Dec 14, 2011

WATU WANENE HUISHI MIAKA MINGI KULIKO WATU WEMBAMBA

     Hatimaye habari nzuri kwa watu wanene, Utafiti uliofanywa na wanasayansi wa Japan kwa watu 50,000 kwa jumla ya miaka 12 umeonyesha kuwa watu wanene wanaishi miaka sita zaidi ya watu wembamba. Wakati watu wanene kila siku wamekuwa wakifanya kila wawezalo ili kupunguza uzito wao, utafiti uliofanywa na timu ya wizara ya afya ya Japan iliyoongozwa na Profesa Shinichi Kuriyama wa chuo kikuu cha Tohoku umeonyesha kuwa watu wanene huishi miaka mingi kulinganisha na watu wembamba.

Utafiti huo ulifanywa kwenye mji wa Miyagi uliopo kaskazini mwa Japan ukiwashirikisha watu 50,000 wenye umri wa miaka kati ya 40 na 79.

Matokeo ya utafiti huo yalionyesha kuwa watu wembamba huishi miaka sita pungufu ya watu wanene.

Utafiti huo uliofanyika kwa jumla ya miaka 12 uliwashirikisha wanawake kwa wanaume wenye umri zaidi ya miaka 40.

Utafiti huo ulifanyika kwa kuangalia vielelezo vya unene na urefu wa mtu (BMI) ambapo kipimo chake kuwa katika mfumo wa kilo kg/m2.

Utafiti huo ulionyesha kuwa watu wenye unene wa wastani (BMI kati ya 18.5 na 25) wenye umri zaidi ya miaka 40 huishi miaka miwili pungufu ya watu wanene kidogo (BMI kati ya 25-30) wakati watu wembamba sana (BMI chini ya 18) huishi miaka sita pungufu ya watu wanene sana (BMI zaidi ya 30).


  1. Sababu iliyochangia watu wembamba kuwa na maisha mafupi kulinganisha na watu wanene ilisemekana kuwa ni kutokana na kwamba watu wengi wembamba hupenda kuvuta sigara na pia kutokana na kwamba watu wembamba miili yao huwa dhaifu katika kupambana na maradhi sugu


Hata hivyo Profesa Kuriyama alishauri watu waendelee kula vizuri na wasibweteke na kujiachia kuwa wanene, badala yake wajitahidi kuwa katika uzito wa wastani unaopendekezwa na mashirika ya afya duniani.

Utafiti huo ulionyesha pia kuwa jinsi mtu anavyozidi kuwa mnene ndivyo gharama za matibabu yake zinavyozidi kuongezeka.

No comments:

Post a Comment