge record when she is officially declared the world's smallest woman.




And despite her miniature stature, 61.95cm-tall Jyoti hopes to celebrate being crowned the world's shortest woman by launching a Bollywood movie career.
She took the Guinness World Record from 2ft 3in American Bridgette Jordan, and celebrated her birthday with a teddy bear which loomed over her tiny 24.4in frame.
She measured 7 centimeters (2.76 inches) shorter than the 22-year-old American Bridgette Jordan, who had held the title since September.

MABALOZI WAPYA WAAPISHA IKULU JIJINI DAR ES SALAAM

Rais wa jamhuri ya muungano DK JAKAYA KIKWETE  ameapisha mabalozi wapya Ikulu jijini Dar es salaam,
hii ni picha inaonesha viongozi wa serikali na mabalozi walioteuliwa.

DK JAKAYA KIKWETE AAPISHA MABALOZI WAPYA

Raisi wa jamhuri ya muungano wa TANZANIA ameteua  mabalozi wapya

KIM JONG IL AFARIKI DUNIA

Televisheni ya serikali ya korea ya kaskazini imetangaza kuwa kiongoz wa nchi hiyo, kim jung Il, amefariki dunia kwenye treni katika ziara ya kikazi ,baada ya kuzidiwa na shinikizo la damu la ghafla.
 China imesema ina majonzi sana kwa kifo cha kim Jon Il na  imeungana na raia wa korea kaskazini kuomboleza kifo cha swahiba wake mkubwa.Rais BARACK OBAMA wa marekani amempigia simu mwenzake wa korea kusini,Lee Myung-Bak, usiku wa manane, kutathimini kifo hcho.usalama na ulinzi umeimarishwa mpakani mwa korea hizo mbili. Na huko japan  masoko ya hisa yameanguka kwa zaidi a asilimia 1.26 kufuatia taarifa za kifo hiki.
jong Il aliingia madarakani mwaka 1994 baada ya kifo cha ghafla cha baba yake Kim Il sung , ambaye alikuwa ameliongoza taifa hilo tangu mwaka 1948.  mafaniko ya kim jong Il yalikuwa ni kuivaa tabia na haiba ya baba yake, na hivyo kujijengea mvuto ambao kabla hakuwa nao.wengi wanasema kuwepo madarakani kwa jong Il madarakani kulikuwa ni sawa na kuwepo kwa Il sung.
   Kielimu, Kim Jong Il alisoma kwanza nchini China kabla ya kujiunga na chuo kikuu cha Kim Il Sung mjini Pyongyang alikosomea siasa na uchumi. Aliingia rasmi kwenye siasa mwaka 1964, kwa kujiunga na chama pekee cha siasa, chama tawala cha Wafanyakazi cha Korea, ambako alipanda vyeo haraka haraka.
Waombolezaji nchini Korea Kaskazini.Waombolezaji nchini Korea Kaskazini.Akiwa na miaka 31 tu hapo mwaka 1973, aliteuliwa kuwa katibu mkuu wa mipango na propaganda, na mwaka mmoja baadaye akatangazwa rasmi kuwa mrithi wa baba yake. Mwaka 1980 aliingia kwenye Kamati ya Ulinzi, ambacho ndicho chombo cha juu kabisa kiutawala. Mwaka 1991 akatangazwa kuwa kamanda mkuu wa majeshi.
Si mengi yanayojulikana na ulimwengu wa nje kuhusu kiongozi huyo. Vyombo vya habari vya Magharibi vinajaribu kumuelezea kama mwanamme anayevaa suti za Mao na miwani meusi, anayependa wanawake, ulevi, vyakula na magari ya kifahari, lakini asiye na ufahamu sana wa mambo ya dunia. Maisha yake binafsi, yakiwemo mahusiano yake na maisha ya watoto wake wanne, yalikuwa ni mwiko kuzungumzwa kwenye vyombo vya habari vya serikali.

TAMKO KWA VYOMBO VYA HABARI KUHUSIANA NA WANAFUNZI WA VYUO VIKUU KUFUKUZWA

UTANGULIZI:

Kwa miaka ya hivi karibuni Vyuo mbalimbali vimekua na tabia ya kuwafukuza ama kuwasimamisha masomo wanafunzi wanaoendelea na masomo kwenye vyuo vikuu mbalimbali hapa nchini mwetu kutokana na mashinikizo mbalimbali kutoka kwa viongozi wa kiserikali kwa kisingizio kuwa wanafunzi hawa wanafanya siasa vyuoni.









