Dec 19, 2011

KAFULILA afukuzwa NCCR-Mageuzi

ampigia magoti MBATIA kwa machozi, wajumbe AMPIGIA MAGOTI MBATIA KWA MACHOZI, WAJUMBE WAKATAA KUMSAMEHE
Fidelis Butahe

CHAMA cha NCCR-Mageuzi kimemfukuza uanachama Mbunge wa Kigoma Kusini, David kafulia na wajumbe wengine sita akiwamo aliyekuwa mgombea urais wa chama hicho katika Uchaguzi Mkuu wa 2010, Hashim Rungwe.Uamuzi huo ulitolewa kwenye kikao cha dharura cha Halmashauri Kuu (Nec) ya chama hicho kilichofanyika katika Ukumbi wa  Poroin jijini Dar es Salaam jana, ambao ulitawaliwa na vurugu mpaka polisi wakaitwa ili kuongeza ulinzi.
Baada ya uamuzi huo kutolewa Kafulila alikwenda kupiga magoti mbele ya Mwenyekiti wa chama hicho, James Mbatia huku akibubujikwa machozi na kuomba radhi akisema: “Naomba radhi, nimekosa mnisamehe...”


Baada ya hapo Mbatia alisimama na kumwombea msamaha  kwa wajumbe wa kikao hicho, lakini walikataa na kumweleza (Mbatia) kuwa akisamehewa watarudisha kadi zao za uanachama.“Hatutaki, Kafulila hatufai anakiharibu chama na akisamehewa sisi tutarudisha kadi zetu za uanachama ili ubaki naye kwenye chama...,” walisikia wajumbe hao wakisema kwa sauti ya juu.Wanachama wengine waliofukuzwa ni, Ally  omari, Mbwana Hassan, Josam Rugugila, Lucy Kapya, Jamwe Batifa na Hashim Rungwe ambao walikuwa viongozi wa chama hicho.


Dalili za Kafulila kufukuzwa zilijionyesha wazi juzi baada ya wazee wa chama hichi kupitia kwa Katibu wao wa Taifa, Ernest Mwasada kuitaka Nec kumfukuza (Kafulila kwa kuwa ndiye chanzo cha migogoro yote inayoendelea ndani ya chama.


















“Hizi vurugu zinachochewa na Kafulila ambaye ndiyo mfadhili na kiongozi wa waasi wa uchochezi huu. Menejimenti inapaswa kumwangalia sana, huyu ni hatari ndani ya chama hastahili kabisa kukaa na jamii yoyote inayopenda amani,” alisema Mwasada.

Hata hivyo, Kafulila juzi  alikanusha akisema kuwa madai hayo ni ya uongo na kwamba, Katibu wa Taifa wa chama hicho anateuliwa na Katibu Mkuu ambaye amekosana naye.

“Ni hivi, Katibu wa Wazee wa Chama anateuliwa na Katibu Mkuu ambaye hatuelewani na juzi alifanya kikao kilichoeleza mambo mengi mabaya dhidi yangu," alisema Kafulila na kuongeza:

“Huyo Katibu wa Wazee amelishwa maneno  na Ruhuza kwani ndiye mwajiri wake ambaye anafanya kazi maalumu ya kumchafua Kafulila na alifanya hivyo kwenye semina ya wenyeviti na makatibu wa chama 19 iliyomalizika jana (juzi) jijini Dar es Salaam.”
Kafulila alisema kazi ya Ruhuza ni kuwanywesha sumu viongozi wa chama kuwa yeye (Kafulila) ni mkorofi badala ya kuendesha semina kuhusu mambo ya msingi ya kukijenga chama.

Aliongeza kuwa, Katibu Mkuu huyo  amefikia hatua ya kutaka  ionekane kuwa wenyeviti wa chama wa majimbo ya mkoa wa Kigoma wanampinga (Kafulila), lakini kati ya wenyeviti  wanane ameambulia wawili tu ambao ndiyo anawanywesha sumu ya chuki dhidi yake.
Kikao hicho cha dharura cha Nec jana kilianza kwa wajumbe kutupiana lawama na kuzozana kwa kile walichosema, kuwapo mamluki na mipango ya kukandamiza demokrasia.

Hali hiyo iliwafanya wajumbe wenye msimamo mkali wakiongozwa na mkongwe wa chama hicho Hashim Rungwe ambaye alikuwa mgombea urais kupitia chama hicho katika uchaguzi mkuu mwaka jana, kutoka nje ya kikao.

