Apr 22, 2012

WASANII WATANO WA HIP HOP WENYE MKWAJA WA KUTOSHA





Forbes imetangaza majina matano ya wasanii
 wa hip hop wenye mkwanja, Alieongoza
kwenye list hiyo ya forbes ni Sean “Diddy”
Combs akifuatiwa na Jay- Z, 50 cent,
Bryan “ Birdman” Williams na Dr Dre.
Diddy aliongoza kwa kuwa na dola milioni mia 
tano na hamsini ($550)..Vitega uchumi vya
 Diddy ana kinywaji ya Ciroc Vodka, kampuni
ya nguo za Sean John na Enyce, Record label
yake ya Bad Boy na vitu vingine alivyovianzisha
 ukiongezea na cable channel yake ya Revolt
itamfanya awe billionaire mwaka 2013.

Jay – Z anafuatia akiwa nafasi ya pili akiwa na
dola milioni mia nne na sitini ($460) kutokana
mauzo ya mavazi ya Rocawear milioni mia mbili
na 4 ($204) mwaka 2007. Dr Dre anafuata kwa
kuwa na dola milioni mia mbili na sabini ($270)
kutokana kitega uchumi chake cha Beats Electronics,
Wakati Birdman akishika nafasi ya nne (4) akiwa
anamiliki dola milioni mia ishirini na tano ($125)
kwa jina lake. Na 50 cent akafunga kwa kuwa
na dola milioni mia na kumi ($110) bank. Forbes
pia imetabiri kuwa Sean “ Diddy” Combs atakuwa
 msanii billionaire wa hip hop. 
Na Dj fetty

SUGE KNIGHT AMTISHIA RICK ROSS ASIFANYE NGOMA ITAKAYOITWA "TUPAC BACK" KAMA DIDDY ATAHUSIKA




Aliyekuwa mmiliki wa Death Row mkali Suge Knight
 ametishia kumletea noma kwa Rick Ross, wakati 
Suge Knight akidhani labda 2Pac anaweza akawa
 ajafa imesababisha Suge kuwa talk of the town, 
inaonekana hicho sio tu alichokisema wakati wa mahojiano
 na 93.5 KDay. Suge Knight alitishia kummind Rick Ross
 kwa ajili ya ngoma ya “Tupac Back”.

Kwenye mahojiano hayo ndani ya 93.5 KDay  na Tatoo
 na Cee Cee, Suge Knight alisema mshikaji akivuka 
mipaka itakua noma, Rozay namkubali sana, anajua
 kuandika anabars za ukweli misina nae noma ila akiwa 
kwa Diddy alafu afanye ngoma inaitwa Tupac Back
 itakuwa noma…Suge Knight anajua Diddy ndo anahusika
 na kifo cha mkali Tupac Amaru Shakur “Siwezi nikakaa
 hapa alafu nikasema namchukia Rozay” alisema Suge Knight.

 “ Coz Kama mtu mwingine yeyote hatumjui Rozay ni mchizi 
anaetumia jina la mtu mwingine kwanza alikuwa askari magereza, 
sio kama namchana wala sina chuki binafsi anafanya good music
 huwezi kuondoa hicho kwake” . Kwa sasa audio ya mahojiano
 hayo tayari yameshatolewa rasmi ili watu waweze kusikia,
 93.5 KDay wanaicheza kwa kuridia mara kwa mara.
na dj fetty

The Dogg - Forget (Official Video) (HD)



Adele nominated for 18 Billboard Music Awards

Adele nominated for 18 Billboard Music Awards 
 

Adele has been nominated for 18 awards for this year's Billboard Music Awards. She is nominated for top Billboard 200 artist and top female artist amongst many more nominations. Rihanna and LMFAO have also been nominated for the Billboard Music Awards this year. The Hollywood Reporter reports:

NEW YORK -- Adele, LMFAO, Rihanna, Lady Gaga and Lil Wayne lead the finalists for the 2012 Billboard Music Awards, which will air live from the MGM Grand Arena in Las Vegas on May 20.

Adele takes the lead as a finalist in 18 award categories, including Top Artist, Top Female Artist and Top Billboard 200 Artist. "Rolling In The Deep," the lead single from her blockbuster sophomore album 21, places the U.K. singer as a contender in seven song categories.