Itakumbukuwa kuwa migomo na maandamano ya wanafunzi kwa vyuo vikuu hapa nchini haijaanza pale mfumo wa vyama vingi uliporuhusiwa kuanza mwaka 1992 ,bali migomo na maandamano haya yamekuwepo tangu kuanzishwa kwa vyuo hivyo.



Mathalani, Chuo Kikuu cha Dar es Salaam kimekuwa na historia ya migomo na maandamano ya mara kwa mara tangu kuanzishwa kwake , na hivyo dhana ya kuwa wanafunzi wanagoma kutokana na misukumo ya kisiasa sio sahihi hata kidogo bali ni mbinu ya watawala kujaribu kuficha madhaifu yao .

Wanafunzi hawa wamekuwa wakigoma kutokana na serikali ya CCM kuendesha mambo yake kibabe na kwa dharahu ya hali ya juu ambapo imefanya elimu kuwa Privilage na si haki kwa watanzania.

Kwa mantiki hiyo basi, kutokutendewa haki kwa wanafunzi hawa na serikali yao, kukosekana kwa miundombinu bora ya kusoma na kujifunzia, wanafunzi hawa kunyanyaswa na watawala wa vyuo hivyo, kukosekana kwa mikopo kwa wakati muafaka, serikali kuingilia uendeshaji wa
vyuo ,serikali kuvunja serikali za wanafunzi bila kutoa sababu za kimsingi na sababu nyingine mbalimbali ndio chanzo cha vurugu na migomo vyuoni.

Hivyo basi , kutokana na sababu tajwa hapo juu Baraza la Vijana na CHADEMA (BAVICHA) tunatamka wazi kuwa kitendo cha Vyuo Vikuu vya Dar Es Salaam, Dodoma na Muhimbili kuwafukuza wanafunzi kwa ujumla wake zaidi ya 100 ni kitendo cha uonevu kwa wanafunzi hawa na kamwe hakivumiliki hata kidogo na haswa ikizingatiwa kuwa ni watoto wa watu
masikini na ambao kimsingi wanajilipia ada wenyewe kwani wanakopa na baada ya muda watapaswa kulipa fedha hizo.

Kwa nini tunapinga uamuzi huu wa kuwafukuza wanafunzi vyuoni;
1. Ni kinyume na Tamko la Ulimwengu la mwaka 1990 la uhuru wa
kitaaluma (Academic Freedom) ambalo tulisaini mnamo mwezi April tarehe
29 hapa Dar Es Salaam , linasema wazi kuwa ni lazima Vyuo vijiendeshe
kwa uhuru kamili bila kuingiliwa na serikali .


2. Kufukuzwa kwa wanafunzi hawa ni utekelezaji wa Maazimio ya vikao vya CCM vilivyofanyika na haswa vile vya Halimashauri Kuu ambavyo vimetoa maelekezo mbalimbali kwa Serikali juu ya kuwachukulia hatua wanafunzi wa vyuo vikuu ambao wamekuwa wakiikosoa serikali waziwazi , na hata wahadhiri ambao wamekuwa wakitumia taaluma zao kwa uwazi na kusema juu ya mapungufu ya serikali wachukuliwe hatua ya ama kufukuzwa
kazi na au ajira zao kusitishwa. Hivyo hii ni muendelezo wa utekelezaji wa maamuzi hayo.

3. Kuvunjwa kwa taasisi za wanafunzi na haswa serikali za wanafunzi , hii ni kutokana na tangazo la serikali kuhusiana na kanuni za serikali za wanafunzi lililochapishwa tarehe 12/06/2009 ambalo ni tangazo namba 178 lilivunja rasmi nguvu za serikali za wanafunzi kuanzia na muundo wake, majukumu yake na hata jina la vyeo husika kwa kufuta rasmi cheo cha urais kwenye serikali za wanafunzi. Hii ni kutokana na ukweli kuwa mara baada ya taasisi hizi kuvunjwa wanafunzi wamekosa chombo cha kuwasilisha matatizo yao kwa menejimenti za vyuo husika.

