Jul 23, 2012

picha na matukio yote uwanja wa taifa leo bila kusahau YANGA NA APR NUSU FAINALI

YANGA imefuzu kuingia Nusu Fainali ya Klabu Bingwa ya soka Afrika Mashariki na Kati, Kombe la Kagame, baada ya kuifunga Mafunzo ya Zanzibar kwa penalti 5-4, kufuatia sare bya 1-1 ndani ya dakika 90 Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam, wawakilishi wa Zanzibar Mafunzo walikuwa wa kwanza kupata bao lililofungwa na Ali Othman Mmanga, dakika ya 34, akiunganisha kona ya Juma Othman Mmanga na Yangab wakasawazisha dakika ya 46, mfungaji Said  Bahanuzi ‘Spider Man’.
Yanga sasa itamenyana na APR ya Rwanda, keshokutwa ambayo katika Robo Fainali ya kwanza, imeitoa URA ya Uganda kwa kuifunga 2-1, mabao yake yakifungwa na Jean Claude Iranzi dakika ya tisa na Suleiman Ndikumana dakika ya 34, wakati la Watoza Ushuru wa Kampala, lilifungwa na Robert Ssentongo dakika ya 57.
yafuatayo ni baadhi ya matukio yaliyojitokeza leo uwanjani 
Jerry Tegete kulia na Haruna Niyonzima kushoto wakimpongeza Chuji- nyuma nyuma ni Bahanuzi 'Spider Man'


Benchi Yanga likiomba dua wakati Chuji anakwenda kupiga penalti ya mwisho

Said Bahanuzi 'Spider Man''

Mmanga akiwa kwenye machela baada ya kupoteza fahamu

Hapa ni mara tu baada ya kuanguka akisaidiwa kwa kupepewa na wenzake
picha na matukio yote yamechukuliwa bongostaz.blogspot.com

No comments:

Post a Comment