Jul 19, 2012

PICHA 45 NA TUKIO ZIMA LA AJALI, ZANZIBAR

PICHA NA TUKIO ZIMA MPAKA SASA HALI ILIVYO ZANZIBAR





Waziri wa Nchi Afisi ya Rais na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk Mwinyihaji Makame akitoa taarifa kwa Waandishi wa Habari kuhusiana na kuzama kwa Meli ya Star Gate hukokatika bahari ya Chumbe Zanzibar na ikiwa na abiria 250.


Wananchi mbalimbali wakishuhudia tukio la kuokolewa watu waliozama na meli ya Star Gate huko katika hukokatika bahari ya Chumbe Zanzibar na ikiwa na abiria 250.


Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Idi akiwa katika Eneo la Bandari akishuhudia kuletwa kwa majeruhi mbalimbali waliookolewa katika meli ya Star Gate iliozama huko katika bahari ya Chumbe Zanzibar na ikiwa na abiria 250.


Spika wa Baraza la Wawakilishi Pandu Amer Kificho pamoja na mawaziri mbalimbali wakiwa katika Eneo la Bandari wakishuhudia kuletwa kwa majeruhi mbalimbali waliookolewa katika meli ya Star Gate iliozama huko katika bahari ya Chumbe Zanzibar na ikiwa na abiria 250


Majeruhi alieokolewa katika meli ya Star Gate iliozama huko katika bahari ya Chumbe Zanzibar na ikiwa na abiria 250.


Majeruhi wakipatiwa Mablanketi kwa ajili ya kujihifadhi baada ya kuokolewa katika meli ya Star Gate iliozama huko katika bahari ya Chumbe Zanzibar na ikiwa na abiria 250.
rais wa zanzibar dkt alli mohammed shein wa pili toka kulia akiwa bandarini zanzibar














meli ikiwa U.S.A








Hizi ndizo Meli za Mv Skagit ambazo kwa mara ya kwanza tuliripoti kwenye blog hii (chiwileinc) ununuzi wake tarehe 19/02/2011 na hapa chini ndiyo maelezo yake,
Vifaa vilivyonunuliwa kutoka Marekani - Washington State na moja ya kampuni za usafiri kwa Dola laki nne kwa zote mbili ambapo vitakapowasili vitatoa huduma za usafiri kati ya Zanzibar na Dar.
Boti hizi zilitengenezwa mwaka 1989 na kila moja ina uwezo wa kubeba abiria 250 ziliwahi kuwekwa kwenye mtandao wa E bay kwa bei ya Dola laki tatu kila moja lakini hazikupata wateja. Zilipotengenezwa mwaka 1989 ziligharimu Dola milioni tano.

Sijui zitakapowasili zitapewa majina gani.




The state finally has sold two of its discarded passenger-only ferries, the Kalama and the Skagit, to the African nation Tanzania.
The ferries have been docked and inactive since September 2009. The Legislature ordered the state to get out of the passenger-only ferry business in '06.
The two ferries had been sold to a boat broker in Port Coquitlam, B.C., which sold them to Tanzania. They will be put in service between the mainland of Tanzania and the Zanzibar archipelago. They were sold for $400,000 combined, far below the $900,000 value the state said they were worth in December 2009.
Marta Coursey, spokeswoman for Washington State Ferries, said the two boats will be taken to Africa by cargo ship.
The state had hoped to sell the two 112-foot boats locally, but when that failed, it placed them for auction on eBay, asking $300,000 each, with no success. The ferries were built in New Orleans and purchased in 1989 for $5 million.
meli ikiwa tanzania


.


Ferry historian Steve Pickens said the Kalama and the Skagit were the first two passenger-only boats the state built. They were supposed to go into service in 1989 but were tied up because there was no money to run them. Following the Loma Prieta earthquake of 1989, the two vessels were sent to San Francisco and served commuters crossing the bay while the city's bridges were r 
        
         Taarifa ya Serikali - Kuzama kwa Meli Zanzibar MAAFA YA KUZAMA KWA MELI ZANZIBAR
Meli ya Mv. Star Gate imezama karibu na Kisiwa cha Chumbe ambapo watu 12 wamefariki hadi muda huu na wengine kadhaa wamejeruhiwa.
Akitoa taarifa fupi kwa waandishi wa habari,Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi,Dk. Mwinyihaji Makame Mwadini alisema taarifa za kuzama kwa meli hiyo ilitolewa na Boti iendayo kasi ya Kilimanjaro III iliyokuwa ikitokea Dar es Salaam kwenda Zanzibar ndipo ilipoiona meli hiyo ikizama.
“Tulipata taarifa kutoka Boti ya abiria ya Kilimanjaro III saa 7:50 mchana waliporipoti kuona meli ikizama karibu na Kisiwa cha Chumbe” Alisema Waziri Mwinyihaji.
Waziri huyo alisema Meli hiyo imezama maili sita kuelekea Kisiwa cha Yasin Kusini mwa Kisiwa cha Chumbe kilichopo Unguja maili kadhaa kutoka Bandari ya Malindi.

