Jun 28, 2012

PAMBANO LA DRAKE & CHRIS BROWN NI $1 MILLION KWA KILA MTU

110495-chris_brown_drake_potw_617_409 



  Kufatia mgomvi uliojitokeza kati ya Drake na Chris Brown katika ukumbi wa W.I.P NIGHT CLUB, hatimaye pambano limetanganzwa endapo wawili hao wataridhika kuingia ukumbini na kuzichapa LIVE
      , a celebrity boxing promoter has offered each artist $1 million to get in the ring together.
CNN reports that the promoter, Damon Feldman, says he has financial backing from Alki David and he also says that he’ll donate $1 million to a charity for abused women if the fight goes down.
       Feldman says the fight would feature three-minute rounds, with the participants wearing over-sized gloves and protective head gear.
Feldman is the same promoter who has put on fights involving ex-baseball outfielder Jose Canseco, Lindsay Lohan’s dad Michael and Rodney King.
         The promoter has yet to receive a response from either parties, but he’s also asking Rihanna to be a ring girl for the fight, although he knows the chances of that are unlikely.

RIHANNA CENTRAL LONDON SWEAT SESSION


                                                                                                      
    Taking a break from her television production efforts to keep up on her physical fitness, Rihanna paid a visit to Fitness First gym in Central London on Thursday evening (June 28).
Clad in a black Adidas tracksuit and black Brooklyn hat with sunglasses and a gold chain, the 24-year-old singer signed autographs as she exited her hotel before making the short trip to the nearby gym.
              The sweat session follows quite the ambitious previous night for RiRi, as she worked with Girls Aloud star Nicola Roberts and fashion designer Henry Holland until the wee hours of the morning on her still unnamed Sky Living fashion show.
Tweeting about the endeavors once wrapped up, the "We Found Love" singer tweeted, "To my friends at Sky Living, thank you for working with me all the way til 5am this morning! I’m happy to be a part of the fam, WELL DONE!!"


      SOME PICTURE:                       











                                                 
 

HAWA NDO WAPENZI WALIOWAHI KUWA RIHANNA



Hawa ndio waliokuwa na mahusiano ya kimapenzi na Rihanna ,Ndio maana anajita Bad girl, Rude girl Rih Rih .

Chris Brown ,Dudley O'Shaughnessy , Ashton Kutcher ,Drake , Matt Kemp ,Meek Mill

Huu alikuwa na Rihanna zamani lakini hakutangaza mahusiano yao anaitwa Shia Lebeouf ni star wa filamu marekani

  

PICHA ZA NYUMBA YA PETER &PAUL aka P SQUARE (THE SQUARE VILLA)




         Wakiwa Na Boss Wao Akon Wa Convict Music .
Kwa Njee Crib Yao Ilivyo
Swimming Pool Sasa
Swimming Pool Inavyo Onekana Kwa Juu





Guest Room


To The Bed Room
 Hard Work Pays

Na Hii Ndio Private Jet Yao Aka Ndege Yao Binafsi

Ndege Ilivyo Njee



Ilivyo Ndani

      


NA;sammisago

Jun 13, 2012

KWANINI BEYONCE ALIMPA MWANAE JINA LA BLUE IVY?


       Tangu ijulikane kuwa BeyoncĂ© na Jay-Z wamemuita mtoto wao wa kwanza Blue Ivy watu wamekuwa wakijaribu kutafuta maana halisi ya jina la binti yao. Kuna wale waliofikiri kuwa limetokana na mapenzi ya Jay-Z kwa rangi ya Blue, lakini Bey ameandika shairi ambalo huenda likawa na sababu halisi ya kwanini waliamua kumuita binti yao Blue.
                    “Dunia ni ya blue katika ncha na kina chake. Blue hii ni rangi iliyopotea. Mwanga katika kikomo cha mkusanyiko wa rangi hausafiri umbali wote kutoka kwenye jua kuja kwetu. Hupotea miongoni mwa ‘molecules’ za hewa na kusambaa kwenye maji. Maji hayana rangi, maji ya juu huonekana kuwa na rangi ya chochote kilichopo juu yake, lakini maji ya kina huchukua rangi zote zilizosambaa, maji yakiwa halisi zaidi ndivyo huwa na rangi ya blue zaidi.”
         Ujumbe huo kutoka kwenye kitabu cha mwandishi Rebecca Solnit kiitwacho ‘Field Guide to Getting Lost’ uliandikwa na BeyoncĂ© kwenye blog yake ya mtandao wa Tumblr jana.
Kabla ya Beyonce kujifungua watu walijaribu kubashiri jina la mtoto wao ambapo watu walidhani angeitwa Brooklyn (kutokana na mstari maarufu wa Jay-Z “If we had a daughter, guess what I’m a call her? Brooklyn Carter), Sasha, Babyonce n.k.
                  Baada ya kujulikana kwa jina alilopewa mtoto wao kuna watu wakalihusianisha jina Blue Ivy na “Eulb Yvi”, wakidai kuwa lilikuwa jina la Latin la binti wa Lucifer (shetani) na mjadala ukaibuka kwenye mtandao wa Twitter.
                  Mtandao wa The Examiner ukapuuzia dhana hiyo kwa kusema Biblia haijataja kama Lucifer ana mtoto wa kike na hakuna jina Eulb Yvi kwenye kamusi ya kilatin. (Fun fact: Unajua kuwa ni marufuku kumuita mtoto wako Lucifer nchini New Zealand?)
Kulikuwepo pia na mitazamo ya maana kuhusiana na uchaguzi wa jina hilo. Good Morning America walidai kuwa Ivy ni utani wa numerali IV ya Roma. Namba nne ni muhimu kwa wanandoa hao – walifunga ndoa April 4, (4/4), siku zao za kuzaliwa ni tarahe 4 (September na December), na albam ya nne ya Beyonce ilipewa jina la “4.” (Huffington Post).






