Freemasonry kwa nijuavyo mimi ni shirika ambalo mambo yake ni siri
kuu. Mimi nilifanya utafiki usio rasmi kwenye mitandao, nikafatilia
historia yao kama inavyoonyeshwa mara kwa mara kwenye makala za historia
katika televisheni za magharibi pamoja na kuongea na watu waliofuatilia
kwa karibu mambo yao.
Kwenye maelezo yao kwa nje Free masons wajitangaza kama shirika zuri tu .Lakini ukweli wenyewe ni tofauti.
Naomba niorodheshe mambo machache niliyoambiwa kuhusiana na Freemasonry.
1. Ni kweli Freemasonry kama ilivyo maana yake kwanza ilkuwa ni kundi
la mafundi waashi (masons) au wajenzi kuwa lugha nyingine. Walikuwa
niwataalamu waliobobea kwenye masuala ya ujenzi wa mahekalu na mabenki
ya zama hizo zinazoitwa kwa kizungu (medieval times). Niliambiwa
walikuwa ni watunzaji wa pesa za kanisa katoliki. Kwani walikuwa
wanajenga mahekalu(cathedrals) za wakatoliki na mabenki/ mahandaki ya
kuhifadhia pesa pamoja na kuzikia(catacombs). Niliambiwa wanaweza
kujenga hayo maandaki wa utaalamu mkubwa kiasi kwamba ukiingia ndani ya
hayo mahandaki bila ramani unaweza ukashindwa kutoka hata unaweza
kupotelea humo humo ndani usiweze kutoka tena. Hicho ndicho kilichokuwa
ni kiwango cha utaalamu wao.
2. Kwa kuwa walikuwa ni waashi ndiyo maana alama zao ni vifaa vya ujenzi. Pima maji n.k
3. Inasemekana mji mkuu wa marekani (Washington DC) ulisanifiwa na
kujengwa na Freemasons. Na inasemekana ni mji makini ambao umejengwa
ukizingatia pembe tatu zenye nyuzi zinazowakilisha u freemason.
3. Ikatokea kipindi ambapo hawa freemasons wakaasi kwa kuanza
kujishirikisha na mambo ya nguvu za giza. Wengine wanasema walianza
kuiba pesa za kanisa katoliki, lakini ukweli halisi haujulikani.
Kutokana na sababu hizi na zinginezo ambazo ni siri kati ya kanisa
katoliki na freemasons, Freemasons wakafukuzwa kutoka ukatoliki. Ndio
maana hakuna maelewano kati ya freemasons na wakatoliki. Wakatoliki
wakaanzisha shirika jingine badala ya hao freemasons lijulikanalo kama
Jesuits.
Jesuit Fathers ni mapadri wa katoliki wa daraja la juu sana wenye
elimu ya juu zaidi ambao hufanya kazi za siri za utawala na udhibiti
ndani ya kanisa katoliki.
4.Kuhusu imani yao (freemasons) nikaelezwa kwa kifupi kuwa wanaamini
Yesu na Lucifer ni mtu na ndugu yake. wanaamini kuwa Lucifer ndiye mwema
na mzuri lakini wanaamini kuwa Yesu ndiye mwenye mbaya alimfanyia hila
Lucifer aonekane mbaya.
4.Kinachoendelea ndani yake kuhusiana na ibada zake ni siri kwani
kuna daraja ambazo muumini wa freemason anapanda kutokana na kubobea
katika imani ikiwa ni pamoja na kutunza siri zao. Ninajua kuwa daraja ya
juu kabisa ni nyuzi ya 33 (33rd degree)
5. Kwa hiyo ijapokuwa wanatumia biblia wanapoongelea “Bwana” huwa
hawamaanishi Yesu bali huwa wanamaanisha Lucifer ambaye ndiye
wanayemwabudu.
6. Ni watu wenye nguvu mno na mambo yao ni makubwa mno na siri zao ni
nzito mno. Ndiyo maana haziko wazi. Wafuasi wa kiwango cha chini wala
hawajui shirika hili linahusika na nini manake hata wao hawaambiwi kitu.
Kwa wafuasi wa daraja ya chini wanakwenda ku socialize tu. Yaani kwa
wasio jua kitu kule kwenye lodge zao ni kama ywca au wmca au club hivi.
Kwenye nchi kama marekani watu wasio jua siri wanachukulia kama sehemu
za kusocialize tu.
7. Freemasonry inawekwa pamoja na makundi mengine makubwa ya siri,
yanayoendesha ulimwengu mzima kwa nguvu za kiuchumi, siasa na mambo ya
utawala.
Wanacho kitabu chao cha kufundishia wanaojiunga kiitwacho “Morals and
Dogma” mwenye kuweza kusoma kizungu chake aangalie kwenye mtandao.