Meanwhile, LMFAO is a finalist in 17 award categories, although the electro-pop duo actually scored 22 entries compared to Adele's 20. LMFAO and Adele will square off in the Top Hot 100 Artist category, which also includes Bruno Mars, Katy Perry and Rihanna.

 

TETESI KUHUSU KIUNGO WA KIMATAIFA NIZAR KHALFAN

Kiungo wa kimataifa wa Tanzania Nizar Khalfan aliyekuwa anacheza soka lakulipwa Marekani katika clubs ya Vancouver Whitecaps FC na Philadelphia Union (Major League Soccer) amesajiliwa na Simba SC.

YALIYOJIRI FACEBOOK,TWIITER &JAMII FORUMS

http://millardayo.com/wp-content/uploads/2012/04/Z-Anto-on-kisiwa-cha-malavidavi-April-22-2012.png



Br3aKiNg n3wZ. REST IN PEACE SAJUKI. Aliyekuwa mkali katika movie za kibongo na mume wa wastara bwana sajuki afariki leo usiku!mungu ailaze roho ya marehemu mahala pema peponi amina! Chanzo Cha Habari www.jamiiforums.com

WABUNGE WAZALENDO WAMETAFAKARI NA WAMECHUKUA HATUA DHIDI YA WIZI

KUONGEA SI KUTENDA ! Wabunge wazalendo wametafakari na kuchukua hatua dhidi ya wizi na ubadhirifu wa fedha za umma kwa maslahi ya Taifa. Je mbunge uliyemchagua yuko katika kundi gani?Je ana na njema na Taifa letu, Anafanya nini panapokuwa na uthibitisho kuwa mabilioni ya fedha ambayo yangesaidia kuboresha huduma za jamii yametumika kizembe au yametafunwa na waliopewa dhamana ya uongozi, Anaungana na wenzake katika kubadilisha hali hiyo au anatanguliza maslahi yake binafsi kwa sababu hakuna chama chochote ambacho kina sera ya WIZI NA UBADHIRIFU hiyo ni sera ya VIONGOZI WABINAFSI, NDULI, DHALIMU, KUPE, MAFISADI, WAOGA NA WANAFKI. Je ulipomchagua ulitegemea kumpa madaraka na cheo ili akalamike au atumie cheo chake kuboresha maisha ya watanzania , Unadhani amewajengea heshima wananchi wa jimbo lenu au amewaletea fedhea. TAFAKARI NA CHUKUA HATUA. MUNGU IBARIKI TANZANIA , MUNGU IBARIKI AFRIKA
na CG FM RADIO

Apr 19, 2012

Boy fights disease that turns muscle into bone

Lil K feat Baraka Winner

YALIYOJIRI FACEBOOK & TWITTER

HISIA ZA UKWELI HUONEKANA KATIKA MAPENZI YA KWELI

Hisia za kweli huonekana katika mapenzi ya kweli

Ni vigumu sana kuishi kwa furaha na mpenzi ambaye moyoni mwako hauna hisia juu yake. Na hii ni kutokana na kujikuta umependa kwasababu ya maslahi kwamba unachokitaka ni pesa ama umeamua kuishi naye kutokana na kumuonea huruma, vilevile kutokana na shinikizo la ndugu nk, ni jambo la muhimu sana kuzingatia hisia ulizonazo inapendeza na ni furaha kuwa na mwenza unayempenda kwa kila kitu yaani hisia zako juu yake ni za kweli na yeye pia awe na hisia za kweli juu yako vinginevyo kama hakuna hisia za kweli basi migogoro inaweza kujitokeza mara kwa mara na kupelekea kutokuwa na penzi la kudumu furaha yako italetwa na namna ambavyo unafuata hisia zako na si kufanya kwa kuiga, tamaa au kujilazimisha

KUJITAMBUA NA KUSIHI KAMA ULIVYO



Katika maisha ni vyema sana kujitambua na kuishi kama ulivyo, ni wazi kabisa binadamu tumeumbwa na tabia tofauti, lakini ukijitambua basi utajikubali na kujua nini ufanye katika maisha yako na unaweza kuishi vizuri kuliko kujiingiza katika matatizo ama shida ambazo zinaweza kukukumba kwasababu ya kutaka kuishi maisha kama ya mtu fulani au mtu mwingine, wapo watu hawalali wapo radhi kuiba, kufanya ukahaba alimradi awe na maisha kama ya fulani, kama fulani ana gari au nyumba ya kifahari isiwe kwako tatizo na kujiona kama maisha haujayapatia maana huwezi kujua mwenzio amepata kwa njia gani. jitambue na ongeza juhudi katika kazi yako na utafikia malengo yako ni mbaya sana kulazimisha kufanya jambo bila juhudi.
Na:Corleone 

