
Wajumbe wa Kamati ya Bunge ya Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama wameanza
ziara ya siku mbili Washington DC, kuanzia tarehe 2 – 4 Julai 2012.
Pichani, Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Mambo ya Nje, Ulinzi na
Usalama Mhe. Edward Lowassa (Mb.) akiweka saini kitabu cha wageni mara
baada ya kuwasili kwenye ubalozi wa Tanzania Washington DC.

Kaimu
Balozi wa Tanzania nchini Marekani Mhe. Lilly Munanka akipokea zawadi
kutoka kwa Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Mambo ya Nje, Ulinzi na
Usalama Mhe. Edward Lowassa (Mb.) kwenye ofisi za ubalozi.

Kaimu Balozi wa Tanzania Mhe. Lilly Munanka akiwa kwenye picha ya
pamoja na Wajumbe wa Kamati ya Wajumbe wa Kamati ya Bunge ya Mambo ya
Nje, Ulinzi na Usalama walioanza ziara ya siku mbili Washington DC.
No comments:
Post a Comment