Jan 10, 2012

shirika la umeme Tanzania

Shirika la Umeme nchini-TANESCO limeanza mchakato wa kupeleka huduma ya umeme kwa wananchi wa tarafa ya IGALULA wilayani UYUI kwa gharama ya shilingi Bilioni MOJA na Milioni 600.
Kauli hiyo imetolewa na Mbunge wa Jimbo la IGALULA, Dakta ATHUMAN MFUTAKAMBA wakati akizungumza na wananchi wa kata ya GOWEKO ambapo amewahakikishia wananchi wa jimbo hilo kwamba atahakikisha anasimamia mchakato wa kuwapelekea umeme unakamilika haraka iwezekanavyo.

No comments:

Post a Comment