USHOGA WASHAMILI

Katika hali isiyo yakawaida ni jambo la aibu kumuona au kuwaona vijana wa sasa wanavyopotea kimaadili. hivi sasa jamii yetu imekuwa ikikubwa na tatizo kubwa la vijana wanawake kwa wanaume ,ambapo wasichana siku hizi wameamua kuvaa nguo nusu uchi ili kudhilisha nafsi zao na bila kusahau wanachukulia nafasi hiyo kama mwanya wa kuwapata wakina kaka.
  leo sitaki kuzungumzia huko ila ningependa kuzungumzia hali inayozidi kuzitokeza hivi sasa katika jiji letu hili, nimeshikitishwa sana na kitendo cha kuwaona vijana kama hawa(rejea picha hapo pembeni), wamekutwa wakijianika wazi wazi pasipo hata haya au aibu miongoni mwao. Hivi kwa sasa dunia yetu hii inaelekea wapi ikiwa vijana wakiume nao wameanza kufanya shunguli ya uchangudoa? inasikitisha sana endapo ukiwa kama mzazi au mlezi ambaye unaona kizazi hiki kinazidi kuwa cha nyoka.

    Ndugu wazazi na walezi tujitaidi kuwalea watoto wetu katika maadili mazuri na yenye kumpendeza mwenyezi mungu,ni aibu sana kwa kijana hasa wakiume kumuona akijianika wazi wazi mbele ya umati wa watu na kujiita sijui shosti au dada fulani?inabidi ifikie kipindi sisi kama wananchi(wazazi,walezi) na serikali pia iangalie upya sheria zake za maadili kwa vijana maana tunakoelekea si kuzuli .Tunatengeneza taifa gani lisilokuwa na maadili mazuri?.

Apr 18, 2012

Past exam papers | ACCA | ACCA Global

Past exam papers | ACCA | ACCA Global

DK JOHN MAKUFULI AZIDIWA GHAFLA

Habari zilizotufikia muda si mrefu zinaeleza kuwa waziri  wa ujenzi wa jamhuri  ya muungano wa Tanzania DK JOHN POMBE MAKUFULI amezidiwa ghafla huko DODOMA ambako taarifa zinasema kuwa dk makufuli amekimbizwa hospitali ,tukio hili limetokea wakati bunge la tisa likiendelea DODOMA.
  Kwa mujibu wa naibu spika bwana  JOB NDUGAI ameeleza ya kwamba DK makufuli alishikwa na homa kali hali iliyopelekea kukimbizwa GENERAL HOSPITAL ,DODOMA.
 

Na. mpekuzi

Ferguson Comments on Title Race

MANENO MACHACHE AMBAYO KOCHA WA MAN UNITED AMEYATOA KUELEZEA HISIA ZAKE JUU YA USHINDANI WA UBINGWA BAINA YAKE NA MAN CITY

MBUNGE WA TEMEKE APATA AJALI

MBUNGE WA TEMEKEMH.ABASS MTEVU APATA AJALI YA GARI AKIWA NJIANI KUELEKEA DAR ES SALAAM



Abass Mtemvu
Mbunge wa Temeke  
Abass Mtevu na dereva 
wake ambaye jina lake
 hakutajwa, wamenusurika 
kifo baada ya kupata
 ajali ya gari  wakiwa 
njiani kuja Dar es Salaam.


Akitoa taarifa bungeni 

mchana huu, 
Naibu Spika wa Bunge Job Ndugai 
amesema baada ya ajali iliyosababishia
 majeraha kadhaa mwilini, Mtemvu na
 dereva wake wametibiwa katika
 hospitali ya Morogoro na 
kuruhusiwa kuja Dar.


"Wamenusurika ingawa wamepata

 majera kadhaa mwilini, na hivi 
ninavyozungumza wapo njiani
 kwenda Dar es Salaam" alisema 
Ndugai kuwaambia wabunge.

