May 2, 2012

YALIYOJIRI FACEBOOK &TWITTER

Sakata la Mtibwa Sugar kutakiwa na baadhi ya wadau wa soka ishushwe daraja kikanuni imenipa jibu kwamba kumbe kweli Sheria ipo kwa matumizi sahihi ya wanasheria tu. Eti kanuni inaposema mwamuzi anapaswa asubiri kwa muda USIOZIDI dakika 15 kabla hajavunja pambano, laymen wanatafsiri kwamba anaweza kufanya hivyo hata ndani ya sekunde 30 kwa sababu HAIZIDI dakika 15! Ridiculous. Hii ni Plain meaning rule lakini ukitazama "intention of the rule-maker" utabaini kwamba alichomaanisha ni kwamba IKITIMIA DAKIKA YA 15 ASISUBIRI ZAIDI BALI AVUNJE PAMBANO HAPO HAPO bila kuongeza sekunde kadhaa. Kama tafsiri ya ki-layman ni sahihi, dakika 15 zimetajiwa nini kwenye kanuni hiyo wakati dakiki ziko kuanzia moja to the infinity? Tafsiri ya ki-layman ingekuwa sahihi kama kanuni ingesema "...dakika yoyote baada ya tukio la vurugu". Yule refa wa Azam vs Mtibwa alikosea kuvunja pambano mapema na mechi hiyo ilistahili kurudiwa. Laymen msipindishe ukweli kwa tafsiri zenu za ki-layman.
 

No comments:

Post a Comment