May 2, 2012

Tanzania tunaweza sana muziki, tatizo ni idadi ndogo ya wasanii wanaozungumza lugha ya kiingereza kwa ufasaha - Def Xtro


Def Xtro
Usaili wa Tusker Project Fame msimu wa tano umeanza. Safari hii TPF5 iliamua kwenda pia Arusha kuangalia vipaji vilivyoko huko.  Katika panel ya majaji waliohusika katika kuchuja vipaji vya Arusha alikuwepo jaji mkuu maarufu katika mashindano hayo Ian Mbugua.

Mwingine aliyepata shavu la kuwa jaji na kuwakilisha Arusha alikuwa ni Henry Minja maarufu kama Def Xtro, mtayarishaji wa muziki na mmiliki wa studio ya Noizmekah Productions ya Arusha. Katika interview hii mahsusi na Leotainment, DX anaeleza mambo yalivyokuwa.

Leotainment: Ilikuaje ukawa judge? I mean jamaa walikujuaje? and ilikuwa siku moja tu ama?

Def Xtro: Mpaka kuwa judge wa TPF5 auditions ni recommendation ya HERMY B wa B-Hitz. Aliniunganisha kwa project manager wa TPF5,kisha nikaelekezwa kutuma details zangu kuhusu music experience ili watathmini kama ni sawa kuketi kama mwamuzi katika usaili wa Arusha zone.


Leotainment: Ilikuwa mara yako ya kwanza kuwa jaji kwenye mashindano ya kuimba?

Def Xtro: Hii ni mara yangu ya pili kuwa judge wa music contest. Mara ya kwanza ikiwa ni katika "Serengeti Fiesta Freestyle" ya arusha zone iliyofanyika "Mawingu Club Arusha,nikisaidiana na judge mwenzangu FidQ" akapatikana mshindi "Tash Tashnificent wa chapia" na second runner up "VeeJay wa Kimziki Zaidi"
Leotainment: Ilikuaje  katika msimu huu TPF waliamua kuja Arusha kutafuta vipaji pia?
Def Xtro: Arusha pameonekana kupata mkono wa baraka mwaka huu kwa shindano kubwa kama TPF season ya tano kuamua kuipa nafasi Arachuga kuwakilisha Tanzania kule katika Academy,mbali na season zote nne zilizopita kufanya zoezi la usaili Dar-es-Salaam pekee. Arusha tunastahili kujipongeza kwa kutambulika na kuweza kupata washiriki wanne bora kati ya wale ishirini na wanne waliojiandikisha.
Leotainment: Were there enough and convincing talents?

Def Xtro: Convincing talents wanne walijipatia nafasi ya kuendelea na mchujo wa academy kule nairobi ambapo watatakiwa kuripoti mwezi huu wa May tarehe 18. Kwa kweli talents hazikutosha. Kwa attendance na signup iliyofanyika tarehe 28 na 29 April,walipatikana watu wachache mno,tofauti na ukubwa wa jiji na wingi wa vipaji.

Setback mojawapo ikiwa ni kuchelewa kutangazwa kwa usaili huo kwa Arusha na pia vyombo vya habari havikupewa taarifa mapema hivyo washiriki wachache kujitokeza. 
Leotainment: Production crew ya TPF ikoje ukilinganisha na auditions kama za BSS hivi?

Def Xtro: Production crew kwa tathmini niliyofanya naweza kusema hawajatofautiana na ya BSS,equipment setup, filming lighting na scripts ni kama BSS.

TPF ni shindano linaloandaliwa na East African Breweries na nchi tano zinapeleka washiriki katika academy kuwania shillingi milioni tano za Kenya. 

Nafikiri tofauti kubwa ipo katika washiriki wanaolengwa na BSS na wale wanaolengwa na TPF,kwa maana kuwa TPF,ticketi kuu ni ufanisi wa mshiriki kuimba VIZURI kwa lugha ya kiingereza mbali na wimbo atakaoimba wa kiswahili.
Leotainment: How did u get along with Ian Mbugua?

Ian na Def Xtro
Def Xtro: Ian alikuwa na ushirikiano mkubwa na sisi majaji wenyeji,very friendly. Waliomtazama katika season zote zilizopita wana tafsiri moja ambayo hata mimi nilikuwa nayo,kwamba huyu jamaa ni mgumu kukubali kuwa mshiriki anastahili nafasi hivyo hata kumwita "Jaji Mnoko". Lakini baada ya project manager kutubrief sisi majaji wenzake kuhusu wanachokihitaji Arusha,basi nikaelewa kwanini Ian ni strict katika uamuzi wake.
Leotainment: Umejifunza nini kutokana na kupata nafasi ya kuwa jaji wa Tusker Project Fame 5 usaili wa Arusha?

Def Xtro: Nimejifunza kwamba Tanzania tunaweza sana muziki. Changamoto kubwa inayotukabili ni tabaka la idadi ya wasanii wanaozungumza lugha ya kiingereza kwa ufasaha.

Kenya wana idadi ndogo ya Music Artists lakini wenye mafanikio na mikataba mikubwa na makampuni tofauti na Tanzania ambapo wasanii wetu ni wengi sana na wengi wao hawana mikataba wala endorsements za kufanya wajiendeleze kimaisha.

Tofauti inakuja kuwa Kenyan artists wapo wachache na wote wanamaintain status kwa miaka nenda rudi because ufanisi wao wa mawasiliano kwa kiingereza unageuka "ticket" ya kufanya ziara nyingi zaidi nje ya nyumbani kuliko ndani hivyo kubaki RELEVANT over TIME!
                           
                                   NA DAILY ENTERTAINMENT TAKE AWAY

No comments:

Post a Comment