Apr 10, 2012

MATUKIO MBALIMBALI KATIKA PICHA KAMA ILIVYOKUWA JANA NYUMBANI KW MAREHEMU STEVEN KANUMBA


 MATUKIO MBALIMBALI YALIYOJITOKEZA KATIKA MSIBA WA MAREHEMU STEVEN KANUMBA
 Ikiwa ni siku ya tatu ya msiba uliojitokeza wa ndugu yetu mpendwa bwana STEVEN KANUMBA, ambaye amepatwa na umauti katika tukio lisilo tegemewa .baada ya kutokea kwa ugomvi kati yake na msanii mwenzake wa kike ELIZABETH MICHAEL “LULU”.

  Wananchi mbalimbali wakiwemo wasanii ,viongozi wa serikali na wapenzi wa tasnia ya filamu wameendelea kujitokeza kutoa pole kwa familia ya ndugu KANUMBA ,kwa kuonesha ni jinsi gani umauti wa msanii wa filamu wenzao ulivyowagusa huku wakiwa na vipeperushi na t-shirt zenye kuonesha kumbukumbu au kuguswa kwa namna moja au nyingine.

Hizi baadhi ya t-shirt ambazo wananchi na wapenzi wa marehemu steven kanumba wamekutwa wamevaa maeneo mbalimbali ya jiji la Dar es salaam,
 
       Hizi baadhi ya picha zinazoesha upenzi wa wanachi kwa hayati steven kanumba

Hata hivyo niliweza kutembelea eneo alilokuwa akiishi marehemu steven kanumba na kujionea umati mkubwa wa watu waliojitokeza kutoa pole na kuunguna na wasanii wa tasnia ya filamu katika wakati huu mgumu wa kifo cha mpendwa steven kanumba.
 Hawa ni baadhi ya watangazaji na waandishi waliojitokeza hii leo katika kutoa pole nyumbani kwa marehemu KANUMBA.
 Msanii chaz baba akishungulisha na ugawaji wa chakula na vinywaji wakati wa mida ya mchana hii leo.
              AMINI, DITTO na KWAMBI walipojokeza katika kutoa pole nyumban kwa marehemu kanumba.
Wasanii wa maigizo katika moja ya mawasilano ili kuakikisha kila kitu kinaenda sawa.
MUNGU AILAZE ROHO YA MAREHEMU MAHALI PEMA PEPONI,MUNGU ALITOA NA MUNGU ALIMETWAA.AMIN

Apr 5, 2012

CHRISTIAN RONALDO NI BORA KULIKO MESSI?

Wataalamu wa mambo ya masoko wametanabaisha kuwa mshambuliaji wa Real Madrid Christiano Ronaldo ana thamani kubwa kuliko mchezaji bora wa sasa  wa dunia na klabu ya Barcelona Lionel Messi.
Chuo kimoja kinachojihusisha na mambo ya masoko cha IPAM kilifanaya utafiti na kugundua kuwa Ronaldo ni jina kubwa sana na linalouza sana katika masuala ya masoko.
Jina la mchezaji Ronaldo ni maarufu sana kwenye mitandao mingi sana duniani, Ana mashabiki wengi sana kuliko Messi kwenye mtandao wa kijamii wa Facebook (ambapo Ronaldo ana mashabiki milioni 42 wakati Messi ana mashabiki milioni 34), kwenye mtandao wa Google Ronaldo ametafutwa zaidi ya mara milioni 139 sawa na milioni 80 zaidi ya Messi, ana jumla ya video 212,000 zilizowekwa kwenye mtandao wa Youtube,wakati kwenye mtandao wa kijamii wa Twitter kuna watu zaidi ya milioni 8 wanaomfuata.
Umaarurfu wa Ronaldo kwenye soko unachangiwa sana na masuala ya kijamii. Nyota huyo kutoka nchini Ureno ametokea kwenye vitabu 205 vya Amazon (wakati Messi ametokea kwenye vitabu 85),pia ametokea kwenye nakala 2157 za kisayansi (wakati Messi ametokea kwenye nakala 1608). Kwenye umaarufu kama ilivyoandikwa kwenye jarida la Forbes Ronaldo anashika nafasi 47 wakati Messi anashika nafasi ya 62.
Chuo hicho cha masoko cha IPAM kinaamini Ronaldo anathamani ya €40 million kwa mwaka ukilinganisha na €37 million ya Messi kwa mwaka.

YANGA ADHABU YAWAKABILI

Na Dina Ismail

KIKAO cha Kamati ya Nidhamu ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) kimemalizika majira ya saa 5:30 usiku huu na kimegoma kujadili suala la klabu ya Yanga kuponywa pointi na Kamati ya Ligi Kuu ya Vodacom ya Tanzania Bara, ikiitaka klabu hiyo ikate rufaa maaulm juu ya hilo.


