Dec 15, 2011

WANAFUNZI 43 CHUO KIKUU CHA MLIMANI WAFUKUZWA

Chuo kikuu cha Dar es salaam kimewafukuza wanafunzi wapatao 43 kati ya 51 ambao walilkuwa ni vinara katika matukio na vurugu zilizojitokeza hivi karibuni , katika wanafunzi hao wanafunzi tisa wame simamishwa masomo kwa muda wa takribani miez tisa(9).
 Hatua hii imefikiwa mara baada ya wanachuo hao kuvunja baadhi ya vitu na ofisin baadhi za utawala  ,huku wanafunzi hao wakiwazuia baadhi ya maofisa na wafanyakazi wa chuo kuweza kufanya shungul zao za kila siku kkwa kuwahamasisha wafanyakazi hao watoe mustakabali wa taarifa za pesa zao kutoka bodi ya mikopo(heslb) .
Wanafunzi hao waliokuwa wanaendeleza mgomo wao ulioanza Jumatatu wiki hii wakidai taarifa za kwa nini pesa zao zinachelewa wakati bodi ya mikopo, ilishasema wamezileta chuoni hapo. Akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam jana Makamu Mkuu wa Chuo hicho, Profesa Rwekaza Mukandala alisema hatua hiyo imekuja baada ya kuongezeka kwa vitendo vya kihalifu na uvunjifu wa amani chuoni hapo tangu mwanzo wa juma hili.

“Desemba 13 (Jumanne) Kamati ya Wakuu wa Chuo na Shule Kuu zilizoko kampasi kuu ya Mlimani walifanya kikao cha dharura na kufanya mapendekezo kuhusu hatua za kuchukuliwa ili kusitisha uhalifu chuoni,”alisema Mukandala na kuongeza:

“Siku hiyo hiyo Baraza la Chuo nalo lilifanya kikao cha dharura na kutathimi mwelekeo wa chuo na kupitia mapendekezo yaliyoletwa na Kamati ya Wakuu wa chuo na shule kuu na kutoa maamuzi.”. Profesa Mukandala alisema, maamuzi yaliyotolewa na vikao hivyo ni pamoja na kuwafukuza wanafunzi hao 43 na kuchukua hatua za kuongeza ulinzi kwa muda katika maeneo muhimu ya chuo ili wanafunzi walio wengi waendelee kusoma bila kusumbuliwa.

Alisema kati ya wanafunzi hao 43, wanafunzi wanane ni wale ambao walisimamishwa masomo kwa muda wa miezi tisa, lakini waliendelea kuonekana maeneo mbalimbali ya chuo hicho huku wakilazimisha kuonana na uongozi. “Kuna hawa 35 ambao ni kati ya wale wanafunzi 51 waliokuwa na kesi mahakamani nao wamefukuzwa, kati ya hao 51 ilibainika kwamba watatu hawakuwa wanafunzi wa UDSM, hivyo wanafunzi walikuwa 48 tu,” alisema Profesa Mukandala.
hizi baadhi ya matukio yanaohusisha makamu mkuu wa chuo kikuu cha dar es salaam Prof Rwekaza Mukandala na wanafunzi walikokuwa wakiwa wanaendeleza migomo.

No comments:

Post a Comment