Sep 12, 2012

mshahara wa shomary kapombe , ni sawa na juma kaseja


Kapombe kulia akiwa amebeba Ngao aliitolea jasho la kutosha tu juzi, Kushoto ni Meneja Vifaa vya michezo wa Simba, Kessy Kaburu

 
      KIRAKA Shomary Kapombe anapigiwa debe aongezewe mshahara kutoka Sh, 800,000 anazolipwa sasa hadi Sh, Milioni 1, sawa na mastaa wengine wa Simba, mfano Juma Kaseja na Mwinyi Kazimoto, ambao wote hawafui dafu kwa Mrisho Ngassa anayelipwa Sh. Milioni 2.
     kupitia mtandao wa BIN ZUBEIRY  umeripoti kuwa taarifa imezipata zinasema kwamba, Kapombe aliongezewa mshahara kutoka Sh. 400,000 baada ya beki Kevin Yondan kutimkia Yanga na miezi mitatu badaaye, yuko kwenye nafasi ya kuongezewa 200,000 zaidi.
       Hata akipewa Milioni 1, bado Kapombe hatawafikia mabeki wa kigeni Komabil Keita na Paschal Ochieng ambao bila kupepesa macho, wote hawamfikii kwa uwezo wa kazi uwanjani.
Kapombe amekuwa akiibeba mno Simba katika mechi za karibuni na ushindi wa Ngao ya Jamii juzi, mabao 3-2 dhidi ya Azam FC, kwenye Uwanja wa Taifa, Dar e s Salaam mchezaji huyo alifanya kazi kubwa mno.
         Kapombe anaweza kucheza beki ya kulia, beki wa kati na nafasi yoyote ya kiungo kuanzia ukabaji, pembeni na katikati.
Siyo tu soka anaijua, bali pia Kapombe hujituma uwanjani, ingawa siku zote ukikutana naye nje ya Uwanja ni kijana mpole na mtiifu. Kapombe si tegemeo kwa Simba SC tu, bali hata timu ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars.
       Huwezi amini, Mwanamichezo huyo bora wa TASWA ndio kwanza anaingia katika msimu wake wa pili Simba SC tangu asajiliwe kutoka Polisi Morogoro, wakati huo ikiwa Daraja la Kwanza. 
 Follow @mwendapole1 on Twitter!
Like us on Facebook!

No comments:

Post a Comment