           Waziri Mwinyihaji alisema idadi ya abiria walikuwa 250 ambao ni watu wazima, watoto 31 na mabaharia 6. “Tumepeleka waokoaji, kuna boti tano zipo eneo la tukio kushirikiana na waokoaji wengine” Alisema Waziri Mwinyihaji.
Alisema maiti zote zitapelekwa viwanja vya Maisara Zanzibar kwa ajili ya ndugu na jamaa kuzitambua maiti za ndugu zao ambapo majeruhiwa wote watatibiwa Hospitali Kuu ya Mnazi Mmoja.
                Katika Bandari ya Malindi mwandishi wetu ameshuhudia maiti kadhaa zikiwemo za watoto zikishushwa, Miongoni mwa abiria waliookolewa ni raia 13 wa Mataifa mbalimbali ya nje huku raia mmoja ambaye hakuweza kutambuliwa utaifa wake  amepoteza maisha.
                      Makamu wa Pili wa Rais Zanzibar, Balozi Seif Ali Idd alifika eneo la Bandari ya Malindi Zanzibar pamoja viongozi wengine akiwemo Spika wa Baraza la Wawakilishi, Pandu Ameir Kificho, Mawaziri na  baadhi ya Wajumbe a Baraza la Wawakilishi walikuwepo kutoa msaada  unaohitajika.
               Katika eneo la pembezoni mwa bandari ya Malindi, makundi ya wananchi yalikuwa yamekusanyika wakisubiri taarifa za tukio hilo tangu saa 8:30 mchana.
Vikosi vya ulinzi na usalama, msalaba mwekundu na watoaji wengine wa misaada ya dharura walifika kwa haraka eneo la tukio.
Hadi sasa kazi ya uokoaji inaendelea karibu na Kisiwa cha Yasin ilikozama meli hiyo.
    Meli ya Mv. Star Gate inamilikiwa na kampuni ya kizalendo ya Sea Gull Sea Transport Ltd ambayo mwaka 2009 Meli yake nyengine ya Mv. Fatih ilipinduka na kuzama katika Bandari ya Malindi Zanzibar na kua watu sita.
        Mwaka jana Zanzibar ilikumbwa na maafa baada ya Meli ya Mv. Spice Islanders kuzama katika bahari ya Hindi eneo la Nungwi katika Kisiwa cha Unguja ikielekea Kisiwani Pemba ambapo taarifa rasmi ya Serikali ilisema watu 197 walipoteza maisha na wengine wengi kujeruhiwa.
Taarifa zaidi zitatolewa hapo baadea.
Imetolewa na:
Idara ya Habari(MAELEZO) Zanzíbar
Julia 18,2012
Zanzíbar,Tanzania

 Mmoja wa Majeruhi akipata huduma ya Kwanza baada ya kuokolewa akiwa katika bandari ya malindi
 Daktari akitowa huduma ya kwanza kwa mmoja wa majeruhi wa boti iliozama ikiktokea Dar-es-Salaam kuelekea Zanzibar






 Majeruhi wa ajali ya Meli wakiwa katika Hospitali ya Mnazi Mmoja wakipata huduma baada ya kuokolewa.
 Majeruhi wakiwa katika hospitali ya Mnazi Mmoja


Mwokoaji akiwa na mmoja wa maiti wa ajali hiyo
 Waokoaji wakiokoa moja ya maiti. wakiwa katika boti ya Kilimanjaro. 
  Majeruhi wakiwa katika mgongo wa boti hiyo wakisubiri kuokolewa.
 Baadhi ya Abiria wakiwa katika moja ya chombo cha kuokolea wakielea baharini wakisubiri kuokolewa.
 Boti ya KMKM ikiwa katika zoezi la kuokowa majeruhi. 
 Helikopta ya Jeshi la Polisi ikiwa eneo la tukio.
 Boti iliozama ni kama hii ni ni pacha wake.
 Boti ya Fly ikiondoka katika bandari ya Zanzibar kueleke kutowa msada w uokoaji.


 Waziri wa Mawasiliano na Miundombinu Hamad Masoud akiwa katika boti ya Kilimanjaro akiwa sehemu ya Tukio ilipozama boti hiyo maeneo ya Chumbe.
 Tagi la Shirika la Bandari likiwa katika sehemu ya tukio.






 

 imeandaliwa na chiwileinc.blogspot.com


No comments:

Post a Comment