Dec 19, 2011

UKWELI KUHUSU YALIYOTOKEA UDSM WANAFUNZI 43 KUFUKUZWA

Mwishoni mwa mwezi wa nane ,bodi ya mikopo ilitoa horodha ya majina ya wanafunzi waliofanikiwa kupata mikopo,ambapo walikuwa takribani wanafunzi elfu ishirini na nne(24000).wanafunzi takribani elfu kumi na tatu (13000)walikosa  mikopo nchi nzima ilihali wengi wao walipata udahili kwenye vyuo na pia  walikuwa na sifa zote za kupata mkopo. Umoja  wa vyuo vikuu nchini (TAHLISO) ulitoa tamko kuwa wanafunzi wote waliokosa mikopo waripoti vyuoni na matatizo yao yangeshungulikiwa wakiwa vyuoni. wakiwa vyuoni wanafunzi hao ambao wengi ni kutoka familia duni, walikuwa wakikabiliwa na maisha magumu yaliyotokana na  ukosefu wa mikopo maarufu kama "NO LOAN".
  Kwa upande wa  chuo kikuu cha Dar es salaam ,takribani wanafunzi 1673 walikosa mikopo.Tulipofungua  chuo mnamo tarehe 10/10/2011 tulikuwa wanafunzi wa mwaka wa kwanza waliokosa  mikopo wakiishi maisha ya kusikitisha chuoin.Baadhi  yao walkuwa wakishinda kwa kula mlo mmoja ambao ni mkate mkavu na maji asubuhi, wengine  walikuwa wakishinda njaa  mpaka siku mbili  hali iliyopelekea kuzimia  ovyo mabwenini.Sisi tuliokuwa na mikopo tulilazimika kukatiana chapati moja wakati waasubuhi na kushirikiana chai kikombe kimoja na d=baadhi ya wanafunzi hao ili siku ziende.Baadhi ya wanafunzi waliokosa  mikopo walikuwa wamekwisha kufungasha vitu vyao na kurudi makwao baada ya kushindwa kulipa  ada na gharama nyingine za maisha chuoni.Hivyo basi tuliyokuwa tunayaona UDSM  yalitoa taswira ya  hali ya mambo ilivyo katika vyuo vingine nchini.
 






No comments:

Post a Comment