Mwenyekiti wa Yanga, Wakili Lloyd Baharagu Nchunga aliyekuwapo kwenye kikao hicho, ameiambia bongostaz dakika chache zilizopita kwamba, kwa kuwa hawakuwasilisha rufaa ya kupinga kupokonywa pointi za Coastal Union, wametakiwa kufanya hivyo ndipo suala hilo lijadiliwe.
Hata hivyo, Nchunga alisema kwamba Kamati hiyo, imewapunzia adhabu wachezaji wote watano wa Yanga walioadhibiwa na Kamati ya Ligi Kuu katika kikao chake cha Machi 12, mwaka huu kwa tuhuma za utovu wa nidhamu walioufanya kwenye mechi ya Azam FC, Machi 10, mwaka huu, Uwanja wa Taifa.

Hao ni Stefano Mwasyika aliyempiga ngumi refa wa mechi hiyo Israel Nkongo ambaye awali alihukumiwa mwaka mmoja na faini ya Sh Milioni 1, ambaye sasa amehukumiwa kukosa mechi zilizobaki za msimu na faini ya Sh. Milioni 2 sawa na mshambuliaji Jerry Tegete ambaye awali alihukumiwa kukosa mechi tatu na adhabu ya Sh, 500,000.

Beki Nadir Haroub ‘Cannavaro’ ambaye awali alihukumiwa kukosa mechi sita na faini ya Sh. 500,000, sasa atakosa mechi tatu na faini ya tatu, wakati viungo Nurdin Bakari na Omega Seme sasa watakosa mechi mbili na faini ya Sh. Milioni 1 kila mmoja.

Awali, Nurdin alihukumiwa mechi tatu na faini Sh. 500,000 sawa na Omega Seme.

Yanga ilipokonywa pointi hizo kwa kosa la kumtumia beki Nadir Haroub ‘Cannavaro’ katika mechi dhidi ya Coastal Union, kwenye Uwanja wa Mkwakwani mjini Tanga Jumamosi,
Coastal ilicheza chini ya pingamizi katika mchezo huo, ambao ilifungwa 1-0 ikipinga klabu hiyo kumtumia beki Nadir Haroub ‘Cannavaro’ ikidai alikuwa hajamaliza adhabu yake ya kukosa mechi tatu baada ya kupewa kadi nyekundu kwa vurugu kwenye mechi dhidi ya Azam FC
Nchunga alisema waliamua kumtumia Cannavaro baada ya Mwenyekiti wa Kamati ya Nidhamu na Usuluhishi ya TFF, Alfred Tibaigana kusitisha adhabu zote zilizotolewa na Kamati ya Ligi kuwafungia wachezaji watano wa Yanga kwa kufanya fujo kwenye mechi na Azam FC, ikiwemo kumpiga refa.
Awali, wiki iliyopita Tibaigana alisitisha adhabu zote akidai kwamba Kamati ya Ligi haina mamlaka ya kutoa adhabu, ispokuwa Kamati yake.
Kwa matokeo hayo, Yanga sasa inabaki nafasi ya tatu kwenye msimamo wa Ligi Kuu kwa pointi zake 44, baada ya kucheza mechi 21, wakati Azam iliyocheza mechi 22 ina pointi 46 na inaendelea kubaki nafasi ya pili.
Simba inayoongoza ligi hiyo kwa pointi zake 50, nayo imecheza mechi 22, moja zaidi, dhidi ya mabingwa watetezi, Yanga.
Nchunga alisema mapema kesho watawasilisha rufaa nyingine kwa Kamati hiyo, kupinga maamuzi ya Kamati ya Ligi Kuu kuwapokonya pointi za ushindi wa Tanga kwa sababu walimtumia beki huyo baada ya maamuzi ya Kamati ya Tibaigana.
Aidha, Nchunga alikana taarifa za kwamba walionywa kutomchezesha Cannavaro katika mechi ya Tanga kabla ya mchezo huo.
“Sikusikia kitu kama hicho, kwa nini tumtumie kama tungepewa angalizo, tumecheza mechi ngapi bila Cannavaro na tumeshinda, iweje tulazimishe kumtumia kwenye mechi hiyo,”alisema Nchunga.