May 2, 2012

LIPUMBA ATATAJWA KWENYE BARAZA LA MAWAZIRI

Bwana LIPUMBA ambaye ni mwenyekiti wa chama cha wanachi(CUF), inasemekana kutakuwepo na uwezekano mkubwa wa kutajwa baraza jipya la mawaziri. kwa mtazamo wangu mdogo hili nalichukulia kama ni RUMOR ambazo zinaendelea kuelewa katika sehemu mbalimbali ya mitandao ya kijamii na hat abaadhi ya watu huku mtaani kwetu wameanza kulizungumzia jambo hili kwa namna nyingine kabisa.
 Kwa habari zinazoelezwa na wananchi  zinasema kwamba kama ikatokea makubariano yoyote baina ya chama cha mapinduzi(CCM) na chama cha wananchi(CUF)  itamlazimisha MH rais JAKAYA KIKWETE  kumpa waziri MH LIPUMBA katika nafasi ya WAZIRI WA FEDHA NA UCHUMI.
 JE SIASA ZETU ZINARUHUSU? 
 
 KWA KUREJEA KATIBA YA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA INASEMA HIVI:
              Ibara ya 68 ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya Mwaka 1977 imetamka kwamba Kila Mbunge atatakiwa kuapishwa katika Bunge kiapo cha uaminifu kabla hajaanza kushiriki katika shughuli za Bunge; lakini Mbunge aweza kushiriki katika uchaguzi wa Spika hata kabla hajaapishwa. Hivyo iiwapo mbunge atateuliwa au kuchaguliwa atapaswa kuapa katika Bunge. Ibara ya 56 ya katiba inasema Waziri au Naibu Waziri hatashika madaraka yake ila mpaka awe ameapa kwanza mbele ya Rais kiapo cha uaminifu na pia kiapo kingine chochote kinachohusika na utendaji wa kazi yake kitakachowekwa kwa mujibu wa sheria iliyotungwa na Bunge.Ibara ya 55(4) inasema Mawaziri na Naibu Mawaziri wote watateuliwa kutoka miongoni mwa Wabunge.

Kwa mujibu wa vifungu vilivyoainshwa hapo juu ni kwamba ili mtu aweze kuteuliwa kuwa Waziri au naibu waziri ni lazima awe mbunge, na mbunge hatashika madaraka yake mpaka awe ameapa kwa Spika katika Bunge. Pia waziri au naibu waziri mteule hatashirika madaraka mpaka awe ameapa kwa raisi.


Kama ikitokea Mh. Rais akatumia mamlaka aliyonayo kwa mujibu wa ibara ya 66(1) (e) ya Katiba kuteua mtu yoyoyte kuwa mbunge kwa nia ya kumteua kuwa waziri basi mtu huyo atalazimika kuapa kwa spika mbele ya bungu. Na kama hili likitokea tutegemee bunge la dharura kuitishwa kwa ajili ya kumwapisha mbunge.


Baada ya maelezo hayo haitawezeakana mtu kukaimu madaraka ya uwaziri au mbunge akisubiri kuapishwa.
 

No comments:

Post a Comment