4. Wanafunzi waliofukuzwa vyuoni hawajatendewa haki kwani hawajapata fursa hata ya kusikilizwa na kujitetea mbele ya vyombo husika vya vyuo hivyo, na wakati huo huo walikuwa wanamadai ya kimsingi kabisa .Hivyo hii ni kinyume kabisa haki za kimsingi (Natural Justice).


5. Waziri wa Elimu na mafunzo ya Ufundi, Dr Shukuru Kawambwa amekuwa
na tabia ya kuingilia taasisi za elimu ya juu , kwa mfano mnamo tarehe
22/06/2011 aliandika dokezo sabili kwa Katibu Mkuu wa Wizara hiyo
akitoa maelekezo kwa Bodi ya mikopo kusimamisha mikopo kwa Wanafunzi
kwa ajili ya Mafunzo kwa vitendo hadi hapo uongozi wa UDOM utakapoamua
nani alipwe na nani asilipwe. Pamoja na ukweli kuwa wanafunzi wana
mikataba na bodi ya mikopo bado waziri anaweza kuagiza mikataba hiyo
kuvunjwa na bodi husika. Na hata kitendo cha kuwafukuza wanafunzi hawa
ni muendelezo wa serikali kuingilia vyuo hivi na utendaji wake.

6. BAVICHA , tunapinga na kulaani tamko lililotolewa na Makamu Mkuu wa
Chuo Kikuu cha Dar Es Salaam kuwa vijana hawa wasipate fursa yeyote ya
kudahiliwa na vyuo vingine hapa nchini , hii ni kinyume na Katiba ya
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kuwa kila mtu ana haki ya kujiendeleza
kwa kadiri ya uwezo wake. Hivyo kitendo hiki kamwe hakivumiliki kwa
mtu mmoja kuwa na mamlaka ya kuwanyima wengine fursa ya kupata elimu
kwa sababu ambazo hazielezeki na ni vitisho visivyovumilika hata
kidogo.

Hivyo basi BAVICHA tunaitaka serikali na management zake za vyuo ziache tabia ya kutibu matokeo au matawi ya matatizo vyuoni humo kwa kukimbilia kufukuza wanafunzi bali kutatua kiini cha matatizo.









Pia tunawahimiza vijana wote wanaosoma katika vyuo , Sekondari ,taasisi mbalimbali za kitaaluma, wanaharakati na wadau wa elimu na maendeleo ya kweli hapa nchini kuungana pamoja ili kuupinga utamaduni huu mpya wa kuwanyanyasa wanafunzi wa Vyuo Vikuu.

Jambo hili likiachwa ili liendelee bila kuchukua hatua litaathiri sana taifa kwani watawala wanataka kutengeneza taifa la watu waoga na wasiokuwa na uwezo wa kuhoji masuala mbalimbali.

Sambamba na haya, kuna wanafunzi wengi waliopaswa kuanza mwaka wa kwanza wa masomo mwaka huu lakini wameshindwa kufany hivyo kwa kile kinachoelezwa na bodi ya mikopo kutokua na bajeti ya kuwakopesha. Wanafunzi hawa wamesharudi makwao.

Majibu haya ya bodi ya mikopo kwa wanafunzi hawa ni kielelezo cha serikali ya CCM kutokujali wala kuthamini elimu na kwamba anasa na kutapanya mali za umma ndio kipaumbele chake. Serikali haina fedha za kusomesha wanafunzi lakini ina fedha za kulipa posho kwa viongozi wake wachache. Katika hili, BAVICHA tunaitaka serikali itafakari upya swala la elimu na hata sera ya elimu ya juu hapa nchini

Tamko hili limetolewa na;
…………….
John Heche
Mwenyekiti wa BAVICHA TAIFA.

KAFULILA afukuzwa NCCR-MAGEUZI

Chama cha NCCR-MAGEUZI  kimemfukuza Uanachama mbuge wa kigoma kusini, ndugu DAVID KAFULILA na wajumbe wengine wapatao sita bila kumsahau mgombea urais wa chama hicho  ambaye alishiliki katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2010, bwana HASHIM RUNGWE. Maamuzi haya yalifanyika katika ukubwi wa halamshauri  kuu ya chama hicho ambapo katika mkutano huo kulitawaliwa na vurugu na fujo hali iliyopelekea chombo cha ulinzi na usalama kuingila kati(polisi).