Na:bongo5

Jun 11, 2012

NEW SONG ''LET YOU GO'' FROM ELIUD KAWALA aka EKA FROM UNIVERSITY OF DODOMA

MSANII ambaye mwenye upenzi mkubwa na muziki ELIUD KAWALA aka EKA .hatimaye ameroki nyimbo yake mpya inaokwenda kwa jina LET YOU GO.
EKA alikonga sana mioyo kwa wakazi wa BUKOBA wakati akisoma shule ya sekondari IHUNGO HIGH SCHOOL ambapo alitumia kipaji chake vizuri kuendeleza mziki wa kizazi kipya.
 EKA kutokana na haili yake ya kujituma katika tasnia ya mziki wa kizazi kipya alichaguliwa kuwa kiongozi wa michezo na burudani hali hiyo iliongongeza hamasa miongon wa wanafunzi wa shule ya IHUNGO HIGH SCHOOL
 EKA ameachia kibao chake LET YOU GO huku akiomba wananchi, wapenzi na wadau wote wa mziki wa bongo fleva wampe support ya kutosha.


 

 
Singer: Eliud kawala a.k.a EKA
Song: Let you go
 Producer: Patrino
Studio: B1 record dodoma
Mixing: KID

This is ma first track for ma fans and am on ma way to give you the best of music you deserve. I count on your support as am preparing my first album titled "MOYO". This song will be accompanied with a video that will be released soon the next month. Music for life. You can send me your comments through my facebook account "Eliud Kawala" and ma mobile phone number 0759385936 or follow me on twitter @eka

tunaomba radhi kwa kushindwa kuipata nyimbo kwa wakati unaweza kutembele hulk share/EKA>LET YOU GO
SORRY

PICHA:RAIS JAKAYA KIWETE AONGOZA WAOMBOLEZAJI VIWANJA VYA KARIMJEE



Rais Jakaya Kikwete akiwa na Makamu wa Rais wa pili kutoka kushoto na Mwenyekiti wa CHADEMA Freeman Mbowe wa mwisho kushoto wakiongoza waombolezaji  kwenye viwanja vya Karimjee wakati Mwili wa muasisi wa chama cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA Mzee Bob Makani ulipoagwa leo jijini Dar es salaam
Mwili wa Marehemu Bob Makani ukiwa umewekwa eneo maalum tayari kwa kuaga mwili huo leo kwenye viwanja vya Karimjee.
Mwili wa Marehemu Bob Makani ukiteremshwa kwenyegari ili kuwekwa eneo hilo kwa ajili ya waombolezaji kutoa heshima zao za mwisho.

PICHA: TUKIO ZIMA LA KESI YA LULU ILIVYOKUWA LEO MAHAKAMANI

Mtuhumiwa wa kesi ya mauaji ya aliyekuwa msanii maarufu wa filamu za Bongo Steve Kanumba, Elizabeth Michael ‘Lulu’ akisindikizwa na askari magereza kutoka katika jengo la mahakama Kuu kwenda mahakama kuu ya biashara.
‘Lulu’ akiwa ndani ya mahakama.
‘Lulu akiteta jambo na wakili wake muda mfupi baada ya kufika mahakamani.
Akitoka mahakamani baada ya kesi yake kusogezwa hadi tarehe 25 mwezi huu, ambapo watetezi wa ‘Lulu’ wametakiwa kuwasilisha vielelezo vyenye uthibitisho wa umri wake ifikapo tarehe 13 mwezi huu, wakati upande wa serikali wameomba kuwasilisha vielelezo vyao tarehe 22 mwezi huu ili kumaliza tatizo la utata kuhusu umri wa mtuhumiwa huyo.
‘Full Ulinzi ndani ya mahakama’ wakati kesi ya ‘Lulu’ ikisikilizwa.
Elizabeth Michael ‘Lulu’ akipanda basi la magereza baada ya kesi yake.
Ulinzi ulikuwa ni wa uhakika eneo lote nda na nje ya mahakama kuu wakati wa kesi hiyo.

