Mashindano
ya Fainali ya Kombe la soka kwa Mataifa ya Ulaya, Euro 2012 yanayoanza
mwezi juni mwaka huu yalikua nuru mpya kwa taifa la Ukraine kushamiri
kwenye medani ya kimataifa na pia kuimarisha uchumi wake unaolegalega.
Badala yake iliyokua fursa ya kujikwamua matatizo limekua tatizo.
Katika hatua inayofananishwa na vita baridi, wakuu wa ngazi ya juu kutoka Muungano wa Ulaya wameapa kua watasusia
mechi zote zitakazopangwa Ukraine kwa sababu ya madai kuhusu
kunyanyaswa kwa Waziri Mkuu wa zamani Yulia Tymoshenko gerezani.
Wakosoaji wameonya kua mashabiki wa soka huenda wakashindwa kuhudhuria
mechi kutokana na viwango vikubwa vya bei za kulala hotelini na kwamba
serikali ambayo ina upungufu wa fedha imeiweka nchi hio katika hali
mbovu ya uchumi kwa kutumia dola bilioni 14 kuandaa mashindano haya.
Hi ilikua fursa kwa nchi hii kujiuza na kuonyesha kiwango chake kwa
sababu ya wandishi wa habari watakaokwenda huko kwa ajili ya mashindano,
amesema Oleh Rybachuk, hapo zamani Waziri katika serikali ya kwanza ya
Bi Tymoshenko.
Bw.Oleh ameongezea kusema kua, hivi sasa, wandishi watakuja kuandika juu ya matatizo mengi kupita kiasi.
Nchi ya Ukrainer ilipewa nafasi ya kuandaa mashindano ya Euro 2012 kwa
ushirikiano na Poland mnamo mwaka 2007 katika hatua iliyobainika kama
zawadi kwa nchi hizi mbili hapo zamani za Kikomunisti zinazopenda soka.
No comments:
Post a Comment