Mmoja wa wajumbe waliokuwa ndani ya ukumbi alitoka nje na kuwaita polisi waliokuwa nje na kuwaeleza kuwa ndani kuna vurugu.
Mgawanyiko wa wazi wa wajumbe ulijikita zaidi kwenye mpasuko unaotokana na tofauti za kimsimamo kati ya Mwenyekiti wa chama hicho (Mbatia), na Mbunge wa Kigoma Kusini, David Kafulila. Inadaiwa kuwa kundi lililotoka nje ni lile linalomuunga mkono Kafulila, baada ya kuona mpango wa kupiga kura za kutokuwa na imani na Mbatia umehujumiwa.Polisi waliingia ndani ya kikao hicho wakiwa na virungu na kuwasihi wajumbe hao kufanya mkutano wao kwa utulivu.

Mbatia ashinda
Taarifa zilieleza kwamba, mvutano mkubwa ulikuwapo ndani ni wa kupinga kura za kutokuwa na imani na Mbatia kufanywa za wazi kwa wajumbe hao kusema 'ndiyo' au 'hapana' badala ya kupigwa kwa siri.

Hata hivyo upande uliokuwa unamuunga mkono Mbatia uliweza kung’ang'ania hadi hoja yao kupita ndipo baadhi ya wajumbe, wakaamua kutoka nje.
Katika kura hizo, inadaiwa Mbatia aliibuka mshindi kwa kura 40 za kuwa na imani naye dhidi ya nane zilizomkataa na mbili kuharibika. Kikao hicho kilikuwa na wajumbe 59, wakiwapo wabunge watatu wa chama hicho.

Kufukuzwa Kafulila
Kuhusu hoja ya kumfukuza uanachama Mbunge wa Kigoma Kusini, David Kafulila, wajumbe walitakiwa kuwa makini ili wasije wakakirejesha chama hicho kwenye vyama visivyo na wabunge.

Kauli hiyo ilisisitizwa na Dk Sengodo Mvungi ambaye alisema NCCR imetoka katika mazingira mabaya kisiasa kwa kutokuwa na mbunge hata mmoja, hivyo chokochoko za kumfukuza Kafulila, zinarudisha nyuma maendeleo ya chama. Naye Kafulila aliwataka wajumbe wawe watulivu na hata kama yupo kwenye mgogoro na Mbatia, wazee wa chama ndiyo wanaoweza kutumia busara kuwasuluhisha.

Vyanzo vyetu kutoka ndani ya mkutano huo vilieleza kuwa mbali na Kafulila, wanachama wengine waliotakiwa kufukuzwa ni Rungwe na makamishna wa chama hicho mikoa ya Tanga na Mwanza.

Hoja ya kundi la Kafulila lililodai kuna mamluki, ilionekana kuwa na nguvu kwa sababu Nec ya chama hicho huwa na wajumbe wasiozidi 40, lakini walishangazwa na kitendo cha wajumbe kufikia karibu 60.

Baadhi ya wajumbe waliibua hoja ya kutaka baadhi ya watu ambao hawafahamiki kutakiwa kujieleza na taratibu zitumike kuwatambua au kutowatambua.

Wakati hoja hiyo ikiwa haijapata ufumbuzi, iliibuka nyingine ya kutaka Rungwe aeleze sababu za kumwandikia barua Msajili wa Vyama vya Siasa nchini kumwarifu kuwa kikao hicho si halali.
Hadi gazeti hili linakwenda mitamboni, kikao hicho kilikuwa kinaendelea, huku vurugu kubwa ikiendelea.
Awali kulikuwa na taarifa kwamba wazee wa chama hicho walijiandaa kumtimua uanachama Kafulila kwa kile kilichoelezwa kuwa ameonyesha utovu wa nidhamu uliovuka mpaka.

Wakati hayo yakiendelea, zilikuwapo taarifa kwamba kundi la wanaomuunga mkono Kafulila, lilikuwa na mkakati wa kumng'oa madarakani Mbatia.
Kwa muda mrefu Mbatia na Kafulila wamekuwa wakitofautiana katika hoja mbalimbali ndani ya chama hicho.
Kutokana na hali hiyo, hivi karibuni, katibu wa chama

No comments:

Post a Comment