Imetayarishwana  http://dewjiblog.com
 

Jun 8, 2012

WACHEZAJI WENYE ASILI YA AFRIKA WATAKAOCHEZA EURO


Viwanja vya mashindano
Viwanja vya mashindano
Mashindano ya kombe la Mataifa ya Ulaya, yajulikanayo kama Euro 2012 yameanza jana nchini Poland na Ukraine. Mashindano haya ni kivutio kwa wachezaji nyota wanaoshiriki Ligi bora za soka Duniani. Jambo la kushngaza ni kwamba kuna baadhi ya wachezaji wenye asili ya Afrika wanaoziwakilisha nchi walizoamua kua nchi zao.
Mamilioni ya mashabiki kutoka kote barani Afrika kuanzia jana walitazamiwa kuganda kwenye viti macho kwenye runinga na masikio kwenye Rediyo kufuatilia jazba la Euro 2012.
Ingawa mashindano haya ni ya Mataifa ya Ulaya, wanashiriki wachezaji wa Afrika pia. Inakuaje Wachezaji wa Kiafrika kushiriki Kombe la Mataifa ya Ulaya?
Sababu ni kwamba baadhi ya wachezaji walizaliwa barani Afrika lakini wameamua kuyachezea Mataifa ya Ulaya ambako wanaishi na kuyageuza kua nyumbani au wazazi walizaliwa Afrika na kuhamia Ulaya lakini wakaamua kuyacfhezea Mataifa waliochagua kua nyumbani kwao.
Wachezaji hawa wangeweza kuzichezea nchi walikotoka lau kama wangependa.
Ufaransa ina kikosi cha Waafrika wengi
Ufaransa ina kikosi cha Waafrika wengi
Ufaransa ndio nchi yenye wachezaji wengi wenye asili ya Kiafrika kwenye mashindano haya ya Euro ikiwa na jumla ya wachezaji tisa.
Miongoni mwao ni kipa Steve Mandanda ambaye asili yake ni Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo, Beki wa Manchester, Patrice Evra kutoka Senegal, Mchezaji wa klabu Manchester City, Samir Nasir kutoka Algeria na mshambuliaji wa Real Madrid Karim Benzema, pia kutoka Algeria.
Ghana ina wachezaji watatu wanaoshiriki Euro 2012.
Wachezaji ambao wangeweza kuichezea Timu ya Black Stars ni mshambuliaji Mario Ballotelli, Beki wa Ujerumani Jerome Boateng pamoja na mshambuliaji wa England, Danny Welbeck anayechezea klabu ya Manchester United.
Mzaliwa wa Tunisia akicheza kiungo Sami Khedira,anayechezea klabu ya Real Madrid ataiwakilisha Ujerumani. Luis Nani wa klabu ya Manchester United alizaliwa kwenye visiwa vya Cape Verde, ataiwakilisha Ureno.
Angelo Ogbonna ambaye wazazi wake ni kutoka Nigeria ataiwakilisha Italia.
Kwa ujumla kuna wachezaji wengi wenye asili ya Afrika kwenye mashindano ya Euro 2012 kutimiza Timu nzima ya wachezaji 11 na meza ya wachezaji wa akiba.
Hivyo, hasara ya Afrika ni ufanisi kwa Ulaya! Suali linalozuka hapa ni Je hawa wachezaji wenye asili ya Kiafrika wangeweza kufikia kiwango gani kama wangeziwailisha nchi moja ya Kiafrika kwenye mashindano haya ya Euro.

