May 17, 2012

LADY JAYDEE MSHAHARA WANGU ULIKUWA TZS 80,000

Ukiwa mtembeleaji mzuri wa twitter kuna mengi kuhusu mastaa utakayoyafahamu. Huko ni sehemu ambayo watu maarufu wanajisikia huru zaidi kuongea masuala yanayowahusu.

Wiki hii Lady Jaydee ameweka wazi mshahara wake aliokuwa anapokea katika kazi yake ya kwanza na ya mwisho katika maisha yake kabla ya kujiingiza kwenye muziki na kuwa mjasiriamali.

“Kazi yangu ya kwanza kuajiriwa mshahara ulikuwa TZS 80,000. Ilidumu kwa miezi kadhaa kazi yangu ya mwisho kabla sijaachana na kuajiriwa," aliandika.
 
Kazi yangu ya kwanza kuajiriwa mshahara ulikuwa TZS 80,000/= ilidumu kwa miezi kadhaa kazi yangu ya mwisho B4 Sijaachana na kuajiriwa, KESHO

Hakusema ni kazi gani lakini kwa mujibu wa historia yake ni kuwa aliwahi kuwa mtangazaji wa radio.

Lady Jaydee kama ilivyo kwa wasanii wengine waliokuwa wafanyakazi kama Profesa J, Ray C na wengine, hakuridhika na kipato alichokuwa anapata na hivyo kuamua kufanya muziki ambao leo hii umempa utajiri mkubwa.

Akiwa anamiliki lounge maarufu sana jijini Dar es Salaam ya Nyumbani ameendelea kujiweka vizuri zaidi kifedha ukiachilia mbali fedha anazopata kutokana na muziki.

Kwa wengine mafanikio yake yanawapa wasiwasi ambao kwetu sisi tunaona hauna maana. Katika kutafuta habari zake kwenye mtandao, tumekutana na swali lililokuwa limeulizwa na mtu asiyejulikana katika mtandao wa wiki.answers.com linalouliza “Is Judith wambura member of freemason?

Jibu lililotolewa kwenye mtandao huo ni “Freemasons do not, generally, advertise the fact they are Freemasons. No public statement can be found by Judith Wambura admitting membership. Therefore any statements made as to membership are speculation.”



Si yeye tu anayehisiwa hivyo kwani tayari Diamond na marehemu Stephen Kanumba wamewahi kuhusishwa na habari hiyo.

No comments:

Post a Comment