Mar 9, 2012

NI VEMA KUTAFAKARI MAISHA YAKO


Katika safari ya mahusiano ya kimapenzi kuna vitu vingi hujitokeza vizuri na wakati mwingine vibaya na katika hili kuna baadhi ya watu ambao wanapenda sana kuchunguza mahusiano ya watu wengine huku wakitaka kujua ndani ya uhusiano huo kuna nini?? kwa mfano unakuta mtu anachunguza mambo ambayo mwanamke au mwanamume anamfanyia mpenzi wake kama amempa zawadi,,ametoka naye,,anawasiliana naye vipi mwanzoni alikuwa na uhusiano na nani? anakula nini?? yaani mwingine atataka kujua hadi mambo ya chumbani yanafanyika vipi??
Ukweli ni kwamba huo ni umbea uliokithiri ni vyema kuwa makini nakufanya mambo ya maendeleo kuliko kuchunguza mahusiano yasiyokuhusu mwisho wa siku utaumbuka na mara nyingi watu hawa huwa ni wivu ama chuki inawasumbua hivyo hawapendi kuona wawili wakipendana . NI VYEMA KUTAFAKARI MAISHA YAKO KULIKO KUKAA NA KUWAZA KUMCHUNGUZA FULANI ANAFANYA NINI.......

No comments:

Post a Comment