Hata hivyo mara baada ya kutangazwa kwa ndugu kafulila kutolewa katiak chama , alikwenda kupiga magoti mbele ya mwenyekiti wa chama hicho, JAMES MBATIA huku akibubujikwa na machozi ,na kuomba radhi  huku akisema "Naomba  radhi , nmekosa mnisamehe.

KAFULILA afukuzwa NCCR-Mageuzi

ampigia magoti MBATIA kwa machozi, wajumbe AMPIGIA MAGOTI MBATIA KWA MACHOZI, WAJUMBE WAKATAA KUMSAMEHE
Fidelis Butahe

CHAMA cha NCCR-Mageuzi kimemfukuza uanachama Mbunge wa Kigoma Kusini, David kafulia na wajumbe wengine sita akiwamo aliyekuwa mgombea urais wa chama hicho katika Uchaguzi Mkuu wa 2010, Hashim Rungwe.Uamuzi huo ulitolewa kwenye kikao cha dharura cha Halmashauri Kuu (Nec) ya chama hicho kilichofanyika katika Ukumbi wa  Poroin jijini Dar es Salaam jana, ambao ulitawaliwa na vurugu mpaka polisi wakaitwa ili kuongeza ulinzi.
Baada ya uamuzi huo kutolewa Kafulila alikwenda kupiga magoti mbele ya Mwenyekiti wa chama hicho, James Mbatia huku akibubujikwa machozi na kuomba radhi akisema: “Naomba radhi, nimekosa mnisamehe...”


Baada ya hapo Mbatia alisimama na kumwombea msamaha  kwa wajumbe wa kikao hicho, lakini walikataa na kumweleza (Mbatia) kuwa akisamehewa watarudisha kadi zao za uanachama.“Hatutaki, Kafulila hatufai anakiharibu chama na akisamehewa sisi tutarudisha kadi zetu za uanachama ili ubaki naye kwenye chama...,” walisikia wajumbe hao wakisema kwa sauti ya juu.Wanachama wengine waliofukuzwa ni, Ally  omari, Mbwana Hassan, Josam Rugugila, Lucy Kapya, Jamwe Batifa na Hashim Rungwe ambao walikuwa viongozi wa chama hicho.


Dalili za Kafulila kufukuzwa zilijionyesha wazi juzi baada ya wazee wa chama hichi kupitia kwa Katibu wao wa Taifa, Ernest Mwasada kuitaka Nec kumfukuza (Kafulila kwa kuwa ndiye chanzo cha migogoro yote inayoendelea ndani ya chama.


















“Hizi vurugu zinachochewa na Kafulila ambaye ndiyo mfadhili na kiongozi wa waasi wa uchochezi huu. Menejimenti inapaswa kumwangalia sana, huyu ni hatari ndani ya chama hastahili kabisa kukaa na jamii yoyote inayopenda amani,” alisema Mwasada.

Hata hivyo, Kafulila juzi  alikanusha akisema kuwa madai hayo ni ya uongo na kwamba, Katibu wa Taifa wa chama hicho anateuliwa na Katibu Mkuu ambaye amekosana naye.

“Ni hivi, Katibu wa Wazee wa Chama anateuliwa na Katibu Mkuu ambaye hatuelewani na juzi alifanya kikao kilichoeleza mambo mengi mabaya dhidi yangu," alisema Kafulila na kuongeza:

“Huyo Katibu wa Wazee amelishwa maneno  na Ruhuza kwani ndiye mwajiri wake ambaye anafanya kazi maalumu ya kumchafua Kafulila na alifanya hivyo kwenye semina ya wenyeviti na makatibu wa chama 19 iliyomalizika jana (juzi) jijini Dar es Salaam.”
Kafulila alisema kazi ya Ruhuza ni kuwanywesha sumu viongozi wa chama kuwa yeye (Kafulila) ni mkorofi badala ya kuendesha semina kuhusu mambo ya msingi ya kukijenga chama.

Aliongeza kuwa, Katibu Mkuu huyo  amefikia hatua ya kutaka  ionekane kuwa wenyeviti wa chama wa majimbo ya mkoa wa Kigoma wanampinga (Kafulila), lakini kati ya wenyeviti  wanane ameambulia wawili tu ambao ndiyo anawanywesha sumu ya chuki dhidi yake.
Kikao hicho cha dharura cha Nec jana kilianza kwa wajumbe kutupiana lawama na kuzozana kwa kile walichosema, kuwapo mamluki na mipango ya kukandamiza demokrasia.