Jun 6, 2012

BINTI MREMBO AKUBALI KUFANYA MAPENZI NA NYANI

   Kama utani alichukuliwa club na Ahaji kwe lengo kuwa wanakwenda kuspend mda wao pamoja na kupeana raha lakini walipofika hotelini ghafla hali ya mambo iligeuka ambayo ilipelekea kifo cha binti huyu mrembo. Alifahamika kwa jina la Cynthia wa huko nchini Marekani ambapo baada ya kufika ndani ya chumba cha bwana huyo alitamkiwa kuwa atapewa dola za Kimarekani 2000 pindi atakapokubali kufanya mapenzi na nyani wa bwana huyu.
      Mwanzoni binti huyo alikataa lakini kwa tamaa ya hela na vishawishi vya bwana huyo hatimaye alikuba kufanya mapenzi na mnyama huyo lakini mda mfupi baadae baada ya tukio hilo binti alianza kuumwa na tumbo na kisha kutokwa na uchafu sehemu zake za siri,rafiki yake alimkibiza hospitalini lakini alifariki kabla hajapata huduma yeyote, Mhhh,ya dunia haya!!

KATUNI ZETU ZA LEO


NA MUSSA

KWANINI MANJI ANAUTAKA UONGOZI WA YANGA?

Shaffih Dauda in Sports.: KWANINI MANJI ANAUTAKA UONGOZI WA YANGA?: *NI KWELI ANATAKA KUIMILIKI YANGA? *NA KAMA AKIFANIKIWA KUWA MMILIKI ATAIFANYIA NINI YANGA? *KWANINI BAADHI YA WANACHAMA HAWAMTAKI? ...

POLISI WAPORA MAITI WALIOUA KWA RISASI MGODINI TARIME

JESHI la Polisi Kanda Maalumu ya Tarime na Rorya Mkoani Mara, kupitia askari wake wa FFU limelazimika kutumia nguvu pamoja na kuwatisha kwa silaha wananchi na waombolezaji wa marehemu, Mgosi Magasi Chacha (30), aliyekufa baada ya kupigwa risasi ya moto na polisi wanaolinda mgodi wa North Mara uliopo Wilayani hapa.

