Dec 16, 2011

MAMBO YA KUZINGATIA PINDI UMEALIKWA CHAKULA KWA NDUGU, RAFIKI au JAMAA

Kwa maisha ya watu wengi hususani nchi zetu hizi swala la kuharikana katika mambo mbalimbali yawe ya sherehe za kuzaliwa, ndoa , komunyio, kipaimara, maulidi, hitimisho katika misiba ,na mbalimbali. lakini kwa upande wangu leo ningependa japo nizungumzie katika swala la mwaliko wa chakula nyumbani kwa ndugu, rafiki au jamaa, pindi unapopata mwaliko MAMBO YA KUZINGATIA WAKATI MNAENDELEA KUPATA CHAKULA MEZANI NI KAMA YAFUATAVYO;

1.Ni kujaribu kuzuia Usitoe comment mbaya kuhusu chakula unachokula kwani kuna mtu ametumia muda wake kukiandaa na kukipika chakula hicho .
2.punguza na ikibidi acha kuongea/maongezi ukiwa na chakula mdomoni.
3.Onyesha kufurahia chakula

4.Kama unahitaji kitu kama chumvi,bakuli ya mboga au chochote na haufikii omba usogezewe na sikupitisha mikono kwa mwenzako ambae tayari anakula.
5.Usitoe kitu mdomoni ukakiweka juu ya meza,kama ni mfupa toa mdomoni weka pembeni kwenye sahani yako.

6.Usibeue/kutoa gas kwa sauti...
7.Ukialikwa mlo kwa rafiki,ndugu au jamaa baada ya mlo shukuru na ueleze ni namna gani umefurahia chakula ulichokula unaweza ukasifu mboga kwa mfano labda "samaki alikuwa mtamu kapikwaje maana kama sijawahi kula samaki.."

hizo ni baadhi za taratibu na sheria unaweza kuzitumia pindi upatapo mwaliko wa chakula ua kujaribu kuziapply katika maisha yako ya kila siku hili upate kuzizoe na kuzifahamu kwa undani zaid, kama unachakuongezea unaweza uka comment kisha wengne nao wapate ideas juu ya swala hili la mwaliko.

No comments:

Post a Comment