Hali hiyo iliwafanya wajumbe wenye msimamo mkali wakiongozwa na mkongwe wa chama hicho Hashim Rungwe ambaye alikuwa mgombea urais kupitia chama hicho katika uchaguzi mkuu mwaka jana, kutoka nje ya kikao.

Mmoja wa wajumbe waliokuwa ndani ya ukumbi alitoka nje na kuwaita polisi waliokuwa nje na kuwaeleza kuwa ndani kuna vurugu.
Mgawanyiko wa wazi wa wajumbe ulijikita zaidi kwenye mpasuko unaotokana na tofauti za kimsimamo kati ya Mwenyekiti wa chama hicho (Mbatia), na Mbunge wa Kigoma Kusini, David Kafulila. Inadaiwa kuwa kundi lililotoka nje ni lile linalomuunga mkono Kafulila, baada ya kuona mpango wa kupiga kura za kutokuwa na imani na Mbatia umehujumiwa.Polisi waliingia ndani ya kikao hicho wakiwa na virungu na kuwasihi wajumbe hao kufanya mkutano wao kwa utulivu.

Mbatia ashinda
Taarifa zilieleza kwamba, mvutano mkubwa ulikuwapo ndani ni wa kupinga kura za kutokuwa na imani na Mbatia kufanywa za wazi kwa wajumbe hao kusema 'ndiyo' au 'hapana' badala ya kupigwa kwa siri.

Hata hivyo upande uliokuwa unamuunga mkono Mbatia uliweza kung’ang'ania hadi hoja yao kupita ndipo baadhi ya wajumbe, wakaamua kutoka nje.
Katika kura hizo, inadaiwa Mbatia aliibuka mshindi kwa kura 40 za kuwa na imani naye dhidi ya nane zilizomkataa na mbili kuharibika. Kikao hicho kilikuwa na wajumbe 59, wakiwapo wabunge watatu wa chama hicho.

Kufukuzwa Kafulila
Kuhusu hoja ya kumfukuza uanachama Mbunge wa Kigoma Kusini, David Kafulila, wajumbe walitakiwa kuwa makini ili wasije wakakirejesha chama hicho kwenye vyama visivyo na wabunge.

Kauli hiyo ilisisitizwa na Dk Sengodo Mvungi ambaye alisema NCCR imetoka katika mazingira mabaya kisiasa kwa kutokuwa na mbunge hata mmoja, hivyo chokochoko za kumfukuza Kafulila, zinarudisha nyuma maendeleo ya chama. Naye Kafulila aliwataka wajumbe wawe watulivu na hata kama yupo kwenye mgogoro na Mbatia, wazee wa chama ndiyo wanaoweza kutumia busara kuwasuluhisha.

Vyanzo vyetu kutoka ndani ya mkutano huo vilieleza kuwa mbali na Kafulila, wanachama wengine waliotakiwa kufukuzwa ni Rungwe na makamishna wa chama hicho mikoa ya Tanga na Mwanza.

Hoja ya kundi la Kafulila lililodai kuna mamluki, ilionekana kuwa na nguvu kwa sababu Nec ya chama hicho huwa na wajumbe wasiozidi 40, lakini walishangazwa na kitendo cha wajumbe kufikia karibu 60.

Baadhi ya wajumbe waliibua hoja ya kutaka baadhi ya watu ambao hawafahamiki kutakiwa kujieleza na taratibu zitumike kuwatambua au kutowatambua.

Wakati hoja hiyo ikiwa haijapata ufumbuzi, iliibuka nyingine ya kutaka Rungwe aeleze sababu za kumwandikia barua Msajili wa Vyama vya Siasa nchini kumwarifu kuwa kikao hicho si halali.
Hadi gazeti hili linakwenda mitamboni, kikao hicho kilikuwa kinaendelea, huku vurugu kubwa ikiendelea.
Awali kulikuwa na taarifa kwamba wazee wa chama hicho walijiandaa kumtimua uanachama Kafulila kwa kile kilichoelezwa kuwa ameonyesha utovu wa nidhamu uliovuka mpaka.