Sehemu ya mgodi wa dhahabu wa North Mara, unaomilikiwa na African Barrick Golds
Katika tukio hilo la leo Jumatano saa 5:10 asubuhi, polisi wakiwa kwenye magari manne huku wakiwa wamebeba silaha ikiwamo bunduki aina ya SMG, mabomu ya machozi na marungu, waliwasili kwenye hospitali ya wilaya ya Tarime kuchukuwa mwili wa marehemu Chacha kwa nguvu ili kwenda kuuzika baada ya kuwakamata baadhi ya viongozi wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) waliokuwa katika msiba huo.
Mgodi wa North Mara unamilikiwa na kampuni kubwa ya uchimbaji madini duniani ya Barrick Gold, na umekuwa katika mgogoro na wenyeji wa eneo hilo mara kwa mara hali inayosababisha kuwapo kwa matukio yanayohatarisha amani mara kwa mara.
Wakati polisi hao wa FFU waliokuwa wametanda aneo kubwa la hospitali hiyo wakitaka kuchukua mwili wa marehemu, mamia ya wananchi, ndugu wa marehemu akiwemo mkewe (jina lake halikupatikana), pamoja na viongozi wa Chadema wilaya ya Tarime, waliwazuia polisi kuuchukuwa mwili huo, wakitaka lazima taratibu za kisheria zifuatwe na si vinginevyo.
Baada ya viongozi hao wa Chadema, wananchi, ndugu na jamaa wa marehemu Chacha kuchachamaa, mke wa marehemu alikuwa akilia kwa uchungu huku akiwa amekaa karibu na mlango wa chumba cha kuhifadhia maiti, akikataa polisi kuchukuliwa mwili wa mumewe kwenda kuuzika bila ndugu na yeye kuridhia, lakini askari kanzu mmoja wa kiume alionekana kuanza kumburuza mke huyo wa marehemu kwa lengo la kumtoa eneo hilo ili polisi wachukuwe mwili huo.
Wakati mke huyo wa marehemu akiburuzwa na mmoja wa askari polisi aliyekuwa akitii amri ya mkubwa wake wa kazi (majina hayakupatikana), mwanamke huyo alikataa katakata kuondoka, lakini polisi nao walionekana kumlazimisha hadi baadhi ya nguo zake alizokuwa amejifunga zikidondoka kisha baadhi ya maeneo ya mwili wake juu ya kiuno yakiwa yanaonekana nje, jambo ambalo lilioelezwa na walioshuhudia  kama ni udhalilishaji.
Mwandishi wa habari hizi alishuhudia vurugu hizo, baina ya polisi na ndugu wa marehemu, ambapo polisi walilazimika kuweka chemba risasi za moto katika bunduki zao za SMG, baada ya kuona wametaka kuzidiwa nguvu, ambapo waliwakamata na kuwaweka ndani mwenyekiti wa Chadema wilayani Tarime, Lucas Ngoto.
Viongozi wengine wa Chadema waliokamatwa na polisi katika tukio hilo ni, Katibu wa Chadema wilaya hiyo, Mroni Mwita pamoja na diwani wa Kata ya Sabasaba, Christopher Chometa, huku mwenyekiti wa Baraza la Vijana Chadema (Bavicha), wilaya ya Tarime, Chacha Heche akiponea chupuchupu kukamatwa kwa madai ya kutaka kuzuia mwili huo wa marehemu usiondolewe hospitalini hapo kwenda kuzikwa.
Marehemu Chacha mkazi wa Kijiji cha Nkende ambaye alikuwa mwendesha pikipiki wilayani Tarime, aliuawa Juni 4 mwaka huu majira ya saa 1:45 asubuhi, kwa kupigwa risasi ubavuni kisha kutokea tumboni na askari polisi wanaolinda mgodi huo wa North Mara, unaomilikiwa na kampuni ya Barrick, na kwamba jeshi la polisi Kanda maalumu ya Tarime na Rorya imethibitisha askari wake kumuua raia huyo, bila kutaja sababu ya mauaji hayo.
Hata hivyo, baada ya vuta nikuvute hiyo iliyodumu takribani dakika 45, hatimaye polisi walifanikiwa kuuchukuwa mwili huo wa marehemu Chacha na kuuondoa nao hospitalini hapo ukiwa chini ya ulinzi mkali wa polisi, na kwamba magari yaliyokuwepo eneo hilo yakiwa yamesheheni askari ni PT 2036, PT 1873, PT 1863, T 754 BLF pamoja na pikipiki moja ya doria, huku gari la halmashauri ya wilaya hiyo SM 5241 ndilo lililotumika kuubeba mwili huo wa marehemu.
Taarifa ya jeshi la polisi Kanda hiyo maalumu, iliyotolewa na Kaimu Kamanda wa Kanda hiyo ya Kipolisi, Sebastian Zacharia-SSP ilieleza kwamba awali marehemu alijeruhiwa kwa risasi tumboni na askari polisi, kwa madai ya kumkata panga mguu wa kushoto mlinzi mmoja wa mgodi huo, Winchlaus Petro (26).
“Kabla mauti kumkuta alijeruhiwa kwa kupigwa risasi tumboni na askari polisi waliokuwa doria eneo hilo la mgodi. Marehemu alianza kumshambulia askari kwa panga na kuikata silaha ya askari huyo mara mbili hata baada ya kuonywa kwa kupiga risasi hewani wakati wa kukamatwa”, ilisema sehemu ya taarifa hiyo ya polisi yenye kurasa moja.
Mganga Mfawidhi wa hospitali hiyo ya wilaya ya Tarime, Nagga Marco ilisema, uchunguzi wake umebaini marehemu Chacha alipigwa risasi ubavuni karibu na mgongo, kisha risasi hiyo ikatokea tumboni.
Kwa upande wao familia na ndugu wa marehemu huyo, akiwemo baba yake mkubwa, Charles Matiko waliieleza FikraPevu kwamba, nguvu iliyotumiwa na polisi kuchukuwa mwili wa kijana wao ni ya kinyama, kwani familia ilikuwa haijaridhia kuchukuliwa kwa marehemu kutokana na ukweli kwamba mipango ya maziko ilikuwa haijakamilika.
Mauaji ya watu eneo hilo la mgodi wa Nyamongo, yanaelezwa kushamiri, ambapo inadaiwa mwaka jana vijana wapatao watano waliuawa kwa kupigwa risasi na polisi, Mei 7 mwaka huu kijana mwingine aliyetajwa kwa jina moja la Mwikwabe aliauawa eneo hilo la mgodi, na kwamba Juni 4 mwaka huu marehemu Chacha aliuawa pia kwa kupigwa risasi ya moto na askari polisi wanaolinda mgodi huo wa North Mara ambao unamilikiwa na kampuni ya kigeni ya Barrick.
Habari imeandaliwa na Sitta Tumma, Tarime

Chris Brown - Sweet Love

Bow Wow ft. T-Pain - Better (Official Video)

PICHA:WAZIRI MKUU AKIENDESHA BAISKEL

WAZIRI MKUU WA UHOLANZI  MH MARK MUTTE , akiwa katika usafiri wa baiskel mara baada ya kurudi kutoka kazini.je viongoz wetu wanalifahamu hili?

Birdman - Born Stunna ft. Rick Ross (Official Video)

Black Rhyno ft Suprano - Taking Over ( Official Video)

AliKiba ft Lady JayDee - Single Boy ( Official Video HD )

nShetta ft Diamond - Nidanganye (Official Video)