Jan 10, 2012

we unasemaje?

Default Mwalimu Christopher Mwakasege: Je anatumia nguvu za giza au nguvu za Mungu wa Israel?

Naombeni msaada wenu, nimesikia mengi sana juu ya Mwalimu Mwakasege kuwa ana ponya na anatenda miujiza, lakini hana kanisa, na hata akikusanya sadaka anawaachia waandaaji wa hiyo mikutano waliyo mwalika.
hakika nina imani naye sana, lakini nilichokisikia leo kwenye kanisa moja la kiroho ndio kinanifanya nihoji wanajamii wenzangu kama kweli nguvu za Mwalimu huyu ni zile za Nigeria au za Mbinguni.
Kwenye kanisa letu la kiroho, Nabii wetu katuambia kuwa Mwakasege anaenda Nigeria kila baada ya wiki mbili na akienda huko miujiza na nguvu zake huongezeka mara dufu.
Nimejaribu kuingia kwenye web page yake ya Yohana 21:17* Yesu akamwambia "Lisha Kondoo Zangu". sijaona ratiba zake.
Mwenye ujuzi wa hili naomba atutoe shaka.

No comments:

Post a Comment