Wakati hayo yakiendelea, zilikuwapo taarifa kwamba kundi la wanaomuunga mkono Kafulila, lilikuwa na mkakati wa kumng'oa madarakani Mbatia.
Kwa muda mrefu Mbatia na Kafulila wamekuwa wakitofautiana katika hoja mbalimbali ndani ya chama hicho.
Kutokana na hali hiyo, hivi karibuni, katibu wa chama

Dec 16, 2011

MAMBO YA KUZINGATIA PINDI UMEALIKWA CHAKULA KWA NDUGU, RAFIKI au JAMAA

Kwa maisha ya watu wengi hususani nchi zetu hizi swala la kuharikana katika mambo mbalimbali yawe ya sherehe za kuzaliwa, ndoa , komunyio, kipaimara, maulidi, hitimisho katika misiba ,na mbalimbali. lakini kwa upande wangu leo ningependa japo nizungumzie katika swala la mwaliko wa chakula nyumbani kwa ndugu, rafiki au jamaa, pindi unapopata mwaliko MAMBO YA KUZINGATIA WAKATI MNAENDELEA KUPATA CHAKULA MEZANI NI KAMA YAFUATAVYO;

1.Ni kujaribu kuzuia Usitoe comment mbaya kuhusu chakula unachokula kwani kuna mtu ametumia muda wake kukiandaa na kukipika chakula hicho .
2.punguza na ikibidi acha kuongea/maongezi ukiwa na chakula mdomoni.
3.Onyesha kufurahia chakula

4.Kama unahitaji kitu kama chumvi,bakuli ya mboga au chochote na haufikii omba usogezewe na sikupitisha mikono kwa mwenzako ambae tayari anakula.
5.Usitoe kitu mdomoni ukakiweka juu ya meza,kama ni mfupa toa mdomoni weka pembeni kwenye sahani yako.

6.Usibeue/kutoa gas kwa sauti...
7.Ukialikwa mlo kwa rafiki,ndugu au jamaa baada ya mlo shukuru na ueleze ni namna gani umefurahia chakula ulichokula unaweza ukasifu mboga kwa mfano labda "samaki alikuwa mtamu kapikwaje maana kama sijawahi kula samaki.."

hizo ni baadhi za taratibu na sheria unaweza kuzitumia pindi upatapo mwaliko wa chakula ua kujaribu kuziapply katika maisha yako ya kila siku hili upate kuzizoe na kuzifahamu kwa undani zaid, kama unachakuongezea unaweza uka comment kisha wengne nao wapate ideas juu ya swala hili la mwaliko.

ANTiVIRUS DAWA YA Virus WA Hiphop in TanzaniaKAMA KWELI WE NI MKAZI WA ARUSHA...!JUMA PILI PALE TRIPPLE "A"

Usikose show ya kijanja na ya ukwel kwa wale wakazi wa ARUSHA na vitongoji vyake, ni wale wale wanaharakati wa mziki wa HIP HOP TANZANIA  ambao wanajulikana kama VINEGA
KAMA HUJUI MAANA YA NENO KINEGA....! kinega ni KIVUMISHI AMBACHO KINAMFANANISHA BINADAM NA NDEGE ANAYEITWA KINEGA,,NDEGE HUYU NI NDEGE AMBAYE HANA SIFA YA KUONEKANA OVYO,NA PIA HUWA ANAONEKANA JUU SANATOFAUTI NA NDEGE WA KAWAIDA,,PIA KUWA KINEGA HALI YA KING'ANG'ANIZI KWENYE JAMBO FLANI..!SO UKIMUONA KINEGA UJUE KUNA JAMBO...!    
so we kama ni shabiki  na mpenzi wa mziki hususani wakazi wa jiji la ARUSHA  mnaombwa kufika kwa wingi maeneo ya TRIPPLE ''A''  siku ya JUMAPILI kuanzia time ya saa 8 mpaka saa 6 usiku kwa kiingilio cha shillingi ELFU TANO TU:

Dec 15, 2011

HILI NDO BATA ALILOLIFANYA CHRIS BROWN PANDE ZA DUBAI

Chris Brown and his boo Karrueche had fun soaking up the hot desert sun as they kicked it in Dubai this past weekend. The two were spotted rolling around the desert in a four wheeler as well as spending time on a private yacht.
Earlier in the week, Chris performed in front of thousands at the Dubai Festival City Concert Arena.
“Look at me now…”

