May 24, 2012

PICHA NA MATUKIO YOTE KATIKA KESI YA MBUGE WA UBUNGO, JOHN MNYIKA

Mahakama Kuu ya Tanzania kanda ya Dar es Salaam, imemthibitisha John Mnyika kuwa ndiye Mbunge halali wa Jimbo la Ubungo, Dar es Salaam kwa tiketi ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo, CHADEMA.


Hakimu Pendo Msuya aliyeisoma hukumu hiyo alitupilia mbali madai yote matano yaliyowasilishwa katika keshi hiyo kwa kuwa upande wa mlalamikaji ulishindwa kuwasilisha ushahidi usio na mashaka kuhusu madai husika.


Kesi hiyo yenye namba 107 ilifunguliwa mwaka juzi na aliyekuwa mgombea kiti hicho kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi, CCM, Hawa Ng’humbi dhidi ya John Mnyika kupinga ushindi alioupata baada ya Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2010.




Madai hayo yalikuwa ni pamoja na:
  1. Mlalamikiwa kumtuhumu mlalamikaji kuhusika na kashifa za uuzwaji wa jengo la Umoja wa Wanawake (UWT)
  2. Kubadilishwa kimakosa kwa kura katika fomu za matokeo ya Ubunge
  3. Kuwepo kimakosa kwa watu katika chumba cha kuhesabia kura
  4. Matumizi ya tarakilishi ya mlalamikiwa wakati wa kujumlisha kura
  5. Ukiukwaji wa taratibu za kisheria katika uchaguzi ambazo zilisababisha kuwepo kura hewa 14,854

Baada ya hukumu kutolewa, wanahabari walimwuliza Ng’humbi ikiwa atakata rufaa ama la, ambapo alijibu kuwa bado hajaamua.








Naye Mwenyekiti wa CHADEMA, Freeman Mbowe, akitoa maoni yake mara baada ya hukumu hiyo kusomwa amesema, Mahakama imetenda haki lakini akawataka watu wote wanaopeleka kesi mahakamani kuhakikisha wanakuwa na ushahidi wa kuthibitisha madai hayo ili kuepusha kupoteza muda na gharama kubwa inayotumika katika kesi.

CHADEMA imepanga kufanya mkutano mkubwa wa hadhara siku ya Jumapili jijini Dar es Salaam. 

No comments:

Post a Comment