Dec 15, 2011

WAVULANA / WANAUME SIKU HIZI HAWAPENDI MWANAMKE TEGEMEZI

Ni wazi kabisa kwa asilimia kubwa ya wanaume sikuhizi hawataki kutegemewa kwa kila kitu kwani maisha yamekuwa magumu wakati mwingine unakuta hata wao wenyewe wanashindwa kujitosheleza hivyo kuwa na mpenzi tegemezi wanaona ni hasara kubwa na kutokana na hilo mwanamume akiona mwanamke pale mwanzo tu baada ya kumtokea mara anaomba vocha, msaada wa kifedha yaani shida zako zote unataka mwanamume akusaidie kiukweli si kitu kizuri ndiyo maana baadhi ya wanaume wakiona tabia kama hizi basi anaanza kukata mawasiliano taratibu mwishowe ukimpigia simu hapokei kabisa .Ni muhimu kujituma ili usiwe ombaomba kila wakati kwani inawezekana mwanamume akakuchoka kutokana na wewe kila wakati kutaka pesa, ijapokuwa wapo baadhi ya wanaume wana huruma na wako tayari kukusaidia kwa lolote ambalo lipo ndani ya uwezo wake hata kama hana uwezo mkubwa kifedha pamoja na hayo usiwe tegemezi fanya kazi kwa bidii ili hata ikitokea na yeye anahitaji msaada wako basi unamsaidia. na hili ni kwa wote mwanamke na mwanamume tushirikiane na si kumuacha mmoja aumie zaidi

No comments:

Post a Comment