May 10, 2012

CHRIS MHINA MTOTO WA TANGA ANAYEWAPAGAWISHA WAREMBO WA SWEDEN




MwanaFA anasema mapenzi yalizaliwa Tanga! Lisemwalo lipo. Kwani hujawahi kusikia wanawake wa kitanga huweka hiriki kwenye maji ya kuoga wapenzi ama waume zao?

Damu ya kitanga imesafiri hadi katika mji mkuu wa Sweden Stockholm. Baba wa kitanga akakutana na mama wa kiswedesh wakatoa kopi ya kijana ambaye angekuja kuwa kipenzi cha mabinti. 

Christopher Augustino Eugene Fumbwe Mhina ama kwa kupunguza nguvu na muda muite Chris Mhina.

Kijana huyu ambaye ukimuona huwezi kumtofautisha na mabronzo wa B2K kwa swagga za hatari alizaliwa Januari, 3 1992.

















Nchini Sweden wanamjua sana kwa sauti yake aliyojaliwa na Mungu.

Ni mwanamuziki wa R&B ambaye Tanzania inapaswa kujivunia. Bahati mbaya kwetu wamjuao ni wachache jambo ambalo limemfanya awe upande wa Sweden zaidi. 

Kwa damu ya mama yake waswedesh wanajivunia,lakini kwa damu ya baba yake, wabongo tumezubaa! Hatujachelewa lakini kwasababu pamoja na uwezo wake wote huo,Chris ndo kwanza alitimiza miaka 20 January mwaka huu.

Ana vipajji vya ziada pia. Ukimpa mic akupe michano unaweza kusahau kama ni mwimbaji wa R&B! Ni muigizaji na dancer matata sana.

mwendapole kupitia Leotainmen imemtafuta na kumpata.Shukrani kwa Mark Zuckerberg kwa kuivumbua Facebook kwani ndiko tulikompata na kumuuliza maswali machache. Kijana hana pozi, ndani ya dakika chache akajibu maswali yetu.

Tulitaka kujua kwanza kama Baba yake ameshawahi kumleta Tanga:

“Of course, nilikuwa huko miaka miwili iliyopita, majira ya kiangazi mwaka 2010 nikiwa na baba yangu na mdogo wangu wa kiume. Ilikuwa ni safari niliyoifurahia katika maisha yangu na ndo ilikuwa safari yangu ya kwanza nje ya nchi”

mwendapole kupitia Leotainment ilitaka kujua kama anafahamu Kiswahili japo kidogo na kudai kuwa huwezi kumteta, anakijua kiasi. Kuhusu mipango ya kufanya ngoma ya Kiswahili alijibu kwa kifupi tu “You'll hear” 

Anaujua vema muziki wa Bongo Flava na anaupenda sana. Tulitaka kujua kama kuna msanii yeyote anayemkubali zaidi ambapo anasema,
“AY, he has a cool look!”

Chris Mhina amewaachia ujumbe wasanii wa Tanzania “If music is what you really want to do deep in your heart, one day all your days of hard work will pay off”. Msikilize hapa chini jinsi alivyomgaragaza Drake kwenye wimbo wake mwenyewe Marvin's room. Mcheki kwa twitter @ChrisMhina na Facebook https://www.facebook.com/christopher.mhina

No comments:

Post a Comment