MATUKIO UK: WEMA AKILALAMIKA KUHUSU JOKATE KUMCHUKUA DIAMOND

MATUKIO UK: WEMA AKILALAMIKA KUHUSU JOKATE KUMCHUKUA DIAMOND

WAVULANA / WANAUME SIKU HIZI HAWAPENDI MWANAMKE TEGEMEZI

Ni wazi kabisa kwa asilimia kubwa ya wanaume sikuhizi hawataki kutegemewa kwa kila kitu kwani maisha yamekuwa magumu wakati mwingine unakuta hata wao wenyewe wanashindwa kujitosheleza hivyo kuwa na mpenzi tegemezi wanaona ni hasara kubwa na kutokana na hilo mwanamume akiona mwanamke pale mwanzo tu baada ya kumtokea mara anaomba vocha, msaada wa kifedha yaani shida zako zote unataka mwanamume akusaidie kiukweli si kitu kizuri ndiyo maana baadhi ya wanaume wakiona tabia kama hizi basi anaanza kukata mawasiliano taratibu mwishowe ukimpigia simu hapokei kabisa .Ni muhimu kujituma ili usiwe ombaomba kila wakati kwani inawezekana mwanamume akakuchoka kutokana na wewe kila wakati kutaka pesa, ijapokuwa wapo baadhi ya wanaume wana huruma na wako tayari kukusaidia kwa lolote ambalo lipo ndani ya uwezo wake hata kama hana uwezo mkubwa kifedha pamoja na hayo usiwe tegemezi fanya kazi kwa bidii ili hata ikitokea na yeye anahitaji msaada wako basi unamsaidia. na hili ni kwa wote mwanamke na mwanamume tushirikiane na si kumuacha mmoja aumie zaidi

WANAFUNZI 43 CHUO KIKUU CHA MLIMANI WAFUKUZWA

Chuo kikuu cha Dar es salaam kimewafukuza wanafunzi wapatao 43 kati ya 51 ambao walilkuwa ni vinara katika matukio na vurugu zilizojitokeza hivi karibuni , katika wanafunzi hao wanafunzi tisa wame simamishwa masomo kwa muda wa takribani miez tisa(9).
 Hatua hii imefikiwa mara baada ya wanachuo hao kuvunja baadhi ya vitu na ofisin baadhi za utawala  ,huku wanafunzi hao wakiwazuia baadhi ya maofisa na wafanyakazi wa chuo kuweza kufanya shungul zao za kila siku kkwa kuwahamasisha wafanyakazi hao watoe mustakabali wa taarifa za pesa zao kutoka bodi ya mikopo(heslb) .
Wanafunzi hao waliokuwa wanaendeleza mgomo wao ulioanza Jumatatu wiki hii wakidai taarifa za kwa nini pesa zao zinachelewa wakati bodi ya mikopo, ilishasema wamezileta chuoni hapo. Akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam jana Makamu Mkuu wa Chuo hicho, Profesa Rwekaza Mukandala alisema hatua hiyo imekuja baada ya kuongezeka kwa vitendo vya kihalifu na uvunjifu wa amani chuoni hapo tangu mwanzo wa juma hili.

“Desemba 13 (Jumanne) Kamati ya Wakuu wa Chuo na Shule Kuu zilizoko kampasi kuu ya Mlimani walifanya kikao cha dharura na kufanya mapendekezo kuhusu hatua za kuchukuliwa ili kusitisha uhalifu chuoni,”alisema Mukandala na kuongeza:

“Siku hiyo hiyo Baraza la Chuo nalo lilifanya kikao cha dharura na kutathimi mwelekeo wa chuo na kupitia mapendekezo yaliyoletwa na Kamati ya Wakuu wa chuo na shule kuu na kutoa maamuzi.”. Profesa Mukandala alisema, maamuzi yaliyotolewa na vikao hivyo ni pamoja na kuwafukuza wanafunzi hao 43 na kuchukua hatua za kuongeza ulinzi kwa muda katika maeneo muhimu ya chuo ili wanafunzi walio wengi waendelee kusoma bila kusumbuliwa.

