Aug 1, 2012

BARNABA, 2FACE,CABO SNOOP,FALLY IPUPA NDANI YA JUKWAA MOJA KATIKA AFRICA UNPLUGGED CONCERT YA LONDON MWEZI HUU


Barnaba kutumbuiza kwenye Africa Unplugged Concert ya London mwezi huu

Mwezi huu msanii wa THT Barnaba atapanda kwenye tamasha kubwa la wasanii wa Afrika kuwahi kutokea mjini London, Uingereza lililopewa jina la Africa Unplugged Concert.
Kenya na Uganda zitawakilishwa na Madtraxx pamoja na Jose Chameleone.
Tamasha hilo lililopewa sifa kama THE LARGEST AFRICAN CONCERT IN EUROPE...EVER litafanyika kwenye uwanja wa Wembley,  August the 27 kuanzia saa 6:00 muda wa huko.
Wasanii wengine watakaotumbuiza ni 2Face (Nigeria) | Zahara (South Africa) |Cabo Snoop (Angola) | Fally Ipupa (Congo) | R2bees (Ghana) | Sarkodie (Ghana) | Flavour (Nigeria) | DJ Arafat (Ivory Coast) | Iyanya (Nigeria) | Zakes Bantwini (South Africa) |  Winky D (Zimbabwe) | Mc Inity (Zimbabwe)
Sehemu ya mapato ya tamasha hilo yatatumika kuwasaidia watoto walioathirika na vita nchini DRC.
Tiketi zinauzwa paundi 25.

No comments:

Post a Comment