Dec 19, 2011

KIM JONG IL AFARIKI DUNIA

Televisheni ya serikali ya korea ya kaskazini imetangaza kuwa kiongoz wa nchi hiyo, kim jung Il, amefariki dunia kwenye treni katika ziara ya kikazi ,baada ya kuzidiwa na shinikizo la damu la ghafla.
 China imesema ina majonzi sana kwa kifo cha kim Jon Il na  imeungana na raia wa korea kaskazini kuomboleza kifo cha swahiba wake mkubwa.Rais BARACK OBAMA wa marekani amempigia simu mwenzake wa korea kusini,Lee Myung-Bak, usiku wa manane, kutathimini kifo hcho.usalama na ulinzi umeimarishwa mpakani mwa korea hizo mbili. Na huko japan  masoko ya hisa yameanguka kwa zaidi a asilimia 1.26 kufuatia taarifa za kifo hiki.
jong Il aliingia madarakani mwaka 1994 baada ya kifo cha ghafla cha baba yake Kim Il sung , ambaye alikuwa ameliongoza taifa hilo tangu mwaka 1948.  mafaniko ya kim jong Il yalikuwa ni kuivaa tabia na haiba ya baba yake, na hivyo kujijengea mvuto ambao kabla hakuwa nao.wengi wanasema kuwepo madarakani kwa jong Il madarakani kulikuwa ni sawa na kuwepo kwa Il sung.
   Kielimu, Kim Jong Il alisoma kwanza nchini China kabla ya kujiunga na chuo kikuu cha Kim Il Sung mjini Pyongyang alikosomea siasa na uchumi. Aliingia rasmi kwenye siasa mwaka 1964, kwa kujiunga na chama pekee cha siasa, chama tawala cha Wafanyakazi cha Korea, ambako alipanda vyeo haraka haraka.
Waombolezaji nchini Korea Kaskazini.Waombolezaji nchini Korea Kaskazini.Akiwa na miaka 31 tu hapo mwaka 1973, aliteuliwa kuwa katibu mkuu wa mipango na propaganda, na mwaka mmoja baadaye akatangazwa rasmi kuwa mrithi wa baba yake. Mwaka 1980 aliingia kwenye Kamati ya Ulinzi, ambacho ndicho chombo cha juu kabisa kiutawala. Mwaka 1991 akatangazwa kuwa kamanda mkuu wa majeshi.
Si mengi yanayojulikana na ulimwengu wa nje kuhusu kiongozi huyo. Vyombo vya habari vya Magharibi vinajaribu kumuelezea kama mwanamme anayevaa suti za Mao na miwani meusi, anayependa wanawake, ulevi, vyakula na magari ya kifahari, lakini asiye na ufahamu sana wa mambo ya dunia. Maisha yake binafsi, yakiwemo mahusiano yake na maisha ya watoto wake wanne, yalikuwa ni mwiko kuzungumzwa kwenye vyombo vya habari vya serikali.

No comments:

Post a Comment