Alisema kati ya wanafunzi hao 43, wanafunzi wanane ni wale ambao walisimamishwa masomo kwa muda wa miezi tisa, lakini waliendelea kuonekana maeneo mbalimbali ya chuo hicho huku wakilazimisha kuonana na uongozi. “Kuna hawa 35 ambao ni kati ya wale wanafunzi 51 waliokuwa na kesi mahakamani nao wamefukuzwa, kati ya hao 51 ilibainika kwamba watatu hawakuwa wanafunzi wa UDSM, hivyo wanafunzi walikuwa 48 tu,” alisema Profesa Mukandala.
hizi baadhi ya matukio yanaohusisha makamu mkuu wa chuo kikuu cha dar es salaam Prof Rwekaza Mukandala na wanafunzi walikokuwa wakiwa wanaendeleza migomo.

Dec 14, 2011

WATU WANENE HUISHI MIAKA MINGI KULIKO WATU WEMBAMBA

     Hatimaye habari nzuri kwa watu wanene, Utafiti uliofanywa na wanasayansi wa Japan kwa watu 50,000 kwa jumla ya miaka 12 umeonyesha kuwa watu wanene wanaishi miaka sita zaidi ya watu wembamba. Wakati watu wanene kila siku wamekuwa wakifanya kila wawezalo ili kupunguza uzito wao, utafiti uliofanywa na timu ya wizara ya afya ya Japan iliyoongozwa na Profesa Shinichi Kuriyama wa chuo kikuu cha Tohoku umeonyesha kuwa watu wanene huishi miaka mingi kulinganisha na watu wembamba.

Utafiti huo ulifanywa kwenye mji wa Miyagi uliopo kaskazini mwa Japan ukiwashirikisha watu 50,000 wenye umri wa miaka kati ya 40 na 79.

Matokeo ya utafiti huo yalionyesha kuwa watu wembamba huishi miaka sita pungufu ya watu wanene.

Utafiti huo uliofanyika kwa jumla ya miaka 12 uliwashirikisha wanawake kwa wanaume wenye umri zaidi ya miaka 40.

Utafiti huo ulifanyika kwa kuangalia vielelezo vya unene na urefu wa mtu (BMI) ambapo kipimo chake kuwa katika mfumo wa kilo kg/m2.

Utafiti huo ulionyesha kuwa watu wenye unene wa wastani (BMI kati ya 18.5 na 25) wenye umri zaidi ya miaka 40 huishi miaka miwili pungufu ya watu wanene kidogo (BMI kati ya 25-30) wakati watu wembamba sana (BMI chini ya 18) huishi miaka sita pungufu ya watu wanene sana (BMI zaidi ya 30).


  1. Sababu iliyochangia watu wembamba kuwa na maisha mafupi kulinganisha na watu wanene ilisemekana kuwa ni kutokana na kwamba watu wengi wembamba hupenda kuvuta sigara na pia kutokana na kwamba watu wembamba miili yao huwa dhaifu katika kupambana na maradhi sugu


Hata hivyo Profesa Kuriyama alishauri watu waendelee kula vizuri na wasibweteke na kujiachia kuwa wanene, badala yake wajitahidi kuwa katika uzito wa wastani unaopendekezwa na mashirika ya afya duniani.

Utafiti huo ulionyesha pia kuwa jinsi mtu anavyozidi kuwa mnene ndivyo gharama za matibabu yake zinavyozidi kuongezeka.

HABARI ZILZOTAWALA MAGAZETI YA LEO








TUTAMKUMBUKA MR EBBO

NI msanii wa bongo ambaye jina lake la asili ni Abel Loshilaa Motika, aka Mr Ebbo, amefariki dunia akiwa na umri wa miaka 37.mr ebbo alilanzwa katika hospitali ya Mission Usa River ambapo alikuwa akipatiwa matibabu ya ugonjwa uliokuwa ukimsumbua hadi hapo mahuti yalipomfika.
MR EBBO ametoa nyimbo mbalimbali na album wakaza wakaza ambazo ni:

 
Albums by Mr Ebbo
Fahari Yako- 2002
Bado- 2003
Kazi Gani- 2004
Alibamu- 2005
Kamongo -2006
tunakukumbuka kwa mchango wako katika tasnia nzima ya kuinua na kuendeleza mziki wa kizazi kipya.
mungu ailaze roho ya marehemu mahal pema peponi,AMIN.