Dec 28, 2011

HALIMA MCHUKA AFARIKI

MWANAMKE mtangazaji wa kituo cha habari cha TBC ,HALIMA MCHUKA amefariki dunia leo alfajiri ,inasemekana HALIMA alikuwa akisumbuliwa na tatizo la ugonjwa wa kiharusi ambalo limejirudia hiyo jana akiwa kazini.
Tatizo ls ugonjwa huu lilishawahi kumpata mnamo mwaka 2007 januari na kupelekea kulazwa hospitalini ambapo wakati akiendelea kupata matibabu katika mwaka 2007 aliweza kutembelewa na mheshima rais Dk Jakaya kikwete na mkeo, kama picha inavyoonesha hapo chini.

kwa taarifa niliyoisikia TBC inasema kuwa "ALIKUWA NA TATIZO HILO JANA MCHANA MARA BAADA YA KUTANGANZA KIPINDI CHA SALAAMU CHA TBC_TAIFA na akazidiwa ndipo alipopelekwa hospitalini kwa matibabu zaidi.
                                          kwenye picha ni aliyesimama katikati
HALIMA MCHUKA alijiunga na RADIO TANZANIA DAR ES SALAAM  mnamo miaka ya 1990 ambapo alikuwa ni mtangazaji mzuri wa mchezo wa soka(mpira) uwanjani.
Mungu alitoa na mungu ametwaa, mungu ailaze roho ya marehemu mahali pema peponi AMINA.
                                           marehemu HALIMA MCHUKA

No comments:

Post a Comment